SoC04 Uboreshaji wa elimu ya vitendo

SoC04 Uboreshaji wa elimu ya vitendo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 11, 2024
Posts
5
Reaction score
3
UBORESHAJI WA ELIMU YA VITENDO
Tanzania ni nchi inayopatikana Afrika mashariki ambayo imepakana na uganda ,kenya ,Burundi Rwandan na Zambia , katika mfumo wa elimu Tanzania bado iko chini sana ukilinganisha na nchi zingine,hivyo imepelekea wimbi la uwepo wa ukosefu wa ajira .tunaweza kutengeneza Tanzania ya kesho kwa kuwaandaa vijana katika elimu bora ya vitendo kwa kufuata utaratibu ufuatao, kuanzisha Shule za Awali na za Ufundi katika Taasisi za
Serikali


Taasisi kama Magereza na Polisi zinaweza kuanzisha shule ili wahitimu wa JKT na VETA wanaoendelea na elimu ya juu waweze kufundisha taaluma na ufundi kwa wanafunzi wa elimu ya awali.

Kuimarisha Masomo ya Ufundi katika Shule Binafsi: Shule binafsi ziwe na masomo ya ufundi ili wahitimu waweze kuweka malengo mapema kuhusu taaluma wanayotaka kufuata. Hii itarahisisha mchakato wa kujiunga na mafunzo ya ufundi.

Kuhamisha Mafunzo ya VETA kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT): Serikali inaweza kuunda sera inayoelekeza mafunzo ya ufundi (VETA) kufanyika kwenye kambi za JKT. Hii itasaidia wahitimu kupata ujuzi wa awali wa ufundi na taaluma, badala ya kurudi na ukakamavu pekee. Pia itapunguza gharama za kwenda VETA baada ya JKT.

Kurejesha Masomo ya “Art and Craft” na Kilimo kuanzia Shule za Msingi
Kufundisha stadi za kazi na kilimo kwa vitendo katika elimu ya awali kunaweza kuwapa wanafunzi ujuzi mapema na kuwazuia kubagua masomo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom