Wakuu habarini za muda huu.
Kwenye kipindi hiki cha kampeni kumezuka na kundi flani la wa hafidhina ambao wamekuwa wakidai kuwa mgombea moja amenunuliwa na mabeberu, na atatumika na mabeberu kuharibu uchumi wetu.
Baada ya utangulizi huo nilipata ukakasi kidogo juu ya hoja hiyo nikaamua kujiuliza maswali ambayo sikuwa na majibu nayo:
1. Ubeberu ni nini haswa?
2. Ni zipi faida za ubeberu?
3. Ipi misingi ya ubeberu?
4. Je, sisi Tanzania hatuwezi kuingia kwenye ubeberu?
5. Kwanini viongozi wetu wanaukataa ubeberu?
6. Je, wewe kama Mtanzania unapenda kuishi nchi za kibeberu mfano USA, UK, Dubai, South Africa na Korea Kusini? Au kiujamaa kama Korea Kaskazini ya bwana kiduku, Cuba, Russia, China, Venezuela, Ecuador na Tanzania?
Ukijaribu kunijibu maswali yote bila propaganda za siasa nitafurahi sana.