Bromensa
Member
- Jan 3, 2024
- 28
- 38
Uchaguzi unapaswa kuwa njia ya kidemokrasia ya wananchi kuamua viongozi wao kwa misingi ya sera na utendaji wao. Kiongozi akishindwa kutimiza ahadi zake, hapaswi kuchaguliwa tena. Lakini je, hilo linatokea kweli?.
Tatizo ni kwamba ujinga, umasikini na ubinafsi vimetufanya kuuza haki yetu kwa bei rahisi. Watawala hutumia ujinga, umasikini na ubinafsi wetu kutunyonya; wanatoa kilo ya mchele, pesa kidogo, au ahadi za kuleta maendeleo ambazo hazitekelezwi, nasi tunakubali kwa sababu ya njaa ya leo tukisahau mateso ya kesho.
Hii ni hila inayotufanya kuwa watumwa wa kisiasa. Tunaendelea kulalamika, lakini hatuko tayari kupigania mabadiliko. Tutaendelea kuuza maisha yetu kwa vipande vya fedha au tutaamka na kudai haki yetu?. Kila mtu anatamani kuona mabadiliko lakini hakuna aliyetayari kuyapigania.
Tuna taifa ambalo limejengwa kwa msingi ya kujipendekeza, watu wanajiunga na mfumo sio kwa sababu ya kuleta maendeleo bali kupata urahisi wa kupata chakula.

- Watu wanaounga mkono watawala kwa sababu wanapata faida binafsi, kama vyeo, mikataba ya kibiashara, au upendeleo wa kisiasa.
- Baadhi ya watu hukubaliana na watawala kwa sababu wanahofia kupoteza kazi, biashara, au ushawishi wao endapo mfumo utabadilika.
- Baadhi ya watu huunga mkono chama au kiongozi fulani, hata kama anawaumiza, kwa misingi ya udugu, ukabila na udini badala ya kutathmini uongozi wake kwa misingi ya utendaji na maslahi ya taifa