pistologist
Member
- Sep 28, 2018
- 16
- 20
Greetings!
"..hauna akili..! " well, japokuwa ni tusi, lakini ana maana gani huyu mtu? sidhani kama ana maana hauna ubongo. Lakini akili ni nini haswa? ubongo ni kitu cha kuonekana na kushikika.. na akili pia hivyo hivyo? " ..Hebu tumia akilii unapoongea mbele ya watu.." watu husema hayo maneno kidole kikiwa kina-point kichwa, akili ipo kichwani? ( au ndio kama kusali mtu akiwa anatazama juu, akiwa anaamini ndio maombi yake yanapoenda? ) . Hivi ni kipi kipo ndani ya kingine, akili sehemu ya ubongo au ubongo sehemu ya akili?
Kuna wakati mwili huongoza na hisia katika kufanya maamuzi, ambapo wengine hufika mbali na kuhusisha kitu kingine hapa, moyo.. mmh! hapa ndio huwa wananichanganya kabisa, utasikia, "..sikiliza moyo wako unakwambia nini, halafu ufuate.." . Hebu tuachane na habari za moyo kwanza... hivi hisia zipo sehemu gani ya mwili? hisia na akili vina uhusiano wowote? maana wengine husema "..hili suala inabidi utumie akili, sio hisia, utasababisha madhara makubwa..." Upendo, hasira au huruma vinafanyika sehemu gani ya mwili ?
Kuna vijitabia ambavyo kila mtu anavyo vya kwake, na hivi vijitabia humtofautisha mtu mmoja na mwingine, ni ngumu sana watu kufanana katika hili, wenzetu wanaita personality! ni kitu gani hiki, kina uhusiano wowote na akili ya mtu husika?