Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni baada ya kuonekana akimuhujumu Rais, akihubiri na kuchochea chuki na migawanyiko ya kisiasa yenye mirengo kikabila na upendeleo wa watu wa kabila na eneo lake la Milima Kenya.
Naibu wa Rais amekiuka sheria na misingi ya kikatiba ya Kenya ya kua nembo ya umoja wa Taifa na kiunganishi cha umoja wa Kenya. Badala yake Naibu Rais huyo wa Kenya, Rigathi Gachagua a.k.a RigGy ameonekana akichochea chuki na migawanyiko serikalini na kumlaumu Rais kwa kuwajumuisha waKenya wa maeneo mengine kwenye serikali anayodai eti hata hawakuchangia vya kutosha kuipata wakati wa uchaguzi 2022.
Kwa katiba mbovu ya Kenya, hiyo inatosha, na ni miongni mwa sababu muhimu zitakazo tumika kumg'oa naibu huyo wa Rais mamlakani.
Na kwasasa, joto la kisiasa liko juu mno, ubabe wa kisiasa na vitisho vya wazi wazi, usaliti wa kambi moja na nyingine, malumbano ya kuhujumiana na kuihujumu serikali kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na kuligawa Taifa kwa misingi ya kikabila na maeneo, utadhani kuna uchaguzi wiki ijayo. Joto la kisiasa ni kali mno. Hakuna kuaminiana tena.
Mbaya zaidi hata ngome yake Naibu wa Rais ya huko Mount Kenya wamegawanyika na tayari wengine wanaunga mkono hatua za kitaka kumbandua. Wengi wadai amejitakia mwenyewe, huku ngome za Rais kote nchini zikiungana na wale wa upinzani waliojumuishwa serikalini ambao naibu wa Rais ndio hasa anawananga, na kuapa kumbandua naibu huyo wa Rais ndani ya kipindi kisichozidi wiki mbili zijazo.
Prof. Abraham Kithure Kindiki waziri wa mambo ya ndani kenya, na Govenor wa County ya Laikipia Anne Waiguru wanatajwa kurithi nafasi hiyo, endapo singombingo hii ya kabokamchizi itafanikiwa.
Je, huu ni usaliti? Au ni miongoni tu mwa athari za ubovu wa katiba ya Kenya au maandalizi ya mapema ya uchaguzi wa 2027?
Je, Naibu wa Rais wa Kenya ndugu Rigathi Gachagua, anaweza kunusurika kwenye jaribu hili la kikatiba linalomzonga, na Kenya itakua na sura gani baada ya hapo?🐒
Mungu Ibariki Tanzania