SoC01 Ubinafsi ndio chanzo cha tatizo la Ajira

SoC01 Ubinafsi ndio chanzo cha tatizo la Ajira

Stories of Change - 2021 Competition

kipenseli2021

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2021
Posts
1,390
Reaction score
1,431
Ongezeko la idadi kubwa ya vijana wanao maliza vyuo vikuu,vya kati na vyuo vya ufundi umepelekea kuleta change moto ya ukosefu wa ajira katika Taifa na Dunia

Serikali na wadau mbalimbali ikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali wametoa na kuendelea kutoa mchango waho juu ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira katika Taifa letu jambo ambalo limekuwa kero na huzuni miongoni mwa vijana wanao maliza vyuo katika ngazi mbalimbali

Pia tumeshuhudia wanasiasa wakitumia changamoto ya ajira kwa vijana kama ajenda yahoo kipindi cha uchaguzi au pale wanapo taka nafasi Fulani ya kuchagulia kwenye uongozi

Pia tumeona hata baadhi ya vijana hususani wa kike kuingia katika utumwa au majaribu ya kutumiwa kigono ili waweze kupata nafasi ya ajira

Matapeli pia awajabaki nyuma katika kutumia mwanya huu kuweza kujipatia pesa toka kwa kundi la vijana

Nukuu fupi

” nilipo maliza chuo nikaanza kuangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu ikabidi niombe familia iweze kunichnagia mtaji nijiajiri mwenyewe ,basi nashukuru wakanichangia mtaji baada ya siki chache nilipo kabidhiwa fedha walizo nichangia,ghafla nikaona rafiki yangu wa muda niliyo soma naye ananipigia simu na kuniambia kuwa kuna mtu amemwaidi kutupatia kazi ila tuna bidi kumlipa,basi kwa kuwa tayari nina pesa walizo nichangia ikabidi niweze kumlipia rafiki yangu na mimi mwenyewe ili tupate kazi,tukafanikiwa kumlipa Yule jamaa baada ya hapo akaanza kutupiga kalenda yani kutuzungusha miezi inakwenda tukiwa na matumaini ya kupata kazi lakini wapi kuja kufuatilia kumbe Yule jamaa ni tapeli na amesha tuzungusha zaidi ya nusu mwaka tukiwa na shauku ya kupata ajira ndoto ya ajira kwa mwaka huu ikaishia hapo”

Ndizo stori za vija wengi na wengine hadi wakikusimulia basi unaweza ukatoka na machozi

“JE LAKINI WAJUA TATIZO HILI LINACHNAGIWA NA UBINAFSI”

Na kama tukiondoa ubinafsi kuanzia ngazi ya familia na kuendelea tutaweza zaidia vijana wengi sana na tutapunguza uchungu huu tunao upitia vijana,kabla sijaeleza ni kwa namna gani UBINAFSI unachnagia tatizo ili nikukumbushe kisa cha vijana wa MOROCCO waliokuwa wanajitia mafuta “petrol” na kujiwasha moto sababu ya wakilalamika ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira

Ubinafsi(Individualism) ni tabia ya kujipendea mno hata kutojali wengine na shida zao

JE KWA NAMNA GANI TUKIACHA UBINAFSI TUTAWEZA TATUA CHANGAMOTO YA AJIRA

  • Serikali/idara/wizara na vitengo vyake v ingeweza kutoa nafasi kwa vijana ambao si waajiriwa kwa mfano pale wanapo taka Mifumo ya Mawasilano,Nembo(Logo),Mawazo ya kibiashara,Michoro ya majengo na madaraja na baadhi ya mambo ambayo si lazima yafanywe na ma afisa walioajiriwa pasipo kuadhiri utendaji kazi wa serikali,basi ingekuwa inakaribisha au kuandaa mashindano kwa kuwakaribisha vijana wenye ujuzi husika kuweza kufanya kazi hizo na kuwapatia zawadi ambazo zingewasaida kuweza kujiimarisha .
  • Kupokea na kuyafanyia kazi mapendekezo mbali mbali ya ubunifu kwa uaminifu baadhi ya vijana wanaogopa kupeleka mapendezo ya ubunifu /biashara kwa sababu ya kuhofia kubaniwa au kutumika kazi zao pasipo kufaidika ivyo serikali ikaandaa utaratibu wa kupokea mawazo au mapendekezo ya vijana na kuyanunua
  • Pia makampuni binafsi,mabenki na mashirika yasiyo ya kiserikali nayo yangekuwa na utaratibu wa kurudisha kile wanacho kipata kwa mwaka kwa jamii na vijana kupitia kuandaa mashindano mbalimbali ya kununua ubunifu wa vijana au mawazo ya vijana na kuyafanyia kazi katika mashiriaka au makampuni yao,lakini kwa hapa kwetu imekuwa ngumu makampuni makubwa sababu ya “UBINAFSI” yanashindwa kuandaa mashindano kama hili la jamii forum ili vijana waweze kupata pesa na kujiajiri
  • Pia serikali iweke utaratibu wa lazima kwa kila kampuni ndani ya mwaka mmoja basi iandae kitu ambacho kitashindanisha vijana au makundi ya vijana katika kutoa ubunifu na mawazo ya biashara na kuwapatia zawadi ambazo zingewasaidia ili waweze kukua au kupata mtaji wa kuendeleza mawazo yaho
  • Pia vyuo navyo viandaee utaratibu wa kutoa pesa/mtaji kwa vijana ambao wamefanya project nzuri ili waweze kuzifanyia kazi wanapo maliza vyuo,tumeona project nyingi nzuri na mawazo mengi mazuri ya miradi yameishia kurundikwa katika maabara/karakana na maktaba ya vyuo lakini wameshindwa kuwasaidia vijana kuyatimiza yote sababu ya “UBINAFSI”
  • Pia bodi ya mikopo iwe inatumika katika kuwezesha mawazo ya vijana pindi tu wanapo maliza basi kila chuo kichague vijana wenye mawazo na ubunifu waweze patiwa mkopo na bodi ya mkopo
  • HITIMISHOTuwekeze katika mawazo ya vijana na pia tusifunge milango ya ofisi zetu ili kupokea mawazo ya vijana kwani “TUMEAJIRI WATU BORA NA TUMEWAACHA WATU BORA
Asante na pole sana ila nina imani kuwa tukiacha ubinafsi basi tutaweza kutatua tatizo ili la ajira kwa asilimia Fulani

Imeandikwa na mimi hapa kipenseli
 
Upvote 3
Ubinafsi huo ndio Mara nyingi hupelekea kuzorota hata kwa utendaji wa maofisa wa serikali,kamlete kamlete hiyo...
 
Back
Top Bottom