officiallai92
New Member
- Jan 25, 2023
- 2
- 1
Maendeleo ni mchakato unaohitaji mifumo bora ya uongozi na usimamizi unaozingatia misingi ya haki na uwajibikaji katika nyanja zote za uchumi, jamii, siasa na utamaduni. Katika kufikia Tanzania yenye maendeleo chanya inahitaji,utawala wenye katiba hai inayoweza kutetea maslahi ya taifa, uongozi wenye kiu na Shauku ya mafanikio,na uboreshaji wa mifumo sahihi ya uendeshaji shughuli za serikali na mifumo ya kisiasa.katika kuboresha mifumo ya utendaji kazi na mifumo ya kisiasa ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia
Uwepo wa mipaka baina ya utawala na shughuli za siasa:
Katika kuijenga Tanzania shughuli za utawala zisiambatanishwe na suala la siasa hii itasaidia kuepuka kuwepo kwa siasa za kurithishana, upendeleo na rushwa. Ukirejerea changamoto za ajira sehemu kubwa ya wanaokosa ajira ni wale ambao hawana historia ya siasa ndani ya familia na wale wenye hali duni kiuchumi, ni vyema shughuli za utawala zisihusishwe na siasa rejerea nafasi za kazi mbalimbali ambazo zinahusisha mwenyekiti wa kijiji ni ngumu kapata nafasi ya ajira sababu mfumo wa upatikanaji tayari umejikita katika kada au upendeleo wa chama husika.
Uwepo wa dira ya Taifa, na mpango kazi unaondaliwa na wananchi kila mwaka:
Kila serikali huwa na vipaumbele vyake. Rejerea katika awamu tofauti za uongozi kila serikali hufika madarakani na mpango kazi wake katika kujenga Taifa mara nyingi mpango kazi wake hautimii kutokana na muda au mazingra ya utekelezaji wake hii inakuwa ngumu kwa awamu inayofuata kuendeleza sera thabiti kutokana na muingiliano wa mpango kazi au viporo vilivyoachwa vinakwamisha mchakato wa maendeleo, lakini kukiwa na mpango kazi, Dira maalumu ni rahisi kufikia malengo, Taifa linahitaji kuwa na dira ambayo itatumika kama muongozo, ambao kila serikali inayofika madarakani itatumia hii itasaidia kufikia malengo na kutokuwa na viporo katika utekelezaji au uboreshaji wa miundombinu au shughuli zingine za maendeleo.
Kuwepo na dola yenye mamlaka na nguvu kwa kuzingatia misingi ya haki:
vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania havina nguvu katika uwajibikaji wake badala yake hufanya kazi kwa matakwa ya serikali husika na sio matakwa ya katiba ya nchi, Tanzania imekuwa na ulinzi lakini hakuna usalama hii imeleta ulevi wa madaraka kwa viongozi wanajilimbikiza mali, rushwa inaendelea kuota mizizi na hata haki za binadamu hupuuzwa. Sheria inapaswa kuwa msumeno ikate pande zote bila kuangalia mali,hadhi,jinsi,au kabila. Upotevu wa mali za umma unaofanywa na viongozi unapaswa kushughulikiwa kwa kukatwa mishahara yao na kuondolewa katika nafasi hiyo ya uongozi hili litawezekana endapo kutakuwa na vyombo vyenye nguvu.
Katiba ya nchi ieleze sera ya uchumi na kuwepo kwa tathimini ya sera husika:
uchumi ni kiini kikubwa katika kufikia maendeleo ya nchi. Katiba ni muongozo stahiki katika kufikisha nchi ya ahadi. Katiba ieleze sera za uchumi ambazo Tanzania itaipa kipaumbele. Ukirejerea kilimo kama uti wa mgongo wa Tanzania basi nguvu iwekwe katika kilimo kwa kuwezesha wakulima wadogo ama wakubwa na kusaidia upatikanaji wa masoko na suala la bei katika kuuza malighafi zao bila kuwepo unyonyaji. Sera ya uchumi iguse suala la kodi kama sehemu ya mapato kwa kukuza uchumi na kuwe na sheria katika kuamua vyanzo vya kodi. Vilevile mikopo kama sehemu ya Mapato itumike katika kuwezesha sekta ya kilimo ili kuimarisha sera ya kilimo kama uti wa mgongo wa Tanzania.
Mageuzi ya mifumo ya kisiasa na uwepo wa utawala bora;
Kuwepo kwa uhuru wa kuzungumza na kuruhusu vyombo vya habari kufanya kazi bega kwa bega na serikali hasa katika kufichua maovu pia kuwe na Kamera na vifaa vya teknolojia katika kipindi cha uchaguzi, hata baada ya uchaguzi. Mfumo wa kisiasa wa Tanzania unapaswa kubadilika ili kuleta maendeleo,viongozi wengi wamejificha katika kivuli cha uzalendo ilihali hakuna uzalendo ndani yao na hata wale wenye uzalendo wa kweli ni ngumu kuubeba uzalendo ndani ya vifua vyao kutokana mifumo husika inabana kuwa na falsafa bora badala yake uwepo wa falsafa ya watu wachache kwa maslahi ya wachache. Na hii ndo sababu ya usaliti ndani ya Taifa,Hata wale wenye uzalendo hukengeuka sababu ya mifumo mibovu iliyopo kiongozi ni mtu hivo anaweza kupoteza maisha ila mifumo ikiwa ya wazi, yenye kukosolewa, shirikishi itaweza kuishi katika uzalendo.
Vyombo vya habari, asasi za kiraia na Tasisi mbalimbali kwa pamoja ziungane kutoa elimu kwa wananchi juu ya ushiriki wao katika siasa, maendeleo ya jamii na kufanya maamuzi;
Wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya serikali yao, na hata wale wenye elimu bado wana hofu na wasiwasi wa kuzungumza juu ya uovu. Suala la utoaji huduma za jamii ni jukumu la serikali inapotokea majukumu hayo hayatekelezeki ni jukumu la wananchi kudai haki zao aidha katika huduma za afya, elimu au uboreshaji wa miundombinu. Wananchi wanapaswa kuwa tayari katika kushiriki midahalo ya kuijenga Tanzania imara Aidha kwa kukosoa au maoni. Vyombo vya habari vinajukumu la kuhamasisha uhuru wa kuzungumza ili kuleta Maono ya kibunifu katika kujenga Tanzania chanya.
Mageuzi ya kisiasa yananzia chini kwa raia kwa kufanya maamuzi sahihi nani awe kiongozi na nani asiwe kiongozi. Vilevile wananchi wanapaswa kuunga mkono Juhudi za vyombo vya habari vinavyofichua uovu unaendelea nchini. vilevile asasi za kiraia zinawajibu wakufanya kazi ya kuelimisha jamii kwa manufaa na maslahi ya kujenga demokrasia na utawala bora.
Hivyo basi, jukumu la kuijenga Tanzania imara ni jukumu la wote, utayari na kujitoa ndio kiini cha msingi cha mafanikio.

Upvote
5