Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Kuna msemo usemao, Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno!.
Hao wenye moyo ni wazalendo wa kweli wa nchi yetu.
Tangu baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, amekufa na Azimio lake la Arusha lililoweka miiko ya uongozi, sifa ya uongozi wa umma enzi za Mwalimu ilikuwa ni uzalendo wa mtu kwa taifa lake na kujitoa kwake kutumikia jamii, Lakini sasa sifa kuu ya uongozi ni kiwango cha ukwasi mtu alionacho na kiasi gani anaweza kugawa kwa wajumbe na kukichangia chama!. Hivyo ili kumpima mtu kiwango cha ukwasi wake, baadhi ya vyama vimeweka viwango vya juu vya fedha za kujaza fomu ya kuombea uongozi, kuanzia 100,000, 500,000, 1,000,000 hadi 5,000,000 kwa baadhi ya nafasi!, hivyo kama wewe ni lile kundi la akina "pangu pakavu", hohehahe mwenzagu na mimi, huna kitu!, pita mbali kabisa na uongozi wa umma!.
Kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Eala, nimeshuhudia utitiri wa wagombea zaidi ya 186 Kuwania nafasi 9 za uwakilishi, kati ya hizo nafasi 6 ni za CCM, 3 za upinzani.
Hivyo mimi kama Mtanzania Mzalendo, Natoa mchango wangu kuhamasisha uzalendo, kwa chama changu CCM, na nchi yangu Tanzania, kwa swali moja muhimu, kwenye uongozi wa umma, jee turudishe mtindo wa kwanza kuwatafuta wazalendo wa kweli wa nchi hii, ndipo kisha tuangalie sifa na vigezo, wakikidhi vyote viwili ndipo wateuliwe kwenye uongozi wa umma.
Sifa kuu ya kwanza iwe ni uzalendo, na uwezo hata kama hawana kitu, au tuendelee kuwateua wenye kitu ndio watuwakilishe hata kama hawana uwezo?.
Bandiko hili ni bandiko elimishi la kukisaidia chama changu jinsi ya kupata competent people kukiwezesha chama kuwatambua hao competent people na kututeulia watu wenye uzalendo wa kweli, kipimo cha Uzalendo wa kweli, ni mapenzi ya kweli na ya dhati kuitumikia nchi yako na hata ikibidi, kuutoa uhai wako kuifia nchi yako ipone hivyo unakuwa umeifia nchi yako.
Ukiona jina la mtu yoyote, anataka uongozi wa umma, kabla hata hatujajua uwezo wake, swali letu la kwanza liwe ni "Jee mtu huyu ni Mzalendo wa kweli wa taifa hili?" Uzalendo wake ni upi?. Ndipo tuje kwenye jee ana kidhi sifa na vigezo?, na la mwisho ni liwe, jee ana uwezo?. Huu uwezo unapimwa kwa a track record ameishawahi kufanya nini?.
Mtu akitaka uongozi wa umma, afanyiwe kwanza uzalendo test, akipita ndio sasa zije sifa na vigezo, akikidhi, atauliwe hata kama hana fedha na akifeli atoswe hata kama ni bilionea na ana ukwasi mkubwa!.
Tuendelee kutegemea tuu mgombea kukidhi sifa na vigezo, mfano kwenye ubunge wa Bunge la JMT, kwa upande wa elimu sifa ni mtu kujua kusoma na kuandika tuu, hivyo hata darasa la 7 anaweza kuwa Mbunge mzuri tuu wa Bunge la JMT, lakini kwenye ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, yaani EALA, wabunge wale ni wawakilishi wa nchi na sio wawakilishi wa watu, hivyo wawakilishi wetu, ni lazima wawe na sifa za ziada za kwenda kuwakilisha nchi na sio tunapeleka baadhi ya wabunge mabubu, ambao michango yao haionekani kwenye hansard zozote za Bunge hilo, wakati baadhi ya majirani zetu, wanatamba kwenye bunge hilo, utadhani Watanzania, hatuna uwakilishi!.
