Ubishi kuhusu share za Wasafi Media naona umeisha sasa

Please jibu swali langu kwanza halafu utauliza ntakujibu why simba walimpa dewji 49%badala ya 51%?
Mimi nimekuulizwa swali ktk comment ya kwanza kuhusu Mengi na Hyundai hujanijibu? Simba watakuwa na sauti, lkn mwisho wa siku faida watagawana na hata Kusaga akitaka kuuza Redio, lazima atamshirikisha Mondi, kwa Kuna mikataba wameingia kisheria.
 
Yaani hawa jamaa wametufanya watanzania ni malofa kweli.
kumbe hapo hamna upinzani wowote.
Aliyeibua hoja ya Kusaga kushindana na radio yake ndio huyo huyo ambae aliibua hoja kwamba Kusaga anamiliki Wasafi kwa 98% na baadae akabadilika akasema 92%!

Baada ya TCRA kutoa tangazo la waombaji wapya wa leseni na kuonesha mgawanyo wa share, hivi sasa amebadili santuri manake haidanganyiki tena! Hoja yake kwa sasa ni kwamba, so long as Kusaga ni majority shareholder basi anaweza kufanya forceful buyout na kuimiliki Wasafi kwa 100%... halafu alisoma MBA huyu!!
 
Kwa ufupi
Kituo hicho kipya cha televisheni kimezua mjadala kuhusu wamiliki wake tangu kilipoanza matangazo ya majaribio, baadhi wakisema kinamilikiwa kwa asilimia 100 na nyota huyo wa Bongo Fleva.

Ni Diamond Platnumz au Joseph Kusaga?

Ndio mjadala mkubwa uliodumu tangu mwanamuziki huyo nyota wa miondoko ya Bongo Fleva aanze kukitangaza kituo kipya cha televisheni cha Wasafi TV.

Baadhi wanadai mmiliki ni Diamond na wengine wanasema Kusaga, mmoja wa manguli katika biashara ya burudani na ofisa mtendaji mkuu wa Clouds Media, wakidai anamtumia nyota huyo wa Bongo Fleva kutangaza televisheni hiyo mpya.

Wakati mjadala huo ukiendelea, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA) imetoa tangazo linalodokeza majibu ya mjadala huo. Katika tangazo lake kwa umma kutaka maoni au pingamizi kuhusu maombi ya leseni ya Wasafi TV, mamlaka hiyo imewataja wamiliki watatu wa televisheni hiyo, ambayo tayari ipo hewani.

TCRA imemtaja mtu anayeitwa Juhayna Zaghalulu Ajmy na ambaye ni Mtanzania, kuwa anamiliki asilimia 53 ya Wasafi TV, akifuatiwa na Nasibu Abdul Juma, maarufu kama Diamond, kuwa anamiliki asilimia 45 na Ali Khatib Dai kuwa anamiliki asilimia mbili.

"Kwa mujibu wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Tanzania, maoni ya maandishi yanakaribishwa kutoka kwa mtu anayeguswa kuhusu kutolewa leseni kwa mwombaji na yaifikie Mamlaka ndani ya siku 14 tangu kuchapishwa kwa tangazo hili," linasema tangazo hilo la mwezi Novemba.

"Maoni hayo yatazingatiwa wakati Mamlaka itakapokuwa ikifikiria kutoa leseni."
Kampuni ya Wasafi, ambayo pia inamiliki lebo ya muziki ya Wasafi, imeingia kwenye mvutano mkubwa na Clouds Media, ambayo inamiliki kituo cha televisheni cha Clouds TV na redio ya Clouds FM.

Clouds Media hujishughulisha zaidi na biashara ya burudani, ikiwa na kampuni ndogo zinazosimamia wanamuziki na studio za kurekodi muziki, kufundisha wanamuziki inayofanywa, hali kadhalika kuandaa matamasha ya muziki, kazi ambayo hufanywa na Primetime Promotions.
Hata hivyo, wengi wamekuwa wakichukulia mzozo huo kuwa ni kiini macho kutokana na kuhisi kuwa Kusaga, ambaye ni ofisa mtendaji mkuu wa Clouds Media, ana hisa katika televisheni ya Wasafi TV, hivyo ndugu wawili hawawezi kugombana.

Lakini tangazo la TCRA halijamtaja DJ huyo wa zamani, ingawa mmoja wa wamiliki waliotajwa, Juhayna Zeghalulu anahusishwa na umiliki wa Primetime Promotions na ni mzazi mwenza wa mmoja wa wamiliki wa Clouds Media.

