Ubinafsi, uroho na tamaa za watawala sheria ya mafao kustaafu katika utumishi wa kisiasa

Ubinafsi, uroho na tamaa za watawala sheria ya mafao kustaafu katika utumishi wa kisiasa

Hongera kwa uchambuzi mzuri.

Kumbe hawa jamaa wanakunja noti kias hiki?

Af wanaishia kugonga meza
 
Hawa wanyonya damu hawataacha kupeleka bungeni miswada yenye kujineemesha wao katikati ya lindi la umasikini wa wengi huku wakija na mapambio ya uzalendo bila kuwakemea na kuwapigia makelele na kukataa hila zoo hakika watafanya watakavyo hatuna budi kupaza sauti na kukemea.
 
Kwani huu mmuswada hata ukiwa sheria mpya ya mafao itamgusa mama Salma? Si huwa mnasema sheria hairudi nyuma( not retrospective)??.

Yaani, itaanza kutumika kwa watakaokuwa marais baada ya sheria kuanza kutumika. Mnisaidie mm wa huku Mbwinde.
 
Nchi ngumu sana hii, walimu wanalia mishahara ni mibovu haitoshelezi mahitaji ya kila siku alfu kuna mtu analipwa pesa nyingi zote hizo na bado anataka zaidi 😀😀😀
 
Naam ubaya ubaya tuu. Acha wazidi kutunyonya
 
Nchi ngumu sana hii, walimu wanalia mishahara ni mibovu haitoshelezi mahitaji ya kila siku alfu kuna mtu analipwa pesa nyingi zote hizo na bado anataka zaidi 😀😀😀
Binadamu kaumbwa na upekee wake wa ubinafsi.Kila kizuri anataka yeye tu.
 
MWANACCM MZALENDO WA KWELI NA MWENYE UCHUNGU NA NCHI HII RASLIMALI ZAKE NA WANANCHI WAKE ALIKWISHA KUFA AMBAYE NI HAYATI BABA WA TAIFA MWL.NYERERE
Wengine wote licha ya kuwa ni WANACCM HAWANA UZALENDO na NCHI HII wala RASLIMALI ZAKE
Wamejiwekea KINGA ili WAKIFANYA UFISADI wasishtakiwe
Wanajirundikia MAFAO huku WALIMU na WATUMISHI wengine wakihaha
Wananchi ni Umasikini wanatembea nao
 
Muswada unapendekeza kiongozi aliyeshika nafasi ya ofisi ya Rais na kustaafu, mwenza wake atapata 25% ya jumla ya mshahara wa mwenza wake alipokuwa ofisini.

Muswada unapendekeza; familia ya Rais Mstaafu itapata mafao yake kila mwezi ambayo ni sawa na 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani
Serikali ya CCM kwa awamu karibu zote zimejaa ubinafsi uliokubuhu, umimi na ubadhirifu ulivuka mipaka!
Hawataki kuona japo wafanyakazi wengine tena waliotumikia Taifa kwa muda mrefu nao wakipata mafao mazuri.
Pamoja na ufisadi mkubwa wanaofanya na uharibifu wa raslimali za nchi badi hata kile kidogo wanataka tena kukikomba!
Mungu wetu yupo kama ni halali.
 
Chalinze na hilo.jimbo la Mchinga linanuka umaskini. Nakumbuka wakati wa JPM Rizmoko alimuomba maji Jiwe alimjibu Baba yako amekuwa rais miaka yaote hukuwaletea maji kwanini hukumuomba waletewe maji hawa wananchi.
 
Serikali imepeleka bungeni muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ambayo kuna marekebisho katika sheria 10 ikiwepo sheria ya mafao ya kustaafu katika utumishi wa kisiasa.

Muswada unapendekeza kiongozi aliyeshika nafasi ya ofisi ya Rais na kustaafu, mwenza wake atapata 25% ya jumla ya mshahara wa mwenza wake alipokuwa ofisini.

Muswada unapendekeza; familia ya Rais Mstaafu itapata mafao yake kila mwezi ambayo ni sawa na 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani

Salma Kikwete ni mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Tanzania, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete.