Nikijitolea tena mfano mimi mwenyewe, katika miaka yangu 30 ya uandishi wa habari, kuna mengi niliandika, niliotangaza, na nilioshauri, yamelisaidia sana taifa langu, naomba kwa sasa niyasitaje wala kuyaorodhesha, nisije nikaonekana najifagilia.
Katika miaka yangu 30 ya uandishi wa habari as nobody, kuna mengi nimeshauri, yalifuatwa yamesaidia, yaliyopuuzwa matokeo tunayajua, hivyo kila kunapotokea ushauri mzuri wa kusaidia na ukapuuzwa na matokeo ya kupuuzwa huko ni majanga, na kuishia kuumia, sasa nimefikia uamuzi na kusema "kuendelea kuumia basi!", nimeamua kujitosa ili kwenda kuisaidia nchi yangu.
Sasa baada ya miaka 30 ya uandishi wa habari as nobody kuna vitu nimeshauri kwa kuaandika, na kutangaza na vikapuuzwa simply because I was nobody!. Unapojitolea kusaidia mambo as nobody na mengine yakapuuzwa na kuleta majanga unaumia sana!. Sasa kumetokea fursa ya kuwa somebody, nimejitathmini na kujiona, kwa sasa mimi kama mwandishi wa habari na mtangazaji mwandamizi, mwanasheria, na wakili wa kujitegemea, kuna mahali nitaweza kulisaidia zaidi taifa langu, kuliko hata hiki ninachofanya kwenye sekta ya habari.
Hatua ya kwanza ni kubadili status ya kutoka kuwa nobody na kuwa somebody, hivyo nitakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa
kubisha hodi na kuingia popote kushauri, ikiwemo kumsaidia Rais wa JMT, ambako ni kulisaidia taifa.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT anaweza kushauriwa vyovyote na yeyote, lakini kwenye kufikia maamuzi, rais atafikia maamuzi, yeye kama yeye, na sio lazima, apokee ushauri wa yeyote.
Ukijitolea kumshauri rais wa JMT jambo lolote, katika ushauri huo, weka na matokeo ya kupuuzwa kwa ushauri wako huo, hivyo ukitoa ushauri, wewe unakuwa umetimiza wajibu wako, ushauri wako usipofuatwa, hiyo sasa sio juu yako, ila unaweza kuyatumia matokeo ya kupuuzwa kwa ushauri huo kama shamba darasa ili next time ukitoa ushauri, uzingatiwe.
Kwa vile mchakato wa kuwapata wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, umetangazwa, nashauri ili taifa lipate wawakilishi wazuri na makini, tufanye mambo mawili yafuatayo
Unaionaje ushauri huu?.
Karibuni.
Paskali.

- Kwa waliokuwa wawakilishi wetu kwenye Bunge hilo ambao wanataka kuwania kuendelea kwa awamu yaa ya pili, waulizwe katika uwakilishi wao, ndani ya Bunge hilo kwa miaka 5 iliyopita, wamechangia nini na wamelisaidia nini taifa?. Taarifa zao ziandamane na uthibitisho wa hansard ya Bunge hilo, ili wale waliotuwakilisha vizuri, ndio wapewe fursa ya kugombea kipindi cha pili, tuwarudishe, na wale mabubu, tuwashukuru kwa uwakilishi wao kwa kuwaambia asante, tuwapumzishe!. Baada ya kuiingiza DRC ndani ya EAC na ujio wa AfCFTA, hizi sio zama za Tanzania kuwakilishwa na mtu ili mradi ni mtu, we real need competent people kutuwakilisha.
- Watu wapya waliojitokeza kutaka kutuwakilisha, kila mmoja atakiwe kupeleke a write up hata ya page 1, yenye ku set ajenda za Tanzania kama nchi anazotaka kwenda kuzipigania kwenye EALA na kupewa dakika 5 za kujieleza kwa lugha ya Kiingereza safi kilicho nyooka!. Moja ya sababu za baadhi ya wawakilishi wetu kuwa mabubu kwenye mijadala ya kuchangia hoja za Bunge la EALA, ni Lugha.
Unaionaje ushauri huu?.
Karibuni.
Paskali.