Voiced Voice
JF-Expert Member
- Feb 1, 2018
- 248
- 249
Wakati bado tunasherehekea ubingwa wa waliopigania dada zetu nadhani inabidi tuwekane sawa. Ni ukweli usiofichika kuwa TFF na wadau wa michezo kwa ujumla wanawekeza fedha, mawazo, na akili zao zote kwa timu za wanaume. Soka la wanawake limekaa kiyatima yatima tu huku la wanaume likitawala vyombo vya habari na mitandao ya kijamii yote. Hata haya mashindano ya Afrika mashariki ilikua nadra sana kukutwa habari zake kwenye vyombo vya habari vya tanzania. Kila gazeti, redio na television imejaa Ali Kiba aenda Coastal Union, Simba Uturuki, Yanga yasajili na umbea mwingine kama huo.
Nani sasa anaweza kujivunia ubingwa wa akina dada hawa? Nadhani ni wao tu, wao na mungu wao, kocha wao na benchi la ufundi. Mchango ambao TFF inautoa kwa timu hii ukilinganisha na ule wa ile 'kichwa cha mwendawizimu" utajua kwa nini nasema TFF hawapaswi kusheherekea wala kujivunia. Wamewekeza kidogo sana kwenye timu ya wadada huku wakipoteza nguvu nyingi kwa timu ya wanaume. LAKINI mavuno waliyovuna kutoka kwa hawa wadada ni heshima kubwa ya kujivunia.
Kwa anayejua mpira wa miguu na amewaona hawa Kilimanjaro queens ataniunga mkono kuwa wanasakata soka na wanaari ya ushindi. Kwanza wanajituma na wanatafuta ushindi kwa nguvu zote. Sasa wale wenzetu na sisi ambao huwa wanacheza huku wakiwaza fedha za MO na Manji waleee, kwanza huwa hawajitumi, wanacheza kutimiza dakika 90 tu, wapo uwanjani kama hawapo. Cha ajabu huko kwa wasiojituma ndiko tumewekeza nguvu zote zote. AIBU SANA. Hawa wadada hata mechi wanazoshindwa ukiangalia wanashindwa 'kiume'. Wanapambana hadi hatua ya mwisho. Naomba angalia goli ya nne lilifungwa dhidi ya Ethiopia kisha utafakari kama kuna mtu Taifa stars kule angekua na nia ya kufunga na akapambana kama aliyoionesha Fatuma Mustapha huku wakiwa mbele kwa magoli matatu kwa moja.
Tunahaja ya kuona aibu na kuamua kuwekeza nguvu kwenye biashara inayolipa. Wahindi wamewekeza kwenye cricket sio wajinga. Hebu tuachane na huuu ukichwa wa wendawazimu, TUWEKEZE KWENYE SOKA LA WANAWAKE ZAIDI MAANA WAO NDIO WENYE NIA YA KULIWAKILISHA VEMA TAIFA.