Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha Mjini ni Monaban, Gambo ama Kalisti

Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
acha ukabila usiwe serious sana na maisha utapotea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Joto likiwa limepanda hadi kufikia nyuzi 360 kwa wagombea wanaotajwa kuwania nafasi hiyo, wananchi wa jimbo la Arusha Mjini wanajadili nani anafaa kuwa Mbunge wao.

Wakati hayo yakiwa yaendelea Arusha Mjini, Mbunge wa sasa Godbless Lema naye ametangaza kutetea nafasi yake kupitia Chadema.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kisiasa wanadai kwamba mvutano mkali uliopo kwa sasa ni ndani ya CCM kati ya mfanyabiashara mkubwa na aliyejijengea heshima kwa jamii na ndani ya CCM, Philemon Mollel (Monaban), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, anayetajwa kuwa kiongozi Kijana mwenye kasi kubwa na aliyekuwa Meya wa Arusha Kalist Lazaro "chaguo la wakubwa" huyu amejijengea heshima kwa kusimamia miradi ya Serikali akiwa upinzani.

Hata hivyo, Makada hao hadi sasa hakuna aliyejitokeza hadharani kutangaza kuwania nafasi hiyo pengine kwa kuogopa mkono wa Mangula ama Bashiru, wakisubiri kipyenga kupulizwa.

Wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ila hawapewi nafasi kubwa ya ushindani ni pamoja na Justine Nyari, Mosses Mwizalubi, Dkt. Batilda Burian, Mustafa Panju, Mwanasheria Edmund Ngemela,Thomas Munis na wengine ambao bado wapo mafichoni wakiwemo wafanyabiashara.

Wakati joto likizidi kupanda nani awe mbunge wa Arusha Mjini, jana Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Arusha imekaa kitako kwa zaidi ya saa 6 ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kinadaiwa kumjadili mmoja wa makada wake anayetajwa kuwania nafasi ya ubunge jimboni hapa kuanza rafu mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Monaban kakatwa mkia huyo!
 
Wakisimamisha Gambo Jimbo litarudi kwa Lema,labda nguvu kubwa Sana na hata kuua raia itumike kwa vile Gambo aliivuruga Arusha na kumtesa mbunge wao kwa lengo la kumkomoa,Hilo Kila mwana Arusha analijua japo nahisi yailikuwa Ni maelekezo kutokana Kona flani,kwa huu upuuzi fanyia Jimbo lingine ila siyo Arusha watu wake wanakiwango cha juu cha uelewa wa mambo ya kisiasa na haki zao tofauti na majimbo mengine nchini Tanzania.

Calsti angeweza kuleta upinzani kwa Lema,ila kosa alilolifanya Ni kuhama CDM akafikiri yy ndo alikuwa diwani mwenye nguvu na mvuto wa kisiasa kuzidi madiwani walobaki CDM na hata kuwazidi wale alowashinda kwenye kura za maoni pindi akiwa CDM.
Alitakiwa kukomaa ndani ya CDM na kuingia kwa mchujo wa ndani ya chama chake Nina hakika angemshinda Lema.
Kuna baadhi ya kauli zimeanza kusikika kwenye kata yake aloiacha kuwa jamaaa alifikia Bei akakubali kununulika,hii si dalili nzuri.

Monabani ataweza kuleta upinzani mkali Sana kwa Lema Kama Lowasa hatakanyaga kwenye kampeini zake,kwa Arusha hawapendi watu wanao onekana kuwasaliti pindi wanapopitia mapito magumu.
wanahitaji mtu jasiri na asiyekata tamaa.Monabani alimtikisa Lema kidogo,kwa CDM Arusha CCM ijupange Sana,juzi nikiwa maeneo ya Sakoni mzee mmoja akasema tumeletewa Steve ili ajaribu kumung'oa Lema kwenye ubunge,atajaribu lakini hataweza.
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
Wewe jamaa kweli ccm imekutoa akili kabisa. Katiba imeruhusu raia mwenye sifa kugombea popote pale ila tu hasivunje sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I

Lema anakutia tumbo joto mpaka umegeukia ukabila sio?

Mzee weka siasa kati,ubaguzi kando!

Lema atawapiga 3-0 asubuhi saa nne!
 
