Ubora wa mbao za Mtiki

Ubora wa mbao za Mtiki

Jamani mbao ya mtiki ni mbao yenye thamani kuliko mbao yoyote duniani hata uuzwaji wake nje inauzwa kwa futi na kiukweli watanzania wengi hatuna uwezo wa kutumia mtiki kama gharama yake ingejulikana ila walio wengi wanalima na kutopata soko linalostahili ndio maana inafananizwa na mninga na mkngo ukipanda ndege chunguze zile furniture za mule ndani ni mtiki kwenye meli angalia vizuri mbao zile ni mtiki hoteli za nyota 5 chunguza vizuri ni mtiki
 
Ngoja niweke ushuhuda wa mtiki hapa, hii ngazi ipo mpaka leo kwenye boma la kwanza la mjerumani pale tanga, boma lilijengwa mnano mwaka 1890 jamaa walitumia mtiki kwenye kila sehemu waliotaka kutumia mbao, jengo lile sahivi linatumika kama makumbusho na lina ghorofa 3, hawakutumia nondo jamaa ila mitaimbo ya mitiki ulitumika kushika zile sakafu mpka leo hapaja teteleka,

Ile milango yote mnayiona kwenye makasri yaliyokuwa ya mwarabu ambayo mengi kule zanzibar yeshatimiza zaidi ya miaka 100 ni mtiki ule, hakuna kama mtiki duniani
IMG_20191201_132829_7.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtiki hata ukinyeshewa na mvua hauharibiki ndiyo inayotumika kutengeneza boti
 

🌱Group hili nikwa wakulima WA miti ya mitiki.

🌱Lengo Nikupeana ushauri juu ya upandaji na uvunaji pamoja na changamoto mbali mbali zinazolenga maswala ya miti.

🌱Pia Nikujua masoko ya ndani na nnjee.
 
Wadau, naombeni ushauri hukusu ubora wa mbao za huu mti uitwao Mtiki katika kitengeneza milango ikilinganishwa na mninga au mkongo. Kuna mdau ananishawishi kwamba wenyewe ndio the best, ingawa majority wanapigia chapuo mninga. Ushauri please.
Vipi kuhusu mtibwa mringaringa unaujua nao ni mzuri unakaribia mninga na mkongo
 
trust me, mninga ndo mti bora wa miaka yote pia hata gharama yake si mchezo na haupatikani kila nchi, tuna bahati sisi kuwa nao, muulize fundi yoyote atakueleza, hizi mbao nyingi tunazoziona ni mipodo na sio imara
Mpingo je?
 
Back
Top Bottom