Mzozo wa pande hizo mbili umesababisha nyimbo za Diamond kutochezwa na vituo vya Clouds, huku wanamuziki wakianza kujitofautisha kwa kutumia kampuni hizo mbili; wako wanaofanya kazi za Clouds Media pekee na wapo wanaofanya kazi za Wasafi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kampuni hizo mbili zilipambana katika sakata la uandaaji wa matamasha. Ingawa matamasha hayo mawili--Wasafi Concert lililofanyika Mtwara, na Fiesta Festival lililopangwa kufanyika Dar es Salaam yalikuwa mikoa miwili tofauti, upinzani mkali ulionekana katika matangazo hadi Serikali ilipozuia tamasha la Fiesta kutokana na sababu za kiafya.

Baada ya barua hiyo ya Serikali kusambaa mitandaoni, Diamond alituma video fupi inayomuonyesha akinywa soda. Na baada ya kushusha chupa, Diamond anaonekana akitoa kicheko kirefu, mithili ya mtu aliyeona mpinzani wake amefeli.

Zaidi ya sauti ya kucheka, video hiyo haina kitu kingine chochote, hali iliyotafsiriwa kuwa anachekeshwa na kitendo cha Fiesta kufutwa.

Clouds hawajazungumza zaidi ya kituo chake cha redio kucheza nyimbo za faraja, ukiwemo wenye maneno yasemayo "hauwezi kushindana na binadamu mwenye kinywa" wa Gozbert Goodluck, ambao huchezwa kila mara tangu Jumamosi.

Wakati baadhi ya wanamuziki wakiilalamikia Clouds kuwa inawabagua, Wasafi inajitangaza kuwa wanaleta "mapinduzi ya burudani".

Chanzo: Mwananchi
 
Joe 45%
Mrs Joe 53%
Mond 2%

Ukitaka ushahidi zaidi nifate PM nyaraka zingine hazifai kumwagwa hapa.
Lakini ukiangalia hizo share hapo huyo mdada anamiliki yeye kama yeye sio as Mrs Kusaga nazungumzia from a legal perspective
 
Baada ya sintofahamu ya umiliki halisi wa hisa za wasafi media leo kila kitu kipo wazi, kuna kipindi watu walikadiria diamond kumiliki asilimia 8 ila imekuwa wazi sasa kwamba kijana wetu nembo ya Tanzania Diamond Platnumza Anamiliki hisa asilimia 45 katika wasafi media

Kwa hisa asilimia 45 diamond ana nguvu hizi

1.Kuwepo kwenye Bodi wa kampuni ya wasafi (hapa pia ni c.e.o wa wasafi)
2.Kushiriki katika kutengeneza sera za kampuni
3.kuhusishwa katika mijadala ya mienendo ya kifedha katika kampuni
4.uwezo wa kuuzianna bidhaa na kampuni ya wasafi
5.uwezo wa kupachika mameneja katika kampuni ya wasafi media
6.kuweza kutoa ushauri wa kitaaluma unaoweza kuisaida wasafi media

Tukirudi katika mapato atayopata Diamond ni kwamba mfano wasafi media imetengeneza faida inayobakia kwa wanahisa ya bilioni 1 basi Diamond anachukua milioni 450 huku kusaga akichukua asilimia 53 (milioni 530) na nyingnine asilimia 2 (milioni 29 ) itaenda kwa mwengine ambaye hajajulikana vizuri.

Ikumbukwe kwamba katika makampuni ni kawaida sana kuwa na wanahisa wengi na kuna kipindi hata alieanzisha kampuni huwa na hisa chache kuliko wengine kama ambavyo mwanzilishi wa facebook anavyomiliki asilimia 25 tu za hisa katika kampuni, Vile vile hata kampuni ya Microsoft wengi wamekuwa wakidhani kwamba yupo Bill Gates peke yake ila kuna wanahisa wengine, Ni jambo la kheri mno msanii ambae ni moja ya nembo ya Tanzania kuleta chachu ya wasanii kujikomboa na kuanza kutumia umaarufu na jitihada zao ili wafike mbali.

KAMA IMEKUKERA HAMIA POST NYINGINE
Dah... mkumbushe asisahau kodi tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Afu sio wasafi kwa ujumla ile ni wasafi TV tu
Kwa ufupi
Kituo hicho kipya cha televisheni kimezua mjadala kuhusu wamiliki wake tangu kilipoanza matangazo ya majaribio, baadhi wakisema kinamilikiwa kwa asilimia 100 na nyota huyo wa Bongo Fleva.

Ni Diamond Platnumz au Joseph Kusaga?

Ndio mjadala mkubwa uliodumu tangu mwanamuziki huyo nyota wa miondoko ya Bongo Fleva aanze kukitangaza kituo kipya cha televisheni cha Wasafi TV.

Baadhi wanadai mmiliki ni Diamond na wengine wanasema Kusaga, mmoja wa manguli katika biashara ya burudani na ofisa mtendaji mkuu wa Clouds Media, wakidai anamtumia nyota huyo wa Bongo Fleva kutangaza televisheni hiyo mpya.

