Ubongo wa mwanamke unavyofanya kazi

naweza kuamini sababu nilisikia tetesi kuwa mwanamke ana uwezo wa kumeza iwe picha au maandishi kwa wingi zaidi kushinda sisi wanaume... na ndo maana wengi wazuri kwenye biology na wabovu kwenye maths..!!!!
 
Mwanamke hajawahi kuutumia ubongo kumshinda mwanaume mkuu.

Wanawake ni watu wa kukurupuka bila kutumia ubongo/akili. Hufuata matamanio ya moyo/hisia.

Ndio maana wanawake huongoza kwa majuto kuliko wanaume.

Hivyo umeongea uongo
Napenda kuongea kutumia facts.No research no right to speak[emoji6].
Okay.Ntakuelezea professionally mkuu.Ila kabla ya hapo.Naomba wanawake na wanaume tusidharauliane kwasababu Ni hizi tofauti zetu ndizo zilizofanikisha humanity.

Point ya kwanza mkuu,ubongo wa mwanadamu Una kitu kinaitwa corpus callosum,kwa waliosoma Biology wanaelewa kuwa kazi yake Ni kuunganisha pande mbili za ubongo.Hii corpus callosum inaanza Ku develop ndani ya wiki 26 za ujauzito wa mtoto wakike.Na inakuwa Ni pana(thicker) zaidi ya mtoto wa kiume.

Point ya pili kabla ya hitimisho,upande(hemisphere) wa kushoto wa ubongo kazi yake Ni logical thinking(sijui kutafsiri.ila Ni Kama kufikiri bila kuhusisha hisia).upande wa kulia unahusika na intuition(hii Ni kufikiri kwa kuhusisha hisia mbalimbali).
Utafiti unaonesha kuwa mwanaume anatumia zaidi ubongo wa kushoto.mwanamke anatumia pande zote sawa.kwanini?kwasababu Ana corpus callosum pana inayo unganisha vizuri ipasavyo pande hizi mbili za ubongo.

Point ya tatu.Sehemu ya ubongo ijulikanayo kama hippocampus, inajihusisha na hisia na kumbukumbu.Mwanamke Ana 'gray matter' nyingi kwenye hippocampus kuliko mwanaume.

Point ya nne
'limbic system' kwenye mwili wa mwanamke Ni kubwa na na imeingia ndani zaidi.Ndio Maana wanawake wako kihisia zaidi.na pia wanauwezo wakueleza hisia zao vizuri zaidi.Hii pia inamponza mwanamke kwani anaweza kupata matatizo ya kihisia kama 'depression'.

Point ya tano
Mwanamke Ana ubongo mdogo kwa asilimia nane kulinganisha na mwanaume.Na ubongo mkubwa wa mwanaume unampa 'processing power'kubwa.Ila haimaanishi kuwa Ana akili zaidi.
Ubongo huu mkubwa Ni muhimu ili kuendesha mwili mkubwa wa mwanaume na misuli.Naona hapa mtakuwa mmelewa.

HITIMISHO
Kama umesoma na kuelewa hizo point hapo juu utakubaliana na mimi kuwa;
Mwanaume anauwezo mkubwa wa kufikiri 'straight'.Ila mwanamke Ana uwezo mkubwa wa KUFIKIRI kwasababu anahusisha pande zote za ubongo.rejea point ya kwanza.

Mwanamke hasahau kisahisi.kwaiyo naona wengi mtaelewa kwa nini mwanawake hata ukimfanyia jambo zamani Sana atakumbuka.rejea point ya3.

Mwanamke anatumia zaidi ubongo wake zaidi ya mwanaume rejea point ya pili.Ndio Maana Ana uwezo mkubwa wa 'multi tasking'
Tafiti zilozofanywa na chuo cha loughborough,zinaonesha mwanamke hutumia zaidi ubomgo wake na hivyo anahitaji kupumzika dakika 20 zaidi ya mwanaume.

Nakadhalika
Mkuu nadhani utakuwa umeelewa.Hakuna alirebora,tuko tofauti tu,ili tuwe jinsi tulivyo.[emoji111]
 
Ukimaliza kumwelewesha nakusubiri hapo nje pulizzz usichelewe dr.
 
Ni kweli kabisa manake unakutana leo mnabadilishana namba kabla hujageuka keshaomba hela na atakupa stori za dhiki zake kama kazaliwa south sudan so ndo hapo nnapoona umahiri wao wa ubongo
 
Mwanamke hajawahi kuutumia ubongo kumshinda mwanaume mkuu.

Wanawake ni watu wa kukurupuka bila kutumia ubongo/akili. Hufuata matamanio ya moyo/hisia.

Ndio maana wanawake huongoza kwa majuto kuliko wanaume.

Hivyo umeongea uongo
Kweli mkuu mwanamke anatumia hisia%60
Akili%18
Nguvu%22
Huyu anasema mwanamke ana akili kuliko mwanaume sijui kafikilia nn. Hakuna kitu chochote mwanamke alichokivumbua daniani hata izo nguo wanazova zimefumbuliwa na mwanaume. Na mwanamke anauwe wa kufanya kazi nyingi za hapa na hapa sio mbali. Angeniambia mwanamke anaishi kwa kisasi apo ningwelewa
 
Reactions: SDG
Hapo ni kwa uchache tu lakini wanawake wengi zaidi ndo wanaponzwa na wanaume.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Sasa ingekuwa hivo kweli, si kungekuwa na tofauti kubwa/za maisha kati ya hizi jinsia 2? Au ndiyo yaleyale binadamu alikuwa nyani?
 
Hao ulio wazungumzia ni wanawake wa Jupiter sio hawa wa hapa dunia


je, mwanaume anaefanya hivi pia tuseme ana ubongo wa mwanamke?
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…