Salma Kikwete ni mama wa Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

April 22, 2022 katika Bajeti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. 2022/23 Salma Kikwete alipendekeza mafao ya wake wa Marais wastaafu

Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Naibu Waziri ni Ridhiwani Kikwete, hoja hiyo sasa imepelekwa bungeni

Muswada umewasilishwa 8/9/23 na Spika wa Bunge na ameupeleka kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa ajili ya kuchambuliwa

Salma Kikwete na wake wa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu watalipwa pesa za kiinua mgongo kwa sababu tu walikuwa wake wa vigogo.

Salma Kikwete ni mwalimu kitaaluma. Hakuona tija kutetea mafao ya walimu wenzake au watumishi wa umma, akatetea “wenza wa vigogo”.

Salma Kikwete, akimaliza miaka yake mitano ya ubunge wake jimbo la Mchinga atalipwa Sh230M kama kiinua mgongo chake.

Kiinua mgongo cha Sh230 milioni analipwa kwa kuwa mbunge wa Mchinga. Bado kiinua mgongo atacholipwa kwa kuwa mke wa Kikwete

Mshahara na marupurupu ya mbunge nje ya posho na kujikimu ni Sh16.5M kwa siku 30. Kwa mwaka, mshahara ni Sh198M.

Mbunge miaka 5, mshahara wake ni Sh990M. Kiinua mgongo kwa kila mbunge ni Sh230M. Salma Kikwete (mbunge) atakusanya hizo.

Salma Kikwete analipwa posho ya kujikimu (perdiem) Sh250,000 kwa siku. Ukijumlisha na posho ya kitako Sh220,000 anakunja Sh470,000 kwa siku moja bungeni

Rais Mstaafu hulipwa posho ya kila mwezi 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani. Kiasi hicho ni sawa na Sh80 kwa kila Sh100 anayopata Rais aliyepo madarakani

Pamoja na malipo ya mkupuo anayopata Rais mstaafu, anapewa pasi ya kusafiria yenye hadhi ya kidiplomasia, pamoja na mke wake na mume wake.

Rais Mstaafu na mke wake wanalipiwa gharama za matibabu ndani au nje ya nchi. Bado Salma Kikwete akaona haitoshi akaomba apewe mafao ya kuwa mke wa Rais

Rais Mstaafu anapewa walinzi, msaidizi, katibu mukhtasi, mhudumu wa ofisi, mpisho, dobi, mtumishi wa ndani, mtunza bustani, madereva wawili

Rais Mstaafu analipiwa matengenezo ya magari mawili yenye uzito usiopungua tani tatu, ambayo hutolewa na serikali, ambayo pia hubadilishwa baada ya miaka mitano

Rais Mstaafu pia hujengewa nyumba mpya, ambayo ni LAZIMA iwe na angalau vyumba vinne, viwili kati ya hivyo LAZIMA viwe na huduma zote ndani (self-contained rooms)

Nyumba hiyo LAZIMA iwe na ofisi iliyokamilika na nyumba kwa ajili ya mfanyakazi wake. Na gharama za mazishi zitagharamiwa na serikali

Mume amekuwa Rais miaka 10 na mbunge wa Chalinze. Amekuwa waziri kwa miaka 10. Ametumikia uwaziri tangu mwaka 1995 hadi 2005 alipokwenda kuwa Rais.

Mtoto wa Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amekuwa mbunge wa Chalinze tangu mwaka 2014 (baba yake akiwa Rais)

Tembelea majimbo ya Mchinga na Chalinze ambayo wamegawana kama mali za urithi. Wananchi wake ni maskini wa kutupwa. Hawana huduma stahiki za kijamii

Watanzania kwa mamilioni wanakosa huduma muhimu za kijamii kama afya na njaa imetawala, watawala wastaafu na wake zao wanajirundikia miposho

Hawa watu wanajineemesha kwa marumbesa ya pesa na familia zao. Siyo rahisi kuwapa njia ya kutoa katiba mpya. Wanajua Katiba Mpya itaondoa huu urasimu.

Lazima mtu timamu aone sababu za msingi za kudhibiti mambo haya kwa kuyawekea utaratibu mzuri.
Kama kuna familia yenye majizi na ya kijambazi ni hii ya kikwete, haina tofauti na ya Uhuru Kenyatta kule Kenya
 
Back
Top Bottom