UBORA WA ZAHERA HUU HAPA.

mikedean

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Posts
3,267
Reaction score
4,634
Kiukweli timu yetu ya Yanga ,timu ya wananchi,mabingwa kihistoria wa Tanzania.mwaka huu tangia msimu huu wa 2019/2020 umeanza timu yetu bado haijapata muunganiko unaotakiwa.

Kocha mwinyi Zahera nae amekuwa mstari wa mbele tusema ukweli kwamba timu bado haijapata muungano.kila mtu anaona hatuna haja ya kujisifu kama mikia kuwa tuna timu bora kisha tunafungwa na UDSongo na kutupwa kabisa kwa aibu katika uwanja wa nyumbani.

Kwa kutambua hilo,kocha Mwinyi Zahera anatumia akili nyingi kuifanya Yanga iwin hizi mechi kwa kutumia mbinu za kupata ushindi au Droo kwa namna yoyote.Katika mechi na Township rollers alitumia mbinu hii katika mechi zote.alitaka aidha ashinde au adroo.pia katika mechi ya leo ametaka aidha adroo au ashinde.Kilichoiua simba ni kutaka droo ugenini(kuzuia wasifungwe nyingi kama ilivyo kawaida yao)ili wakija kwa mkapa washinde nyingi wasijue kuwa UD songo walitumia mbinu kama ya Zahera to win or droo.

Mpaka sasa nina imani na Yanga kuwa inaweza kusong mbele kwa kwenda aidha kushinda au kudroo pale Ndola.

Yanga ingekuwa chini ya Zahera msimu wa 2017/2018 katika kombe la shirikisho ikiwa na kundi rahisi kabisa la timu za Gormahia, timu ya Rwanda nimesahau jina na timu fulani ivi ya ivory coast.Kundi jepesi kabisa.Lakin Yanga ilikuwa katika ukata mkubwa wa pesa.Kocha Hans van plujim alishindwa kabisa.Hatimaye hatukuvuka .Ila kwa kundi lile kwa kweli Yanga na Gormahia zingevuka kama Kocha angekuwa Zahera kwa kweli pale tulipoteza bahati.

Naiombea Yanga ishinde ama la hata kuingia hatua ya makundi ya shirikisho itapendeza zaidi.kama Yanga na Azam zikiingia makundi na Yanga bado point zitaongezeka na nafasi 4 zitaendelea kubaki baada ya mikia na KMC kung'oka.
Hofu yangu ni kuwa simba mwakani atashiriki Champion League na atatolewa tena hatua za awali am akijitahidi ni kwenda shirikisho.
 
Kwanza kabisa Simba haikufungwa na Udsongo. Walitoka draw ya goli moja kwa moja.
Pili,hakuna timu isiyopenda kushinda goli nyingi ikiwa nyumbani. Yanga pia ilitaka hivyo lakini Zesco nao walikuwa na mipango ya kushinda au kudraw.
Yanga kupata draw isiwe defensive mechanism kuwa mlipanga iwe hivyo. Haya matokeo Ni mazuri kwa Zesco na mabaya kwenu.
Cha kufanya Ni kujipanga ili muweze kushinda au kupata draw ya kuanzia goli mbili na kuendelea.
Msijipe moyo Sana maana bado ngoma Ni mbichi hii. Jengeaneni hamasa mashabiki pamoja na wachezaji ili mkapindue meza Kama mlivyowafanya Township rollers.
Nawatakia Kila la kheri.
 
Umenena kweli.Lengo letu kubwa lilikuwa ushindi tukishindwa basi tudroo.lakin ukiangalia watu wengi waliona ni ngumu yanga kuingia gola moja kwa Zesco.kama ilivyokuwa kwa Rollers kwa sababu kikosi si cha kueleweka.
 
Heeeeh!! Kumbe hawa ndugu zetu Mikia walitolewa raundi ya kwanza na UD Songo!! Sasa mbona wana kiherehere sana huku mitaani?
 
Sasa mbona hata hujaweka picha? Ungeweka picha kama unataka na wengine wauone.


 
kwa kuweka kumbukumbu sawa.....zesco hajafungwa goli lolote msimu huu...yanga alimbikiri Jana
[emoji16][emoji3]
 
Heeeeh!! Kumbe hawa ndugu zetu Mikia walitolewa raundi ya kwanza na UD Songo!! Sasa mbona wana kiherehere sana huku mitaani?
Sio raundi ya kwanza..hatua za awali wale wakina Esperance.TP Mazembe nk hawachezi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…