- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Katika Uchunguzi uliotajwa na Jarida la MailOnline, unasema kuwa UBER wamekuwa na tuhuma hizo za kuchaji wateja bei kubwa kama simu zao ziko low Battery.
kwasababu wanajua unaharaka, na huna namna nyingine hivyo inakufanya kuwa mteja wa uhakika ambaye huwezi kukataa Bei utakayopewa.
Naomba JamiiCheck msaada wa kuchunguza hili.
Naomba JamiiCheck msaada wa kuchunguza hili.
- Tunachokijua
- Uber ni kampuni ya usafirishaji ya mtandaoni iliyoanzishwa huko Marekani inayohudumu katika maeneo tofauti tofauti ulimwenguni.
Imekuwapo taarifa ikieleza kuwa watumiaji wa Uber ambao simu zao zina asilimia ndogo ya chaji huchajiwa pesa kubwa ukilinganisha na wale ambao simu zao zina kiwango kikubwa cha chaji.
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa madai hayo kwa njia ya mtandao na kubaini kuwa madai hayo yamekuwapo kwa muda mrefu na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Uber wamekuwa wakijibu kuwa madai hayo hayana ukweli.
Tovuti ya forbes mwaka 2006 iliandika kuhusiana na suala hilo na walitumia mahojiano aliyoyafanya kiongozi wa utafiti wa uchumi wa Uber na podcast ya NPR ambapo miongoni mwa maswali aliyoulizwa ilikuwa ni kuhusiana na suala hilo la ongezeko za bei kwa watu wenye kiwango kidogo cha chaji katika simu zao. Chen alieleza kuwa ongezeko la bei huchangiwa na mambo tofautitofauti ikiwemo mabadiliko ya kimazingira mathalani uwepo wa mvua au siku za maadhimisho.
Hali hiyo huweza isiwaathiri sana watu wasio na haraka kwani wanaweza kusubiri kwa dakika kadhaa kusubiri bei ipungue, lakini hali huwa tofauti kwa watu ambao wamebakiwa na kiwango kidogo cha chaji ambapo wanaweza kulipa kiwango hiko cha ongezeko kwa kuwa wanaogopa kukwama katika eneo husika ukilinganisha na wenye kiwango kikubwa cha chaji ambao wanaweza kusubiri hadi bei itakapopungua.
Aidha tovuti ya Wkyc ilieleza kuwa madai hayo hayana ukweli ambapo wao walifanya pia majaribio kwa kutumia simu mbili zilizokuwa na kiwango tofauti cha chaji na kubaini kuwa hakukuwa na utofauti wa bei za kuitisha usafiri kwa njia ya mtandao huo kwenda kwenye eneo hilo hilo moja.
Aidha wameeleza kuwa uber katika vigezo vyao na masharti wameruhusu Application yao kuchukua taarifa za kiwango cha chaji cha simu ya mtumiaji lakini lengo si kuongeza bei ila lengo ni kuiongoza application kupunguza matumizi ya chaji iwapo kiwango cha chaji ya simu ya mtumiaji ni kidogo.