Ubinadamu unapo ingia kwenye maslahi ya wakubwa, na kupelekea tafrani

Ubinadamu unapo ingia kwenye maslahi ya wakubwa, na kupelekea tafrani

Episode 2.

Akiwa Moscow akakata kabisa mawasiliano na makachero wa MI6 Alitumia muda mwingi akijifunza kiingereza na pia akikusanya taarifa nyeti za uingeleza na kuwapa mabosi wake ambazo alidai amezipata kutoka kwa watu aliowapandikiza uingeleza.

Kihalisia taarifa zile alikuwa akizipata kwenye open sources kama magazeti nk Taarifa zile kwa lugha ya kijasusi ziliiywa “Chicken feed” kwani hazikuwa na athari mbaya kwa serikali ya Uingeleza. Kutokana na jinsi alivyokuwa akitoa taarifa ambazo wakuu wake waliamini ni “intell” kutoka Uingeleza, aliwashawishi wakuu wake na mwezi june mwaka 1982 Sunbeam akapangiwa kazi ubalozi ya urusi nchini uingeleza.

Naam! Kachero wa Urusi akawa rasmi jijini London akifanya kazi za MI6 Urusi ikiamuamini sasa mtu wao kama “Resident Designate” Hii tunaiita kitaalamu “Home and Away” Alipofika Uingeleza akawashawishi maafisa wa MI6 kupitia wizara yao ya mambo ya nje wafanye juu chini kuwakataa mabosi wake waliopo Ubalozi ili yeye awe bosi aweze kufanya kazi vizuri.

Hili lilifanyika hatua kwa hatua na Sunbeam akajikuta anapandishwa cheo cha Kanali na kufanywa mkuu wa KGB nchini Uingeleza. Naam! Hata maafisa wa MI6 wakambadilishia jina lake la uficho la SUNBEAM Sasa aliitwa kwa jina la uficho la NOCTON na sio SUNBEAM tena Huku CIA sasa wakimuita kwa jina la uficho la TICKLE.
Kazi ya kwanza aliyofanya akiwa London ni kumsanua aliyekuwa anatarajiwa kuwa mgombea wa uwaziri mkuu kupitia chama cha Labor Party bwana Michael Foot kuwa ni mtu aliyekuwa akilipwa na Serikali ya Urusi kufanya ujasusi dhidi ya Uingeleza.

Huyo alikuwa ni Mbunge na Kiongozi wa chama cha Labor. Kachero huyu aliwapa taarifa zile Makachero wa MI6 ambao walisubiri kwanza waone mwenendo wa uchaguzi kama anaelekea kushinda ndio wamlipue kulinda Maslahi ya Uingeleza. Lakini tatizo hili lilijitatua lenyewe kwani waziri mkuu Margaret Thatcher alishinda uchaguzi na Michael foot akalazimishwa kujiuzuru. Kachero huyu alitoa taarifa nyingi na nyeti juu ya mipango ya KGB Lakini alikuja kufanya kazi moja nzuri sana kwa wapenda amani wakati wa Vita baridi. Kwanza taarifa zake zilikuwa zinawafanya rais Reagan na waziri Mkuu Margaret kupunguza makali ya sera zao dhidi ya urusi baada ya kuwahakikishia Urusi haikuwa hostile kama walivyoichukulia.

Kisha akafanikiwa kuwachezesha mziki katika tune moja aliyekuwa rais wa Urusi Mikhail Gorbachev na waziri mkuu Thatcher. Wakati ule mwaka 1984 Gorbachev alikuwa ni katibu mkuu wa chama cha Kimomunisti cha Communist Party na alipanga kuzuru Uingeleza. Kwakuwa sasa NOCTON alikuwa ndiye jicho la KGB nchini Uingeleza, akatumwa akusanye details zote za muhimu kabla na wakati wa Ziara hiyo.
Kwa ufupi ni mashushushu wa Uingeleza ndio walikuwa wakimpa Mole wao taarifa hizi naye akawa anaipa timu ya Gorbachev.
Aliweza hata kutabiri mazungumzo yatakayofata yatahusu nini alivyoamuliwa kufanya hivyo kwa kuwa MI6 walikuwa wanamueleza kila kitu kwa upande wa waziri wao Mkuu. Aliweza hata kumshauri Gorbachev aongee nini wakikutana na Thatcher na hivyo hivyo aliwashauli MI6 wamwambie Thatcher mambo yatakayomfurahisha Gorbachev.

Kazi hii nzuri ilifanikisha sana kubadili mtizamo wa Marekani na Uingeleza dhidi ya serikali ya Kijamaa ya Urusi na ukawa ndio mwanzo wa kuisha kwa vita baridi. Mwaka 1985 haukuwa mzuri kwa Jasusi huyu ambaye si vibaya sasa tukimfahamu kwa jina lake halisi.

Jasusi huyu si mwingine bali ni Oleg Gordievsky Kama una kumbukumbu nzuri kulikuwa na Jasusi wa CIA bwana Aldrich Aimes aliyekuwa anauza siri za CIA kwa Urusi. Ni jasusi huyu ndiye aliwatonya KGB kuwa mtu wanayemuamini sana jijini London ndiye anayewauza. Kwamba mtu huyu ana jina la uficho la TICKLE Kichomi huyu wa CIA akaeleza baadhi ya taarifa walizouziwa na TICLE Kwa maelezo yake, Maafisa wa KGB wakabaini kuwa huyu TICKE si mtu mwingine bali ni Oleg Goldievsky Haraka sana wakaitwa arudi nchini Urusi mwaka huohuo wa 1985 Kachero huyu akajua lazima inawezekana mambo yatakuwa yameharibika Maafisa wa MI6 wakamtaka akatae kurudi Urusi na wao watampa ulinzi. Lakini jamaa alikataa na kusema ngoja akajue walichomuitia.
View attachment 2918146
I will be back, I mean no malice to nobody
Mkuu hii stori ishawahi kusimuliwa ila simkumbuki msimuliaji tu nilipoona jina la NOCTON ndo nikakumbuka

Ni ndefu kweli yani ila humu jf ishawahi kusimuliwa
 
Back
Top Bottom