Ubinadamu Umefiwa Mlima Kilimanjaro – Ukimya wa Serikali, Manyanyaso ya Makampuni na Kilio cha Wapagazi

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Jamii nzima ya Tanzania na ulimwengu kwa ujumla mnapaswa kufunguka masikio, kufumbua macho na kusikiliza kwa makini kilio hiki kinachotoka kwenye mioyo ya wale ambao wamesahaulika – Wapagazi (porters), wapishi na magwiji wa milimani (guides) wa Mlima Kilimanjaro.

Hawa ndio watu ambao kwa mikono yao, migongo yao, na pumzi zao, wameufanya Mlima Kilimanjaro kuwa kivutio cha dunia. Hawa ndio waliochangia maelfu ya watalii kufika kilele cha Afrika. Lakini cha kusikitisha, cha kusikitisha mno – ni kwamba watu hawa wanaishi katika giza la dhuluma, manyanyaso na ukandamizaji wa hali ya juu. They are being systemically oppressed by the very institutions that should protect them.

Utumwa wa Kisasa Unaendelea Kupitia Milango ya Utalii

Ni aibu kwa taifa kuona wapagazi wakipewa mikataba ya ajabu ambayo haieleweki, haina uwazi wala haki. Mikataba hii siyo ya kazi bali ni ya kutesa na kuangamiza utu wa binadamu. Wanapewa masharti ya manyanyaso, hawapati nakala zao, hawajui hata wanachokubali kwa sahihi zao. This is psychological abuse in the disguise of “employment”.

Kuna kampuni zinawalipa wapagazi Tsh 8,000 kwa siku, pesa ambayo haiwezi hata kununua mlo wa maana katika mazingira ya kawaida, sembuse huko mlimani kwenye baridi kali, mvua, ukosefu wa hewa na hatari ya kupoteza maisha. Hii siyo kazi tu – hii ni sadaka ya maisha yao kwa taifa, na bado hawapewi heshima hiyo.

Where is the Ministry of Natural Resources and Tourism?

Wizara ipo kimya. Haijishughulishi. Hakuna framework ya kulinda hawa watu. Hakuna auditing ya haki zao. Hakuna uwajibikaji kwa makampuni ya kitalii ambayo yanafaidika kwa mamilioni lakini yanawaminya wapagazi mpaka tone la mwisho la jasho.
This silence is criminal. This negligence is wicked. This is systemic violence wrapped in silence.

Wapagazi Hawana Kinga, Hawana Sauti, Hawana Haki – Lakini Tunaweza Kuwapa Sauti

Serikali mko wapi? Wizara ya Kazi mpo wapi? Halmashauri za mkoa wa Kilimanjaro mpo wapi? Huu ni wakati wa kuacha kusimama pembeni kama watazamaji wa sinema ya mateso. Wapagazi wanahitaji:

Mikataba ya haki yenye uwazi

Malipo ya heshima yanayoendana na mazingira magumu ya kazi

Bima za afya na maisha

Makampuni ya kitalii kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara (labour audit)

Uundwaji wa chombo huru cha kutetea na kusimamia haki za wapagazi (Porters Union)

Enough is Enough!

Wapagazi si watumwa wa utalii. Ni sehemu ya urithi wa taifa. They are custodians of our national pride. Ukiona mtu amefika Uhuru Peak, fahamu kuna mtu alilala kwenye barafu, alibeba kilo 25 kwa mguu, bila chakula cha kutosha, bila hewa ya kutosha, bila kinga ya afya. That man is a porter – and right now, he is crying for help.

Kama taifa tumeishiwa huruma, basi tumeishiwa kila kitu. Kama serikali haina uwezo wa kuwalinda watu wake wanaofanya kazi hatarishi kwa heshima, basi hatustahili kujivunia Kilimanjaro.
 
Attachments

  • F00dpOSWYAAj0vH.jpeg
    F00dpOSWYAAj0vH.jpeg
    294.4 KB · Views: 49

Serikali ya CCM haiwezi tetra mfanyakazi yeyote isipokuwa maslahi yao
 
Mama Karen wa KPAP? Kajiungeni huko muache kulia lia, the problem is demand and supplies, mpo wengi sana, na ajira ni issue, Gharama ni kubwa sana, pakubana ni kwenu mara nyingi!

Hakuna siku serikali itawasaidieni, maana gharama za ku run hizo biashara ni nyingi sana, na serikali inakusanya haswa, sasa mfanya biashara anafanyaje?

Yeye anatoa wapi pesa kulipa wakati na yeye kabanwa hivyo hivyo kama wewe? Ni kujiongeza, kutafuta mtaji au kujiendeleza na kufanya mambo mengine!

Ukombozi ni initiative binafsi!
 
Jamii nzima ya Tanzania na ulimwengu kwa ujumla mnapaswa kufunguka masikio, kufumbua macho na kusikiliza kwa makini kilio hiki kinachotoka kwenye mioyo ya wale ambao wamesahaulika – Wapagazi (porters), wapishi na magwiji wa milimani (guides) wa Mlima Kilimanjaro.

Hawa ndio watu ambao kwa mikono yao, migongo yao, na pumzi zao, wameufanya Mlima Kilimanjaro kuwa kivutio cha dunia. Hawa ndio waliochangia maelfu ya watalii kufika kilele cha Afrika. Lakini cha kusikitisha, cha kusikitisha mno – ni kwamba watu hawa wanaishi katika giza la dhuluma, manyanyaso na ukandamizaji wa hali ya juu. They are being systemically oppressed by the very institutions that should protect them.

