Ubinafsi wetu wanawake ndio chanzo cha wanaume kutuumiza

Ubinafsi wetu wanawake ndio chanzo cha wanaume kutuumiza

Mwanaume unaweza kuihudumia familia mda wote ,kama hamna kitu ndani mwanamke anaagiza tu ,hata awe na hela utakuta hata chumvi hanunui. Ikitokea huna hela haelewi zaidi atafanya mambo yake binafsi.
Hao viumbe Wana roho mbaya Sana,sio wakuwatendea wema kabisa kabisa
 
1. Hakumpenda

2. Alimjeruhi

Mwanamke akikupenda atakuwa tayari kwa lolote ili akustiri.

Ila sio haki kuchukulia mfano wa mwanamke mmoja kuhukumu wote!!!
 
Nina shost yangu ni mfanyabiashara mzuri tu wa nafaka na anaingiza faida nzuri kwa sasa.
Ana mtu wake ambaye alisimama bega kwa bega kuhakikisha anafika hapo alipo. Huyo mtu wake kipindi hicho aliamua kuwekeza akili, mawazo na hela kwaajili ya kuhakikisha mpenzi wake anasimama kibiashara. Kweli bi shost wangu alifanikiwa kufikia malengo kwa msaada wa huyo shem.


Lakini kile chakula kikubwa cha Usiku si huwa anampa??--- ili kumliwaza!!🤣
 
Ntachangia nondo milimita 20...na mchanga Lori kubwa
Sanamu Yako Tunaijenga Wapi Nataka Nitangaze Tender Kwenye Gazeti. Tafadhali Taja Mkoa Wilaya Kata Tarafa Kijiji!!
Ukishindwa Kabisa Mimi Kwakuwa Natoa Cash
Nitapenda Ijengwe Msamvu Round About
Vigezo Ni Uelekeo Wa Dodoma
 
Mwanamke mwema yupo na mbaya yupo, sema namna ya kumpata mwema ni kazi....
 
Wanawake ni wabinafsi sana, dawa ya mwanamke ni kuishi nae na kumuacha kama ulivyo mkuta. Usimfungulie biashara wala kumuendeleza muache kama alivyo. Unapo muimarisha mwanamke anakuona wewe ni mjinga hasa ukiyumba au kupata changamoto yotote
Hali zikiruhusu, namuimarisha mwanamke mwenye watoto wangu. Akisepa hizo pesa atalisha wanangu. Kuna kafaida katapatikana tu. Baada ya hapo yakitokea ya kutokea naendelea kuganga na yajayo.

Ila katu simuimarishi kiuchumi hawala labda niamue kutoa kama sadaka.
 
Huyo dada hakumpenda jamaa,ila mwanamke akikupenda NYIEEEE
Back to me mama watoto hana kazi ni mama wa nyumbani,ila can u imagine huwa anabana hela ninayomuachia then ananichukulia zawadi kali sana,,halafu ukichek hela ninayomuachia ni kuduchuu mno
Huwezi jua ubaya wake kwakuwa anakutegemea wewe,subiri siku kibao kigeuke yeye ndio awe ana pesa kukuzidi ndio utamjua vizuri...
 
Kwenye mahusiano yao kuna kitu hakipo sawa

Ukiacha swala la roho mbaya kwa wanawake

Hakuna roho mbaya ya kiasi hicho kwa watu wanaopendana
Upendo una nguvu sana

Hakika nawaambia kama mahusiano yao yangekuwa yako sawa huyo jamaa angejivunia kuwekeza kwa mpenzi wake

Mpenzi wako aliyekusaidia ufike hapo ulipo tena kiuchumi leo kapata changamoto unasema apambane na hali yake??

Mbona jamaa hana ujasiri wa kwenda kwa mpenzi wake ambaye anajua hapo alipofika ni kwa sababu yake? Had analala na njaa?

Kuna kitu bado hujakijua kipo nyuma ya panzia, chunguza.
Subiri yakukute mkuu
 
Huyo dada hakumpenda jamaa,ila mwanamke akikupenda NYIEEEE
Back to me mama watoto hana kazi ni mama wa nyumbani,ila can u imagine huwa anabana hela ninayomuachia then ananichukulia zawadi kali sana,,halafu ukichek hela ninayomuachia ni kuduchuu mno
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Acha nicheke mie,una uhakika hakuna kidume anayemtunza kwa vimsimbazi msimbazi?.
 
Nina shost yangu ni mfanyabiashara mzuri tu wa nafaka na anaingiza faida nzuri kwa sasa.
Ana mtu wake ambaye alisimama bega kwa bega kuhakikisha anafika hapo alipo. Huyo mtu wake kipindi hicho aliamua kuwekeza akili, mawazo na hela kwaajili ya kuhakikisha mpenzi wake anasimama kibiashara. Kweli bi shost wangu alifanikiwa kufikia malengo kwa msaada wa huyo shem.

Bahati mbaya mwaka jana mtu wake akasimamishwa kazi ghafla. Mpaka hivi sasa hajafanikiwa kupata kazi sehemu nyingine. Kama mmavyofahamu hapa dar maisha yalivyo magumu...mkaka wa watu anaishi kwa kuunga unga. Kinachonishangaza ni kuwa huyu mtu wake ambaye ni shost yangu, haonyeshi ushirikiano kwenye matatizo aliyonayo mtu wake. Kwa bahati mbaya, anamsema vibaya akiwa na sisi mashost zake.

Kwa story zake anadai mtu wake inafikia hatua anaweza kushinda siku mbili hajala kwa kukosa hela ya chakula. Na anachosema huyu best yangu ni kuwa huyo mtu wake wala hajawahi kumuomba msaada wowote. Mimi namuambia akuombe msaada kivipi wakati hali yake unaijua na unaweza ukamsitili? Anachojibu ndicho kilichonifanya nije nianzishe thread hapa. Anasema apambane na hali yake.

Huu ubinafsi tulionao utatufanya tuendelee kuona wanaume hawafai japo na mimi nimetendwa na mwanaume kiasi cha kunifanya niogope kuingia kwenye mahusiano mengine.

Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu. Wanaume ni bidhaa adimu ambayo kipata na kuishikilia ikawa yako, ni bahati sana. Ndio maana mimi wa kwangu nilitaka nianze naye chini, lakini alinigeuka. Sijui alifikwa na nini, mpaka leo sipati jibu
There is a great woman and human in you. Libarikiwe tumbo lililobeba ujauzito wako na mikono iliyokubeba na kukulea.
 
Back
Top Bottom