Usemayo Ni kweli kabisa,
Nna mwanamke wangu mmoja uyo, Ni mbinafsi wa kutupa.
Leo ndo tumerudiana baada ya wiki Juzi kuzinguana, vibaya mno.
Ananiomba Ela ya kuboost biashara yake afu eti ananiwekea na DEADLINE.
Na deadline line imefika,
Namweleza asubiri nitoke msibani, yeye analazimisha Ela itumwe Kwenye simu sikU Iyo iyo.
Anasema ikishindikana, ataenda kuomba msaada kwingine na nisije mlaumu.
(NMEMJIBU,
" Wee Nenda tu hata hainistui coz utakaoumia ni uchi wako na najua kwangu you are always after your something"
Na Tena anafoka eti,
Nimekua mwanaume asiyena msaada kwake kila anapokwama,
Ila
Anasahau kua hata Iyo biashara inayoleta chokochoko,
-wazo nimempa Mimi, baada ya kuchoka kua ananiomba omba Ela ovyo.
-mzigo wake wa kuanzia nmechangia Zaid ya 50%,
-Kodi ya fremu miezi 6 ya Kwanza nmemlipia mimi,
- anakonunua mzigo nmemuunganisha Mimi.
-usafirishaji wake, ushuru, clearance n.k kwa mizigo yake kila akiagiza nagharamia Mimi maana anaviziaga nnapoagiza mizigo yangu anaomba na yeye mzgo wake nimuunganishie. Kwaiyo hatoi hata Mia.
Yaani uyu kiumbe Hana shukrani kabisa,
Bad enough,
Afu alivoking'anizi eti anataka tuzae mtoto.
Kiukweli,
Nikifanya kosa la kumzalisha mwanamke kichwa box Kama huyu,
Ntakua nmeikosea Sana damu yangu kumchagulia mama MBINAFSI Kama uyu.