Utumwa wa Kisasa Unaendelea Kupitia Milango ya Utalii

Ni aibu kwa taifa kuona wapagazi wakipewa mikataba ya ajabu ambayo haieleweki, haina uwazi wala haki. Mikataba hii siyo ya kazi bali ni ya kutesa na kuangamiza utu wa binadamu. Wanapewa masharti ya manyanyaso, hawapati nakala zao, hawajui hata wanachokubali kwa sahihi zao. This is psychological abuse in the disguise of “employment”.

Kuna kampuni zinawalipa wapagazi Tsh 8,000 kwa siku, pesa ambayo haiwezi hata kununua mlo wa maana katika mazingira ya kawaida, sembuse huko mlimani kwenye baridi kali, mvua, ukosefu wa hewa na hatari ya kupoteza maisha. Hii siyo kazi tu – hii ni sadaka ya maisha yao kwa taifa, na bado hawapewi heshima hiyo.

Where is the Ministry of Natural Resources and Tourism?

Wizara ipo kimya. Haijishughulishi. Hakuna framework ya kulinda hawa watu. Hakuna auditing ya haki zao. Hakuna uwajibikaji kwa makampuni ya kitalii ambayo yanafaidika kwa mamilioni lakini yanawaminya wapagazi mpaka tone la mwisho la jasho.
This silence is criminal. This negligence is wicked. This is systemic violence wrapped in silence.

Wapagazi Hawana Kinga, Hawana Sauti, Hawana Haki – Lakini Tunaweza Kuwapa Sauti

Serikali mko wapi? Wizara ya Kazi mpo wapi? Halmashauri za mkoa wa Kilimanjaro mpo wapi? Huu ni wakati wa kuacha kusimama pembeni kama watazamaji wa sinema ya mateso. Wapagazi wanahitaji:

Mikataba ya haki yenye uwazi

Malipo ya heshima yanayoendana na mazingira magumu ya kazi

Bima za afya na maisha

Makampuni ya kitalii kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara (labour audit)

Uundwaji wa chombo huru cha kutetea na kusimamia haki za wapagazi (Porters Union)

Enough is Enough!

Wapagazi si watumwa wa utalii. Ni sehemu ya urithi wa taifa. They are custodians of our national pride. Ukiona mtu amefika Uhuru Peak, fahamu kuna mtu alilala kwenye barafu, alibeba kilo 25 kwa mguu, bila chakula cha kutosha, bila hewa ya kutosha, bila kinga ya afya. That man is a porter – and right now, he is crying for help.

Kama taifa tumeishiwa huruma, basi tumeishiwa kila kitu. Kama serikali haina uwezo wa kuwalinda watu wake wanaofanya kazi hatarishi kwa heshima, basi hatustahili kujivunia Kilimanjaro.
Nyie ndio wale wa tupazieni sauti? Hamjui jinsi ya kujitetea? Tuendelee na huu uzezeta wetu basi.
 
mkuu unajua kama ofisi za porters ukienda pale labda kukata kitambulisho cha upagazi wanakuelimisha adi malipo yako yanatakiwa yasiwe chini ya 25k?
shida ipo kwa wapagazi huwa wanaambiwa mkiona kampuni inalipa chini ya 25k mtujulishe just piga simu na msipande kwanza mlima kabla ya makubaliono ila kama unavyotujua sisi wabongo kwa kulalamika tupo vyema ila vitendo aaahka.. hi inakuwa ngumu kujua kama kuna wapagazi wananyanyasika.
Na porters association ukisema wakaze kabisa ile serious niamini mimi wapagazi watakaofuzu kupanda huo mlima watakuwa wachache sana ka maana ya kuwa na mountain gears zote zinazoitajiwa sema ndo hivyo ni kubebana bebana.
 
hivyo nidhahiri kabisa shida ni ubinafsi yaani wewe ukisema bila 25k huendi mimi natia mzigo begani nakata njia (tatizo ubinafsi)

Kubebana pia tatizo nikweli inawapa fursa wenye kazi zao (ukibebwa bebeka)
 
Bora media watamuliwe maana kazi hawazijui
Wengine wanamualika mchekeshaji aje awachekeshe redioni huku watu wanataabika

Media ingefunguka zaidi kama kina Ayo wangeenda huko na kuwaweka mtandaoni basi lazima wakubwa wangejitokeza

Mwafrika hana aibu wala soni, ila ni muoga
 
hivyo nidhahiri kabisa shida ni ubinafsi yaani wewe ukisema bila 25k huendi mimi natia mzigo begani nakata njia (tatizo ubinafsi)

Kubebana pia tatizo nikweli inawapa fursa wenye kazi zao (ukibebwa bebeka)
Tatizo hawajui hizo kazi ndio zimetupa mitaji! Pesa ndogo ndio zinalipa
 
mimi nlipanda mwaka jana na kampun x walikuwa wanalipa 10k ila guide mkuu alikuja tuambia siku ya 3 kwamba mnajua hii kazi mnalipwajwe? ase nlilegea baada ya kusikia ni 10k na tulipitia machame gate lakini mungu ni mwema mboneka ilitoka dola 100 mia kwa kila mgumu..
ile kazi siwez sahau siku saba zote ilikuwa ni mvua mwanzo mwisho afu msos ulikuwa wa shida na mzigo ni ngaa yaan nlipata hasira na nliapa siku napanga huu mlima tena nitapanda kama guide na si kama mgumu.. nashukuru mpaka sasa nimepiga kazi kama 4 kama guide
 
Back
Top Bottom