Nilikua ccm kirumba. Mambo ni hayohayo. Kiongozi mmoja wa yanga alipewa 'mzigo' awafikishie vijana wa Toto. Akakaa nao hakuufikisha pengine aliamini yanga wangeshinda kwa uwezo. Vijana wa Toto walikomaa kisawa sawa, na huenda wangeamua wangeshinda maana walikua wanaingia mpaka kwenye 18 halafu wanapiga fyongo. Mpaka half time ngoma ilisomeka 0 - 0 huku matokeo ya Dar tunasikia Simba anaongoza bao 2. Ilibidi waulizwe viongozi wa Toto "vp mbona vijana wamekaza?" na endapo wamepata mzigo, waliposema hawakupata mzigo, ilibidi yule kiongozi atafutwe na mzigo ufikishwe. Hata hivyo inadaiwa, mzigo uliokua umeandaliwa toto waliukataa wakidai ni kiduchu, ndipo yanga wakaongeza dau. Ndipo mabao yakaanza kumiminika 'kiajabu' yakianzia mapema tu baada ya kuingia kipindi cha pili (dk 46). Pia kipa mahiri wa Toto aliondolewa dk za mwisho, na kuingizwa kipa ambaye kwa wanaoijua vizuri toto wanamuelezea kuwa kibonde, na akafungwa bao la 3 kizembe sijapata kuona. Pamoja na ushabiki wangu wa Yanga, Sikufurahia kilichotokea uwanjani, na yanga hawakuonesha kiwango chochote. Walionekana kuzidiwa kimchezo. Naweza kutabiri kirahisi tu kwamba endapo mabadiliko makubwa yasipofanyika Yanga haitafika popote klabu bingwa Africa. Soka letu linaporomoka kwa mtindo huu.