Wakati mjadala huo ukiendelea, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA) imetoa tangazo linalodokeza majibu ya mjadala huo. Katika tangazo lake kwa umma kutaka maoni au pingamizi kuhusu maombi ya leseni ya Wasafi TV, mamlaka hiyo imewataja wamiliki watatu wa televisheni hiyo, ambayo tayari ipo hewani.

TCRA imemtaja mtu anayeitwa Juhayna Zaghalulu Ajmy na ambaye ni Mtanzania, kuwa anamiliki asilimia 53 ya Wasafi TV, akifuatiwa na Nasibu Abdul Juma, maarufu kama Diamond, kuwa anamiliki asilimia 45 na Ali Khatib Dai kuwa anamiliki asilimia mbili.

"Kwa mujibu wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Tanzania, maoni ya maandishi yanakaribishwa kutoka kwa mtu anayeguswa kuhusu kutolewa leseni kwa mwombaji na yaifikie Mamlaka ndani ya siku 14 tangu kuchapishwa kwa tangazo hili," linasema tangazo hilo la mwezi Novemba.

"Maoni hayo yatazingatiwa wakati Mamlaka itakapokuwa ikifikiria kutoa leseni."
Kampuni ya Wasafi, ambayo pia inamiliki lebo ya muziki ya Wasafi, imeingia kwenye mvutano mkubwa na Clouds Media, ambayo inamiliki kituo cha televisheni cha Clouds TV na redio ya Clouds FM.

Clouds Media hujishughulisha zaidi na biashara ya burudani, ikiwa na kampuni ndogo zinazosimamia wanamuziki na studio za kurekodi muziki, kufundisha wanamuziki inayofanywa, hali kadhalika kuandaa matamasha ya muziki, kazi ambayo hufanywa na Primetime Promotions.
Hata hivyo, wengi wamekuwa wakichukulia mzozo huo kuwa ni kiini macho kutokana na kuhisi kuwa Kusaga, ambaye ni ofisa mtendaji mkuu wa Clouds Media, ana hisa katika televisheni ya Wasafi TV, hivyo ndugu wawili hawawezi kugombana.

Lakini tangazo la TCRA halijamtaja DJ huyo wa zamani, ingawa mmoja wa wamiliki waliotajwa, Juhayna Zeghalulu anahusishwa na umiliki wa Primetime Promotions na ni mzazi mwenza wa mmoja wa wamiliki wa Clouds Media.

Mzozo wa pande hizo mbili umesababisha nyimbo za Diamond kutochezwa na vituo vya Clouds, huku wanamuziki wakianza kujitofautisha kwa kutumia kampuni hizo mbili; wako wanaofanya kazi za Clouds Media pekee na wapo wanaofanya kazi za Wasafi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kampuni hizo mbili zilipambana katika sakata la uandaaji wa matamasha. Ingawa matamasha hayo mawili--Wasafi Concert lililofanyika Mtwara, na Fiesta Festival lililopangwa kufanyika Dar es Salaam yalikuwa mikoa miwili tofauti, upinzani mkali ulionekana katika matangazo hadi Serikali ilipozuia tamasha la Fiesta kutokana na sababu za kiafya.

Baada ya barua hiyo ya Serikali kusambaa mitandaoni, Diamond alituma video fupi inayomuonyesha akinywa soda. Na baada ya kushusha chupa, Diamond anaonekana akitoa kicheko kirefu, mithili ya mtu aliyeona mpinzani wake amefeli.

Zaidi ya sauti ya kucheka, video hiyo haina kitu kingine chochote, hali iliyotafsiriwa kuwa anachekeshwa na kitendo cha Fiesta kufutwa.

Clouds hawajazungumza zaidi ya kituo chake cha redio kucheza nyimbo za faraja, ukiwemo wenye maneno yasemayo "hauwezi kushindana na binadamu mwenye kinywa" wa Gozbert Goodluck, ambao huchezwa kila mara tangu Jumamosi.

Wakati baadhi ya wanamuziki wakiilalamikia Clouds kuwa inawabagua, Wasafi inajitangaza kuwa wanaleta "mapinduzi ya burudani".

Chanzo: Mwananchi
 
Hapo kwenye kichwa cha habari jaribu kurekebisha,siyo kamapuni nzima ya Wasafi bali zile shares ni kwa Wasafi Tv pekee!
 
Hamna akili yes, namiliki kampuni yangu hela yangu yote asilimia 100, wanangu sharing. Akili hamna hamuoni hapo Kusaga kaandika jina la mkewe?Yes Diamond anaweza miliki asilimia 100 zake zote akazigawa kwa kuandika majina ya esma au mama yake. Nyambafu tumieni akili zenu vizuri.
Wewe ndo huna akili, Hio kampuni yako ya chini lazima mwanahisa aishughulikie juu chini ndo uweke ugali mezani😉
 
Back
Top Bottom