Kitu ambacho nakifuruhia ninaposikiliza maneno/hotuba za wanasiasa hapa nchini ni matumizi yao ya lugha hasa pale wanapounda maneno mapya na tungo/virai ambazo zinasimama kama utambulisho wao kwenye uwanja wa siasa. Yafuatayo ni baadhi ya misamiati na tungo za wanasiasa na majina yao kwenye mabano.
- Hata nyasi tutakula (Bazil Mramba)
- Soka la Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu (Rais Mwinyi)
- Akili za kuambiwa changanya na zako (Rais Kikwete)
- Ukitakaka kuona nyeti za kuku, subiri upepo upulize (James Lembeli)
- Kubadili gia angani (Freeman Mbowe)
- Sawa Sawa! (Maalim Seif)
- Wacha wazime tutawasha vibatali (Rais Shein)
- Kujimwambafai (Rais Kikwete)
- Bao la mkono (Nape)
- Wanaoshi mabondeni, wacha mafuriko "yawa-bondoe" : Hapa alimaanisha wacha wakumbwe na mafuriko wale wanaokaidi kuhama mabondeni.