Mungu wangu. David Kapya mbona hakuniambia nimshauri jamani??Njia ya kwenda bungeni ina michongom
a na mshimo mengi kweli. Yule bwana mdogo Mkumba is very smart. Atamweza kweli?
Nkumba is not smart, alikuwa na advantage moja kwamba alikuwa anabebwa na baba yake kwenye kura za maoni. Mzee Nkumba alipoteza uenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora kwenye uchaguzi wa 2007, so Bwana mdogo Said Nkumba hana ujanja.
Kama umekuwa ukifuatilia mijadala, Nkumba amekuwa akilia kila siku kwamba Rostam Aziz ana agenda ya kummaliza. Wengine wanasema kwenye uchaguzi wa CCM 2007, RA alikataa kumuunga mkono Mzee Nkumba S. Nkumba, na matokeo yake Mzee alipoteza uenyekiti.
Kwa maoni yangu, kiti cha Ubunge Jimbo la Sikonge ni kama vile kiko wazi na mwaka huu Nkumba hawezi kuvuka kwenye kura za maoni. Mojawapo ya sababu za kutovuka ni ugomvi uliopo kati ya Nkumba na RA. Wengi walio kwenye nyadhifa za CCM mkoani Tabora wako pro-RA.
Siyo hilo, bado kuna maswali mengi ambayo yanahitaji majibu: Nkumba amefanya nini kwa kipindi cha miaka 10 ambayo amekuwa Mbunge? Barabara bado mbovu na hazipitiki nyakati zote. Barabara ya kutoka mkoani kwenda jimboni kwake (Wilaya ya Sikonge) ni matatizo matupu na hakuna ambaye anaongelea ujenzi wake.
Mwaka huu JK alienda Kitunda, akakwama ikabidi chopper itumwe kwenda kumchukua huko ambako alikuwa amekwama. Huko alikokwama ni barabara kuu inayounganisha mkoa wa Tabora na Mbeya na sehemu kubwa ya barabara hiyo inapita jimboni kwa Bwana Nkumba. Kama barabara hiyo ingeweza kuwa inapitika kirahisi mwaka mzima, Sikonge ingekuwa na maendeleo ya kibiashara kwa kuwa ili mtu aende Mbeya, lazima aende kwanza Tabora mjini, apande treni mpaka Itigi, then apande mabasi. Au aende mpaka Dodoma au Morogoro, then apande mabasi kwenda Mby. Kwa hiyo biashara inakuwa ngumu sana.
Wilaya ya Sikonge imekaa kushoto sana na wanahitaji sana barabara hiyo. Urambo wamekaa kushoto, lakini reli inawasaidia pindi ikiwa inafanya kazi. Pia sasa hivi wana barabara nzuri na inapitika mwaka mzima. Wilaya za Igunga na Nzega wameunganishwa na barabara kuu (Dar - Mwanza). Ni wilaya ya Sikonge tu ndiyo ambayo imebaki kama kisiwa. Inahitaji Mbunge mwenye vision na atakayeweza kuibana serikali ili wajenge hiyo barabara. Hilo linaweza kufanyika kwa kushirikiana na wabunge wa Chunya, Mbeya mjini na Mbeya Vijijini ambao wanaweza kufaidika na ujenzi wa barabara hiyo.