Uboreshaji sekta ya elimu unaendelea

Uboreshaji sekta ya elimu unaendelea

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea na lengo lake la kuimarisha sekta ya elimu ujenzi wa madarasa 8000 ya secondary unaendelea.

Lengo la ujenzi wa madarasa haya ni ifikapo 2023 wanafunzi wote wa kidato cha kwanza waweze kuanza masomo kwa wakati mmoja bila kuwepo kwa second selection, Idadi ya wananfunzi waatakaojiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi zaidi ya Milioni 1 ndio maana serikali inaboresha mazingira ya kusomea.

Lakini pia ikumbukwe wanafunzi watasoma katika mazingira bora huku wakipata elimu bila malipo na walimu wa kutosha Rais Samia Suluhu anaendelea kutimiza lengo lake la kujenga Tanzania ya wasomi.
 
Mtaboresha hadi lini? Mahutaji ya madarasa yamekua yakiongezeka kila mwaka tangu mwaka 1961 hadi leo.

Ongezeko kubwa la idadi ya watu bila mipango na rasilimali ni umasikini.
 
Ndio maana Serikali inaendelea na na kuongeza madarasa kwasababu inajua watu wanaendelea kuongezeka kila siku sasa kuanzia mwakani hautasikia tena shida ya madarasa ba madawati au upungufu wa walimu
 
Kumbe, Kwahiyo;

Ajira za waalimu mmetangaza kuajiri waalimu laki ngapi hiyo January?

Mwalimu ataanza na mshahara wa milioni ngapi kwa mwezi?

Na watoto wa wakubwa wataanza kusoma shule za kata ama hilo halimo?

Mkiboresha hayo walau elimu itapata pa kuanzia na chini ya hapo tutasema, maboresho ya elimu yanelekea kuizika elimu futi 100.

Alafu nisisahau, masomo ya sayansi yanahitaji practicals. Twambieni kila shule ya serikali na kwa kila somo yaani Physics, Chemistry na Biology kati ya mahitaji ya vifaa kwa 100% nyie mmepanga January kila somo liwe na vifaa walau 80%? ama ndo inabaki ile ile 30% ya leo?

Mie navyojua nchi hii masomo ya sayansi wala si magumu kama tunavyodanganywa, huu ugumu unatengenezwa ili watoto wafeli sayansi. Haangii akilini somo linatakiwa kusomwa kwa vitendo, shule ina 30% tu ya mahitaji ya vifaa kwa somo hilo alafu mtoto akafaulu, na hata wanapofaulu nadhani uwa kuna ka moderation ili ionekane "walau" wamefaulu na sie wadanganyika tunaridhika.

Kama vifaa vinapatikana hata kwa 70% tu mie naamini masomo haya yanaitwa magumu watu watakuwa wanajiokotea A za kumwaga sana ...sayansi siyo blaa blaa, sayansi ni vitendo, sayansi ni vifaa.

cc. Nyabukika
 
Hutasikia tena ilhali yaloongezwa mwaka huu ni kukidhi ongezeko la mwaka huu? Unajua mwakani kutatakiwa kujengwa mengine kukidhi ongezeko la mwaka huo? Lini mtatulia kuwaza vipaumbele vingine?
 
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea na lengo lake la kuimarisha sekta ya elimu ujenzi wa madarasa 8000 ya secondary unaendelea.

Lengo la ujenzi wa madarasa haya ni ifikapo 2023 wanafunzi wote wa kidato cha kwanza waweze kuanza masomo kwa wakati mmoja bila kuwepo kwa second selection, Idadi ya wananfunzi waatakaojiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi zaidi ya Milioni 1 ndio maana serikali inaboresha mazingira ya kusomea.

Lakini pia ikumbukwe wanafunzi watasoma katika mazingira bora huku wakipata elimu bila malipo na walimu wa kutosha Rais Samia Suluhu anaendelea kutimiza lengo lake la kujenga Tanzania ya wasomi.
Baada ya miaka 61 ya uhuru ndio kwanza tuko hapa. Naona aibu mimi.
 
Hivyo vyote ulivyoongea vimefanyiwa kazi mkuu maana sio ujenzi wa madarasa tu hata waalumu wataajili zaidi ya elfu 42 na kufanya practical inawezekana kwasababu shule nyingi zimewekewa umeme kwaiyo upande wa elimu Rais Samia Suluhu yupo vizuri
 
Kweli ni baada ya miaka 61 ya uhuru lakini Rais Samia Suluhu anakasi ya ajabu katika maendeleo ya sekta mbalimbali na ameipa kipaumbele sekta ya elimu ukifatilia mpaka vijijini madarasa yamejengwa na kuna walimu
 
Hutasikia tena ilhali yaloongezwa mwaka huu ni kukidhi ongezeko la mwaka huu? Unajua mwakani kutatakiwa kujengwa mengine kukidhi ongezeko la mwaka huo? Lini mtatulia kuwaza vipaumbele vingine?
Hakuna shida kwasababu watoto wanazaliwa kila siku na kwa ujenzi wa madarasa haya tatizo la madarasa halitajitokeza tena Rais Samia Suluhu amejipanga kuhakikisha elimu inaimarika zaidi
 
Samia ataondoka madarakani na ataiacha shida ya madarasa.
 
Hivyo vyote ulivyoongea vimefanyiwa kazi mkuu maana sio ujenzi wa madarasa tu hata waalumu wataajili zaidi ya elfu 42 na kufanya practical inawezekana kwasababu shule nyingi zimewekewa umeme kwaiyo upande wa elimu Rais Samia Suluhu yupo vizuri
Mmeshafeli Mkuu kwasababu hiyo M1 ya fomu 1 tayari mnaijua na leo zimesalia siku 25 shule zifunguliwe lakini hizo ajira 42 elfu hazipo na hamjatangaza hapo nazo hazitoshi hata robo.

Wakati kuna almashauri ina uhaba wa waalimu 500 leo, nchi hii ina halmashauri ngapi na hawa 42elfu wanakuja kukidhi nini kwenye ongezeko la watoto m1?

Alafu mie nimekuuliza ki% ya mipango yenu kuhusu vifaa vya masomo ya sayansi, wewe umeongea kisiasa eti umeme. Ishu haikuwa umeme tu kwani hata zenye umeme vifaa ni chini ya 40%, sasa utasemaje ishu ni umeme?

Twambie kiujumla kama nchi na idadi ya shule zenu mnaijua vizuri, mmepanga hata masomo kuyapa vifaa kwa % kuanzia mwakani ili tuongee kama watafiti na si kama wanasiasa Mkuu

cc. Nyabukika
 
Wanafunzi zaidi ya milioni wanajiunga kidato Cha kwanza mwakani, je, waliomaliza kidato cha nne ni wangapi? Tofautu yake Ina uwiano gani na madarasa yanayoongezeka?

Back
Top Bottom