Ubatizo ni nini na ulio sahihi ni upi?

Ubatizo ni nini na ulio sahihi ni upi?

Bado natafuta

Senior Member
Joined
Oct 3, 2021
Posts
126
Reaction score
138
Kabla ya kufahamu ubatizo ni nini…Hebu jiulize mtu katokea na akakuuliza “kuzamisha maana yake ni nini?”..utamjibuje?…Bila shaka utamwelezea kwa kina kwamba ni kitendo cha kukitosa kitu chote kwenye kimiminika Fulani au kitu Fulani, pasipo kubakisha sehemu ambayo ipo wazi. Meli iliyopata ajali na kushuka chini ya bahari, tunasema meli hiyo imezama baharini. Mtu anayechimba shimo la taka akachimba chini sana na kuzitupa humo na kuzifukia, hapo ni sawa na kusema kazizamisha/kazizika.

Sasa mpaka hapo tutakuwa tumeshajua maana ya neno “KUZAMA au KUZAMISHA”..Sasa ukilichukua neno hilo “kuzamamisha” ukalitafsiriwa kwa lugha ya kigiriki linakuwa ni BAPTIZO…Ni sawa uchukue Neno la kiswahili “kanisa” na kulitafsiri kwa kiingereza na kuwa “CHURCH”…Vivyo hivyo Neno “kuzamishwa” likitafsiriwa kwa kigiriki linakuwa ni Baptizo..neno hilo hilo likipelekwa kwa lugha ya kiingereza linakuwa ni “IMMERSION”..na linaweza kutafsiriwa kwa lugha mbali mbali..

Kwahiyo mtu anayesema “leo naenda chachi”..ni sawasawa na mtu aliyesema “leo naenda kanisani”…neno “chachi” sio Kiswahili, na wala sio kiingereza fasaha lakini utakuwa umemwelewa amemaanisha nini kusema hivyo.

Vivyo hivyo mtu akikuambia “leo nime batizwa kwenye maji” utakuwa umemwelewa kwamba amemaanisha leo kazamishwa kwenye maji…kwa lengo Fulani.. (katumia tu msemo wa kigiriki lakini utakuwa umeshamwelewa).

Kwahiyo mpaka hapo utajua kuwa hakuna mtu atakayekuambia kwamba kabatizwa kwenye maji halafu awe “amenyunyuziwa”…Mtu aliyenyunyuziwa hajabatizwa!…kwasababu kubatizwa sio kunyunyuziwa bali kuzamishwa kabisa. (mpaka hapo tutakuwa tumeshaelewa ubatizo ni nini)

TUKIRUDI KATIKA IMANI YA KIKRISTO.

Katika imani ya kikristo, yapo mambo ambayo yanafanyika kama ishara lakini yanafunua kitu kikubwa sana katika roho. Kwamfano utaona Bwana Yesu alitoa maagizo ya kushiriki meza ya Bwana, ambapo wakristo wakutanikapo wanakula mkate pamoja na divai. Hivyo ni vyakula vya kimwili lakini vinapolika kwa maagizo hayo ya Bwana Yesu vinakuwa vinafunua vitu vingine katika roho. Kwamba ni sawa na tunainywa damu ya Yesu na Mwili wake katika ulimwengu wa roho. Na alisema mtu asiyefanya hivyo basi hana uzima ndani yake. (maana yake hana ushirika na Yesu).
Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu”.

Umeona ni agizo dogo tu, la kula chakula cha kimwili, lakini lina maana kubwa sana katika roho, sio la kulipuuza wala la kulifanya isivyopaswa…Na hapo hajasema tuonje!..bali tuule..

Kadhalika Bwana Yesu alitoa maagizo mengine yanayofanana na hayo ya watu kuzamishwa katika maji kwa jina lake(au kirahisi kubatizwa), ambapo alisema kwa kufanya hivyo katika mwili..kunafunua jambo kubwa sana katika roho, ambalo jambo lenyewe ni “kufa na kufufuka pamoja naye”
Wakolosai 2:12 “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”.

Umeona na hapo?..maana yake usipobatizwa (yaani kuzamishwa katika maji)..basi katika roho bado hujafa wala kufufuka pamoja naye…wewe bado si wake!. Vile vile kama hujazamishwa na badala yake umenyunyuziwa hapo bado hujabatizwa, unapaswa ukabatizwe tena katika maji mengi.. kwasababu ndio tafsiri ya neno ubatizo.
Hivyo ndugu mpendwa kamwe usiudharau “ubatizo”..kama bado hujaelewa kwa undani ubatizo ni nini, na umuhimu wa ubatizo tafadhali rudia kusoma tena taratibu na nakuomba chukua muda mwingi…katafute kuuliza huko na huko na pia piga magoti peke yako mwulize Roho Mtakatifu, halafu kasome biblia yako atakupa majibu.

Na ubatizo sahihi ni wa Jina la Yesu kulingana na mistari hii; Matendo 2:38, 8:16,10:48 na 19:5. Jina la Yesu ndio jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Kama hujampokea Yesu saa ya wokovu ni sasa. Kristo yupo mlangoni kurudi kuwachukua wateule wake..hivyo ingia leo ndani ya neema hii, kabla mlango wa neema haujafungwa. Yesu anakupenda na anataka kukupa raha nafsini mwako leo kama utamkubali…sawasawa na neno lake hili..

Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni lai
ni, na mzigo wangu ni mwepesi”.
 
Ngoja wale wayahudi waliokuwa wanasubiri ndege iwafikishe ughaibuni na hawakuwa na tiketi wala visa waje kudadavua kwa umakini.
 
UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?
Kabla ya kufahamu ubatizo ni nini…Hebu jiulize mtu katokea na akakuuliza “kuzamisha maana yake ni nini?”..utamjibuje?…Bila shaka utamwelezea kwa kina kwamba ni kitendo cha kukitosa kitu chote kwenye kimiminika Fulani au kitu Fulani, pasipo kubakisha sehemu ambayo ipo wazi. Meli iliyopata ajali na kushuka chini ya bahari, tunasema meli hiyo imezama baharini. Mtu anayechimba shimo la taka akachimba chini sana na kuzitupa humo na kuzifukia, hapo ni sawa na kusema kazizamisha/kazizika.
Tunaishi kwa maandiko matakatifu yanayomtaka mtu ili kuzaliwa upya ndani ya kristo na kumkiri kuwa ni Bwana na Mwokozi wa wanadamu lazima Ubatizwe kwa
Kuondolewa dhambi ya asili.

Katika Imani
Wapo wanaoamini ubatizo wa maji mengi huku ukiwa mtu mzima kwamba wewe kwa akili zako timamu umeamua kumkiri Yesu. Hili hufanyika kwa wasabato na wengineo.

Pili ni Makanisa yanayoamini katika ubatizo wa watoto wadogo mfano wakatoliki.

Zote ni imani takatifu kikubwa tunamtafuta mungu mmoja. Tuishi humo 🙏🤭
 
Ubatizo wowote ni sahihi kulingana na matakwa ya Mungu husika na makubaliano ya watu wake, mfano sisi huku kwetu unabatizwa kwa Panga na ngeu ndio alama ya wokovu.
 
Tunaishi kwa maandiko matakatifu yanayomtaka mtu ili kuzaliwa upya ndani ya kristo na kumkiri kuwa ni Bwana na Mwokozi wa wanadamu lazima Ubatizwe kwa
Kuondolewa dhambi ya asili.

Katika Imani
Wapo wanaoamini ubatizo wa maji mengi huku ukiwa mtu mzima kwamba wewe kwa akili zako timamu umeamua kumkiri Yesu. Hili hufanyika kwa wasabato na wengineo.

Pili ni Makanisa yanayoamini katika ubatizo wa watoto wadogo mfano wakatoliki.

Zote ni imani takatifu kikubwa tunamtafuta mungu mmoja. Tuishi humo 🙏🤭
Kukiri na imani vinakuwa kwenye maji/kuigeshwa/kuloweshwa/kuzamishwa mwili mzima au ni muhuri wa imani/kusadiki NENO moyoni na kwa dhati?
 
The fact that two baptized parents can give birth to a sinful child then baptism itself is nothing/nonsense.

Ubatizo ni dhana uchwara.

Ubatizo ni utambulisho wa kubuniwa tu.
 
Tunaishi kwa maandiko matakatifu yanayomtaka mtu ili kuzaliwa upya ndani ya kristo na kumkiri kuwa ni Bwana na Mwokozi wa wanadamu lazima Ubatizwe kwa
Kuondolewa dhambi ya asili.

Katika Imani
Wapo wanaoamini ubatizo wa maji mengi huku ukiwa mtu mzima kwamba wewe kwa akili zako timamu umeamua kumkiri Yesu. Hili hufanyika kwa wasabato na wengineo.

Pili ni Makanisa yanayoamini katika ubatizo wa watoto wadogo mfano wakatoliki.

Zote ni imani takatifu kikubwa tunamtafuta mungu mmoja. Tuishi humo 🙏🤭
Habari asante kwa comment yako na mchango. Kila kitu kinapaswa niende kama Neno linavyotaka.

Ulisoma uzi ukiwa bado haukukamilika kwa sasa umekamirika tafadhali rudia
 
Unaamini biblia ni kitabu cha Mungu na ndio Neno la Mungu
Kwanza huyo Mungu hayupo.

Hakuna Neno la Mungu.

Kuna Maneno ya wanadamu tu, Yanayo fosiwa na kudaiwa kwamba ni Neno la Mungu.

Biblia ni hadithi/hekaya za kutungwa sawa na hekaya za Abunuwasi, Esopo, kalume kenge na Alfu lela ulela.
 
Hapa ndipo nakiri mzungu alitumia akili sana kuiteka dunia, hasa kumteka mwafrika. Tunafanya arguments za ajabu sana, ambazo hazina impact yoyote katika maisha.

Mwisho wa siku tukifa tunaoza na ndio mwisho wa maisha ya binadamu, swala la kuoina mbingu/pepo ni muendelezo wa brainwashing ambayo mzungu alihakikisha inakubalika ili aitawale dunia vizuri.
 
Back
Top Bottom