Ubepari katika siasa za kibwanyenye hapa Tanzania, ni bora ukoloni

Ubepari katika siasa za kibwanyenye hapa Tanzania, ni bora ukoloni

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Tulivyowaondoa wakoloni tulikubaliana kuwa tutakuwa huru na tukaanza kujenga siasa za ujamaa na kujitegemea! Hatukusema waliopigania uhuru watakuwa miungu watu. Makabaila na mabwanyenye!

Tulikubaliana uhuru kwa wote na usawa miongoni mwa jamii yetu. Tulikubaliana kwamba binadamu wote ni sawa. Lakini nauona ukoloni mambo Leo na ubepari wa kisiasa katika teuzi za viongozi mbalimbali katika jamii yetu. Waliopewa mamlaka ya kuteuwa kwa niaba yetu wametugeuza mateka wa wapigania uhuru ! Bahati mbaya sana wengi wetu humu hatubahatika kuishi siku angalau chache kabla ya uhuru.

Nirahisi kubeza hiki kilichopo kwakuwa kilichokuwa kinaitwa ukoloni wengi wetu tumekisoma kwenye vitabu vya historia . Dhana haikuwa hii, Bali ilikuwa ni haki sawa kwa wote! Umejiuliza ni kwanini wanateuliwa wale wale ambao ama wazazi wao au bibi na Babu zao wamewahi kuwa viongozi?

Huo ndio ubepari na ukoloni mambo Leo. Utasikia Leo Steven wasira kateuliwa kushika wadhifa Fulani! Kabla hujameza mate utasikia mtoto wa kigogo fulani kawa mkuu wa wilaya yaani viongozi chungu nzima ni ama wazazi au Babu zao wamewahi kuwa viongozi kwa namna Moja au nyingine kwa hiyo sasa wanaopewa nafasi hizo nikama kupeana fadhila na wengi hawana hata weledi wa kimantiki wa kukalia ofisi za umma! Nenda dodoma pale bungeni wengi ni waliokuwa watoto wa vigogo tu.

Ni wachache wanaovuka viunzi vya watoto wa vigogo. Katiba mpya ije itusaidie hapo kwamba mtu akistaafu hatakiwi Tena kuteuliwa. Na watoto wa vigogo wateuliwe kwa weledi sio fadhila!
 
Back
Top Bottom