Kuna kijana machachari mzawa Hillary Loishiye amekua akitajwa tajwa sana kuchukua nafasi hiyo maana wazee wote wanaonekana kumshindwa Lema sasa wanampa kijana mwenzake.
IMG-20190814-WA0031.jpeg
IMG-20190814-WA0029.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya hao sijaona hata mmoja wa kumtoa Lema hapa Atown.
Akisimama Mona,na Lowasa asitie mguu baada ya kuwasaliti anaweza kumtoa jasho Lema.
Lema tatizo ana vijana wengi na ana mvuto kwa akina Mama,kuhakikisha hayo pita soko la Samunge kwa hao wa mama wanaopanga vitu chini sokoni kwa juu,Kama Kuna ajenda ya kumuongelea Lema utasikia visauti vidogo vkisema watuachie kijana wetu,wao walikula tokea zamani bado hawajashiba tu,yerewiiii.
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
Kwa akili hizi endelea kuwa CCM tu. Yaani Sugu ana asili ya MBEYA? Alli Keissy ana asili ya Rukwa. Ayesh ni Mfipa? Said Morad ni Mkagulu? Mnyika ni Mzaramo? Kiluswa ni Mmang'ati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za Arusha mwaka huu chama dola kitachukua jimbo, kimbembe ni nani wakumsimamisha maana sasa hivi kunaonekana uwepo wa makundi mbalimbali kila mmoja akitaka asimame yeye ama kikundi chake. Mbunge wa viti maalumu wa sasa Catherine Magige ni moja ya watu wanaotajwa sana japokua ushawishi wake sio mkubwa. Tusubiri muda utasema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
Wabunge wa Dar wote wahamiaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kutumia tume ya wakurugenzi makada ccm itashinda ila sio umma
 
Joto likiwa limepanda hadi kufikia nyuzi 360 kwa wagombea wanaotajwa kuwania nafasi hiyo, wananchi wa jimbo la Arusha Mjini wanajadili nani anafaa kuwa Mbunge wao.

Wakati hayo yakiwa yaendelea Arusha Mjini, Mbunge wa sasa Godbless Lema naye ametangaza kutetea nafasi yake kupitia Chadema.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kisiasa wanadai kwamba mvutano mkali uliopo kwa sasa ni ndani ya CCM kati ya mfanyabiashara mkubwa na aliyejijengea heshima kwa jamii na ndani ya CCM, Philemon Mollel (Monaban), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, anayetajwa kuwa kiongozi Kijana mwenye kasi kubwa na aliyekuwa Meya wa Arusha Kalist Lazaro "chaguo la wakubwa" huyu amejijengea heshima kwa kusimamia miradi ya Serikali akiwa upinzani.

Hata hivyo, Makada hao hadi sasa hakuna aliyejitokeza hadharani kutangaza kuwania nafasi hiyo pengine kwa kuogopa mkono wa Mangula ama Bashiru, wakisubiri kipyenga kupulizwa.

Wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ila hawapewi nafasi kubwa ya ushindani ni pamoja na Justine Nyari, Mosses Mwizalubi, Dkt. Batilda Burian, Mustafa Panju, Mwanasheria Edmund Ngemela,Thomas Munis na wengine ambao bado wapo mafichoni wakiwemo wafanyabiashara.

Wakati joto likizidi kupanda nani awe mbunge wa Arusha Mjini, jana Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Arusha imekaa kitako kwa zaidi ya saa 6 ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kinadaiwa kumjadili mmoja wa makada wake anayetajwa kuwania nafasi ya ubunge jimboni hapa kuanza rafu mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado kuna mfanyabiashara anataka kuacha biashara zake na kwenda kutumikia SIASA? Waulize mashamba ya maua ya LA FLEU DE L'AFRIQUE yako wapi ndiposa wajipime kama mitaji yao waielekeze kwenye kukuza biashara walizo nazo au wawekeze kwenye SIASA
 
Mgombea atakuwa Dr. Mosses Mwizarubi na hatimaye atakuwa mbunge na waziri kijana kabisa kwenye serikali ijayo ... mark my words
 
kwani GAMBO ni wa Arachuga au kwasababu ni RC wa Arachuga??
 
Back
Top Bottom