Amaizing Mimi
JF-Expert Member
- Feb 2, 2019
- 489
- 1,102
Napenda kutoa malalamiko yangu kwa bank ya MCB.Hii bank kitengo chao cha huduma kwa wateja hakina msaada wowote kwa sababu baadhi ya namba hazipatikani na namba inayopatikana simu haipokelewi.Ni muda wa wiki moja sasa kila nikijaribu kuwapigia simu haipokelewi kwa zaidi ya saa moja.Hata makampuni ya simu za mikinoni ambayo yana wateja wengi lakini huwezi kusubiri saa zima bila simu kupokelewa.Nawashauri wabadilishe mfumo wao wa huduma kwa wateja kwa sabau mfumo wao wa sasa ni kero kubwa.