Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
RC Chalamila
Nimesafiri kutoka kwetu "Sumbawanga Town" nikaja Dar kumsalimia bibi huko Gezaulile Kigamboni.
Kutoka Posta nilipitia Feri nikapanda pantoni, kisha basi kwenye kituo cha manasi cha Kigamboni Feri.
Taarifa nilizokutana nazo ni kwamba watumiaji wa stendi ya mabasi Kigamboni Feri wanamtafuta "RC Makeke" Chalamila awatembelee.
Ukitoka kwenye pantoni kuelekea Kigamboni lazima upande mabasi, boda na bajaji zinazopaki stendi ya mabasi Kigamboni Feri.
Vivyo hivyo, ukitoka Kigamboni kati kwa mabasi, boda na bajaji na unataka kuvuka kuelekea Posta Mpya lazima ushuke stendi ya mabasi Kigamboni Feri.
Sebule za pantoni abiria wanakosubiria usafiri zinavutia.
Lakini stendi ya mabasi Kigamboni Feri imejaa uchafu, makorongo, msongamano na uvundo.
Wananchi waloongea nami wanasema kuwa imani yai ni kwamba "kama yule RC makeke aitwaye Chalamila akitutembelea Kigmboni tunaweza kuamka."
Nimechukua picha moja kuonyesha hali ya stendi ya mabasi Kigamboni Feri ilivyo.
Msongamano wa mabasi ni mkubwa. Ushuru unakusanywa. Lakini maboresho hakuna.
Ni kama dhana ya mipango miji haifahamiki kwa viongozi wa serikali huko Kigamboni, tena mita 300 kutoka Ikulu ya Magogoni.
Huu ni ujumbe kwako "RC Makeke" wa Dar es Salaam.
Mjumbe hauwawi.