carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Serikali ya Ubelgiji imelaani kuundwa kwa muungano mpya wa kisiasa na kijeshi wa Front for the Refoundation of the Nation (FRN), unaoongozwa na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Joseph Kabila, ikieleza kuwa hatua hiyo inatia wasiwasi na haikubaliki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Maxime Prévot, amesema kuwa haikubaliki kwa kiongozi wa zamani wa nchi kuongoza vuguvugu linalolenga kupata madaraka kwa kutumia silaha badala ya njia za kidemokrasia.
Ameonya kuwa kutumia ghasia kama nyenzo ya kisiasa hakuwezi kuleta amani, utulivu wala demokrasia nchini humo.Muungano huo ulitangazwa Oktoba 12, 2026, mjini Goma, mashariki mwa DRC, ukiwa na lengo la kupinga serikali ya Kinshasa.
Unajumuisha viongozi wa makundi ya waasi, wakiwemo wa kundi la M23, huku FRN ikisema inalenga kukomesha kile inachokiita udhalimu na iko tayari kutumia njia mbalimbali, ikiwemo nguvu.Prévot amezitaka pande zinazohusika kutafuta suluhisho kupitia mazungumzo na kuheshimu makubaliano ya amani ya Doha na Washington.
Amesisitiza kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mgogoro wa mashariki mwa DRC na kwamba kuongezeka kwa mapigano kutazidisha mateso kwa raia.Hatua hiyo inakuja wakati Kabila akikabiliwa na hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama ya DRC bila yeye kuwepo mahakamani, kwa makosa yanayohusishwa na uhaini na uhalifu wa kivita.
=============
Belgian Minister for Foreign Affairs, Maxime Prévot (Les Engagés), has condemned the alliance between the former President of the Democratic Republic of the Congo (DRC), Joseph Kabila, and the M23 rebel movement.
“This is a deeply worrying development which I condemn in the strongest possible terms," said the Belgian
Foreign Minsiter. He added that it was "deplorable, incomprehensible and unacceptable" that Joseph Kabila, a former head of state who had witnessed the impact of armed rebellions, has supported a political-military movement seeking to gain power through force instead of democratic elections.
Joseph Kabila, now an opposition figure facing the death penalty for treason, has taken the helm of the Front pour la Refondation de la Nation (RFN), a new political-military movement that includes the M23.
The announcement of the alliance was no surprise, given the contacts the former president had with the rebel movement active in the east of the DRC. The Foreign Ministry is monitoring the situation closely, but so far no fundamental changes have been observed on the ground.
Sources : Brussels times