Ubora wa gari aina ya Nissani X-trail

Ubora wa gari aina ya Nissani X-trail

RORYA79

Senior Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
130
Reaction score
61
Naomba kujua ubora wa hizi gari kama kuna mtu ameshawai kuzitumia tafadhari hasa kwa barabara za vumbi.
 
Hizi Gari nyingi zake hazinaga 4WD,
Sasa unakua na Mgari Mkubwa lakini kwenye Mchanga au Tope unasanda
Hii si kweli,gari kuwa na 4WD ni chaguo lako mnunuaji,mm ninayo na nina mwaka wa tano huu na ni 4WD, ubovu au uimara wa gari ni ww mtumiaji kuzingatia matumizi na kuifanyia service kwa wakati.
 
Hii si kweli,gari kuwa na 4WD ni chaguo lako mnunuaji,mm ninayo na nina mwaka wa tano huu na ni 4WD, ubovu au uimara wa gari ni ww mtumiaji kuzingatia matumizi na kuifanyia service kwa wakati.
Umeelewa lakini nilichoandika??
Au umejibu tu mradi nawe uonekane umejibu??
 
Ni mojawapo na gari bora na imara ila inahitaji matunzo. Ijali service na kama imevuka km 100,000 hakikisha unatumia original oil za Nissan ama oil zingine zenye marking ya 5w 20 na kuendelea ni mahsusi kwa gari zenye odomiter zilizozidi laki moja
 
Umeelewa lakini nilichoandika??
Au umejibu tu mradi nawe uonekane umejibu??
Nimeelewa ulichoandika na ndo maana nikakujibu si kweli kuhusu hizo gari unazosema nyingi si 4WD, kuhusu 4WD ni uchaguzi wako wakati unanunua hayo maelezo mengine ni kwa muuliza swali wa mwanzo, usipaniki.
 
Yaani umejibu kama vile mie nimepondea 4WD, maana umesema 4WD sio mbaya ndio maana unayo na haijakusumbua. Mie hakuna popote niliposema 4WD inasumbua ndio maana sijakuelewa.

Ila nlichosema mie ni kua kwa Gari kubwa kama ile then haina 4WD sio poa. Gari ikishakua SUV na kwa ukubwa ule inapendeza zaidi ikiwa na 4WD. Ni sawa usikie mtu an Range Rover, Nissan Patrol, Land Cruiser, etc lakini ukaambiwa haina 4WD, haipendezi
 
Nasikia hizi gari ni imara ila ni za kitajiri sana. Oil yake tu bei mkasi balaa nasikia ni laki 2+, hapo bado gearbox oil majanga tupu
Engine oil haubanwi na aina yoyote,unaweza tumia yoyote tu ila kwa gearbox ni lazima utumie nisani na kwa extrail kuna oil inaitwa Matic J ndo yake hiyo,inauzwa kwenye range ya 40,000 mpaka 45,000 kwa lita, zinaingia lita 4, ila unatembelea kuanzia km 60,000 mpaka 120,000 ndo unabadilisha.
 
Nasikia hizi gari ni imara ila ni za kitajiri sana. Oil yake tu bei mkasi balaa nasikia ni laki 2+, hapo bado gearbox oil majanga tupu
acha kuamini hear say...miliki kwanza ndiyo useme....nissan zote hazitaki ubabaishaji...ila oil zake sibghali kiasi hicho unachosema . .nissan ni gari nzuri sana endapo utafuata masharti yake na si kununua oil za kupima kama kwenye toyota
 
Ni gari nzuri sana. Mimi ninayo tangu nimekuwa nayo tangu 2015 nikiwa nimeinunua kwa mtu aliyeiagiza nje akaitumia kutoka km 51000 hadi 80600. Na mimi nimeanzia hapo hadi sasa ikiwa na km kama 110000 hivi. Mimi naishi mikoani ambako ili ukutane na barabara ya lami ni lazima upige vumbi km zaidi ya mia mbili njia nyingine hata zaidi ya Mia nne. Nilichobadilisha ni oil ya injini na gia box, tairi na shokap za nyuma tu
 
Back
Top Bottom