Ubosi unanifanya nisiolewe, umri unazidi kusonga

Ubosi unanifanya nisiolewe, umri unazidi kusonga

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Tangu nimalize harakati za masomo ni miaka 6 sasa. Wenzangu wote niliyokuwa nao ama wameolewa na kupata watoto ama wamepata watoto nje ya ndoa.

Mimi tangu nikiwa mdogo na kwa maadili niliyolelewa niliapa kutokuzaa nje ya ndoa. Lakini mpaka sasa nina miaka 33 sijapata mume wa kunioa.

Mbaya zaidi kwa sasa nina cheo kazini kwangu, basi kila mwanaume ananiogopa. Hapa nauona uzee unasogea sina mume wala mtoto.

Najiuliza, nivunje kiapo changu cha kutokuzaa nje ya ndoa ama niendelee kusubiria mume nisiyejua atapatikana lini na huku umri unaenda?

Niko njia panda jamani naombeni ushauri.

NB: Sexless siyo mtu ni taasisi iliyosheheni KE na ME
 
Sexless,

Waonekana unachagua sana MTU wa kuishi naye. Kuwa boss sio sababu bali maadili ya mke kwa mume. Je unavyoishi unavutia wanaume kwa style Yako ya maisha? Je unakua mnyenyekevu kwa wafanyakazi wenzako? Je umejiwekea u tayari wa kua approached? Usivunje kiapo chako japo sijajua km hujapata Mtt je mpenzi pia huna na hujawahi kufanya mapenzi? Ni hayo
 
Mi sidhani kama wanaume wanakuogopa ila kwa jinsi unavyojiweka ndo tatizo, either unavaa kibibi bibi, na wanaume wengi hawapendi kibibi, najua unakuwa unaona unavaa nguo za heshima bali pia unavaa kibibi.

- Jaribu kuishi maisha ya kawaida na si ya kisomi ili uwe sawa nao

- Always tabasamu usiwe kila kitu serious hapana usikute ulishapendwaga mda mrefuu sema tuu umepishana na gari la pesa

- Punguza kuchagua watu Wenye hazi zako tuu ndo uwe nao kwa kuogopa wale makapuku eti wanakuja si kwa mapenzi bali kutaka mali zako

_ Unapoelekea utakuja ku-adopt Mtoto ili tu uwe na Mtoto au utamlipa mwanaume ili akuzalie Mtoto

*U still have a time to back up ur brain and change ur perception about gentleman [emoji12] [emoji12]
 
Uboss wako wala sio shida kama utampata aliye na Hekima na wewe ukajishusha kwake huwezi Amini maisha yaweza kuwa matamu balaa, tatizo vijana wengi huogopa wanawake wenye Uwezi Kifedha/Kikazi kwa sababu Vikwazo hawataki kuelekezwa hata kama wamekosea ni wepesi kusema tuachane kwa visa vidogo tu!

Huwa wanapenda wawe juu ya mwanaume kimaamzi na hakuna kitu mwanaume asichotaka kama kumilikiwa kimaamzi Nikiombe kama utabahatika kumpata aliyesahihi yawezekana ikiwa ni mimi Kubali kijishusha hakika mtaishi mlelea mwanaume ni kama mtoto Ukimbembeleza usimsemee kwa sauti ya ukali nakuhakikishia huyo ni wako milele ila ukimfokea tu! Umemkosa.
 
1. Unapotoka nje ya mazingira ya kazi usiendelee na ubosi wako

2. Jichanganye kwenye makundi mema baada ya kutoka kazini kama wewe ni mkristo nenda kwenye vyama vya kitume au kwaya.

3.Jitahidi kuwa myenyekevu kwa watu waliokuzidi umri na tabia yako isomeke hadharani kuwa ni njema

4.Usiishi maisha ya juu sana kama kuendesha gari masaa yote kwani neema za wanaume unazikosa saa nyingine unapotembea kwa miguu ndio waoaji wanakuona na kuanza kukufukuzia

5. Usipende kuvaa vitu vya garama saana kwani kuna wanaume wema wataona wakikuoa utawaingiza hasara hata kama ana kipato

6. Epuka sana kuwa wa bandia kama kubadilisha ngozi na kuvaa madude mengi artificial kwani kuna wanaume wengi hutathmini mwanamke aliyebadilisha ngozi kuwa hata tabia yake anaweza kuibadilisha kama kinyonga jinsi apendavyo na ajiamini na uzuri aliopewa na Mungu

7.Usipende kukosoa wanaume hadharani kwani kwa yule unayemkosoa kuna wengine wanakufuatilia kwa siri bila kukuambia na ukiona kitu kidogo tuu gubu la kufa mtu basi na wao wanajitoa kiulaini

8. Epuka sana kufikiria kuolewa na msomi mwenzako ama tajiri bali yeyote utakayempenda na anayekupnda kwa dhati na mwenye tabia njema anaweza kukufaa na mkaishi maisha mazuri na ya amani kuliko msomi mwenzako ambaye kwanza kumpata inakuwa kazi kwani baadhi huoa ambao hawajasoma kwa sababu hushuhudia live vituko vinavyofanyika vyuoni

9. kubali utumwa na kamwe usishawishike na wanaharakati wanataka kuwa sawa na wanaume

10. Kumbuka kuwa katika muungano wowote kila mtu lazima apoteze sehemu ya uhuruwake na kupokea mapungufu ya mwenzake na kuyavumilia. Hivyo usitarajie mtu ambaye yupo pafect kama malaika ndio akuoe utakosa wale ambao uliowakataa kwa kusema sii kiwango chako masi kama bado wapo warudie kwa unjenyekevu laa sivyo "imbombo ngafu""
 
Kuna dada nilisoma nae yupo temeke Hosp ni midwives (mkunga) hana mtoto kila siku analia hajawah pata ata mimba akatoa au kuolewa analiaga sana anapokuja mtu w kujifungua chini ya miaka 25..... Yeye ana miaka 35 sasa
 
Ewe dada unaweza kuwa kila siku unamtafuta mchawi kwann huolewi, kumbe mchawi ni wewe mwenyewe.<br /><br />Kilomita za umri zinasonga wewe unazidi kuchubua magoti kwenye nyumba za ibada ukiomba upate mume, lkn kumbe tabia zako ni kama bulldozer inayosukumia mbali.

Haya maneno nmeyatoa kwenye uzi wako " nkisikia I drink socially"
 
Back
Top Bottom