DOKEZO Ubovu wa Barabara ya Mbagala - Mbande ni kitegauchumi

DOKEZO Ubovu wa Barabara ya Mbagala - Mbande ni kitegauchumi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest


Ubovu wa Barabara kutoka Mbande kwenda Msongola imekuwa ni kama kitega uchumi.

Ni Barabara ambayo haijengwi Bali huchongwa tu kwa greda tu kwa muda Kisha huaribika tena na kurudiwa kuchongwa mfano kipindi hiki cha masika wamechonga kabla mvua hazijaisha imechongwa tena na tayari imeshaharibika yani kwa mwaka huchongwa Mara Tatu au Mara nne.

Mamlaka hawaoni kuwa hii ni biashara na upotevu wa pesa za mlipa kodi kwakuwa Hakuna kampuni inayofanya kazi Bure!
 
Back
Top Bottom