Mbunge anayemaliza muda wake Said Nkumba,jana alitangazwa rasmi kama ndiye mshindi halali wa kura za maoni ndani ya CCM hasa kufuatia kata za Kipili,Kitunda na kiloli kuwasilisha matokeo yake!
Soma hapa kama Gazeti la Mwanahalisi leo lilivyoandika
"Sikonge, Msimamizi Bakari Mfaume alitangaza matokeo yakionesha mbunge aliyekuwa akitetea kiti chake, Said Nkumba ameongoza kwa kura 2,633 akifuatiwa na Mlenzi Kakunda aliyepata kura 2374 huku Rukia Agustino akipata kura 832.
Alisema matokeo hayo yalichelewa kutokana na kata za Kipili, Kitunda na Kiloli kuchelewa kuwasilisha ya kwao"
Ndugu yangu Sikonge,habari ndiyo hiyo,watoto wa mjini wanasema imetoka hiyo la sivyo na nyie fanyeni kama Iringa ambapo juzi CCM ilibadili matokeao na kumvua ushindi Dr Mgimwa na kumtangaza Mzee Kandoro kama ndiye mshindi;wananchi wakatishia kuondoka CCM na wenyewe wakafyata na kumtangaza tena Dr Mgimwa kama ndiye mshindi halali!
Awali mgombea Mlenzi Kakunda alitangazwa ndiye mshindi hata akapongezwa na watu wengi tu,iweje sasa avuliwe ushindi wake?