Ubaya kwa ubaya: Club ya CD De Agosto yawalalamikia Namungo FC kudhoofisha kikosi chao

A teller

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2018
Posts
523
Reaction score
715
Club ya CD De Agosto ya Angola imetumia ukurasa wake wa instagram kulalamika kwamba Wenyeji wao Namungo FC wanadhoofisha kikosi chao baada ya kupewa majibu kuwa Wachezaji watano wa De Agosto hawawezi kucheza leo kwasababu wana Corona.

Wachezaji wa De Agosto wanaoripotiwa kuwa na Corona ni golikipa Nebi, Bobo, Boni, Mario, Mabululu pamoja na mratibu wa timu Untonesa Sampaio.

Mechi yao inachezwa leo Chamazi Mbagala Dar es Salaam ambapo De Agosto anahesabika kama Mwenyeji baada ya awali kushindwa kuchezwa nchini Angola kutokana na Wachezaji na CEO wa Namungo FC kudaiwa kuwa na Corona. #MillardAyoSPORTS
 
Huyo mabululo ndio striker wait hatar na anaongoza kwa mabao ligi yao Angola

Na wao wailaumu serikal yao haya yote yasingetokea wametufundisha wenyewe naiona namungo robo fainal kwan mechi za home lazma ashnde zote kwa mgongo wa korona
Hili swala la corona si nilisikia kuwa CAF watatumia watalamu wao wa afya kupima wachezaji ili kuondoa malamiko yanayohusiana na hujuma kwa vizingizio vya corona
 
Club ya CD De Agosto ya Angola imetumia ukurasa wake wa instagram kulalamika kwamba Wenyeji wao Namungo FC wanadhoofisha kikosi chao baada ya kupewa majibu kuwa Wachezaji watano wa De Agosto hawawezi kucheza leo kwasababu wana Corona...
Hii habari ni toka kuzi na game imepigwa jana Namungo imeshinda 6-2, Kuna watu humu nafikiri wapo longitide nyingine
 
Walidhani hawatakuja kwetu🤣🤣 this is Tanzaniaaa
 
Hii habari ni toka kuzi na game imepigwa jana Namungo imeshinda 6-2, Kuna watu humu nafikiri wapo longitide nyingine
Sasa mbona imepigwa kimya kimya.

Mimi mwenye sikuwa na taarifa!
Je unaweza nipa ka link niicheki mwanzo mwisho.
 
Club ya CD De Agosto ya Angola imetumia ukurasa wake wa instagram kulalamika kwamba Wenyeji wao Namungo FC wanadhoofisha kikosi chao baada ya kupewa majibu kuwa Wachezaji watano wa De Agosto hawawezi kucheza leo kwasababu wana Corona.

Wachezaji wa De Agosto wanaoripotiwa kuwa na Corona ni golikipa Nebi, Bobo, Boni, Mario, Mabululu pamoja na mratibu wa timu Untonesa Sampaio.

Mechi yao inachezwa leo Chamazi Mbagala Dar es Salaam ambapo De Agosto anahesabika kama Mwenyeji baada ya awali kushindwa kuchezwa nchini Angola kutokana na Wachezaji na CEO wa Namungo FC kudaiwa kuwa na Corona. #MillardAyoSPORTS
Safi sana, akikupiga shavu la kushoto wewe piga mateke kabisa. Hao wagonjwa wapelekwe mkoani Kagera wakauguzwe [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wafanye sasa kuwapeleka kwa treni moka kigoma wakalale huko huku kesho kama ndo marudiano wapandishwe basi mpaka na wacheze siku hiyo hiyo
Kabla ya mechi wawazungushe mpka kibiti then bagamoyo kisha wapige u turn mpka chamazi

Pumbavu zao
 
Sasa mbona imepigwa kimya kimya.

Mimi mwenye sikuwa na taarifa!
Je unaweza nipa ka link niicheki mwanzo mwisho.
Mwenyeji wa hii mechi alikuwa ni timu ya Angola,na hakutaka washabiki waingie wala Tv mubashara hawakutaka iwepo,kwa ujumla timu ya Angola imekula kwao!!!!!!
 
Kama ya plateau na simba sc
 
Wailalamikie Serikali yao ya Angola kwa kuwanyima fursa ya kucheza ktk nchi yao

Na Nawashauri viongozi wa Serikali yetu ya Tz hao wachezaji wa De Agosto wawekwe karantini mpaka pale tutakapohakikisha nchi ya Angola wamewaachia Watanzania wenzetu wa Namungo club
 
Back
Top Bottom