Ubora na Udhaifu wa SPACIO

mdoghosho

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2016
Posts
969
Reaction score
1,383
Wakuu,ninahitaji kuagiza Toyota Spacio ya Cc 1500 mwezi ujao.

Ninaomba kujua yafuatayo kuhusu gari husika.

1. Fuel Consumption yake ikoje? inakula sana au kidogo?

2. Itaweza kuhimili matumizi ya kijijini huko milimani Upareni? (ndiko itakoenda kutumika siku zote)

3. Ni gari Imara ?

Natanguliza shukrani wakuu, karibuni mnipe mawazo.
 
Ile ya cc 1799 new model ni gari Kali sana pia inaimili Shida ulaji wa Mafuta ni mzuri sana nimeenda nayo songea tokea arusha Mara 2 bila tabu
 
Ile ya cc 1799 new model ni gari Kali sana pia inaimili Shida ulaji wa Mafuta ni mzuri sana nimeenda nayo songea tokea arusha Mara 2 bila tabu
Inakula litre ngapi kwa kilomita kwa experience yako?
 
ina maana hamna watu wengi wenye uzoefu wa Spacio humu ndani?
 
Siku hizi mimi kama gari sio 6 clyinders whether ni straight/V-shape linakua halina utamu ninaoutaka mimi,kasoro gari zenye boxer engine kama Subaru..
 
Ninzuri sana ila hakikisha niengen ndogo cc 1399 usije kununua ya cc 1799
 
Ninzuri sana ila hakikisha niengen ndogo cc 1399 usije kununua ya cc 1799
Ile ndogo ni cc 1490.

Vipi una experience na hii ya engine ndogo? Uimara wake ukoje? Ni economical (kwa ishu ya mafuta) ?
 
Namba 1 na 3 spacio ipo very good......lakini namba 2 hapo kwa location uliyotaja na muda itakayotumika mmmmmh nahisi kama itatoa boko mapema
 
Me ninayo sijutii kwa kweli nikiweka full tank from kyela to Songea nafika Mafuta yamebaki robo tank kinachonifurahisha ni uwezo wa kubeba vitu vingi bonnet safi Gari ina Nguvu safi mno hakika sijutiii ni CC 1490
 
Wakuu, nakaribisha mawazo yenu. In 2 weeks naenda kuagiza, naombeni maoni yenu kwa experience zenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…