Ahhh Mkuu Elnino,
Nisahau wapi hayo mambo? Ninamiss sana "mahama" maana zamani pale Usupilo, Sikonge kama unakwenda Kisanga, kulia kulikuwa na mji wa Shangazi na mumewe Elia Masanja. Ukienda kumtembelea wakati wa likizo basi unakuta yameanguka, ni raha tupu. Nyumbani mzee alikuwa na miti mingi sana ya matunda kama mapapai, michungwa, mastafeli, matopetope, mapera, limau, maembe, miforosadi, minazi ............
Msituni ndiyo unakuta Nsungu, nkuni, matonga (tulipokuwa JKT Msange, watoto wa Dar walikuwa wanayala kama hawana akili nzuri), Nfulu, ....
Kuwinda ndenge vipi? Upile, Kigwaulima, Jorwe, titi ( wa mpotya mpotya, kwikala mkalambo Lu**ndo fyetete, mtwee pono. Mtaka kwa mponda kusema, lakini limvwa, ihhhh kusata....) Ahhhh, those was real sweet old days. Elnino memory yangu huwa inafanya kazi safi sana. Hivi yule Ndege anaitwa MTINDI, kwa kiswahili anaitwaje?
Turudi kwenye habari kuu. Kwa mwaka huu mie lazima nikiri kuwa sijajiandaa na sidhani kama hata ntakuja kugombea. Ntaanza kuangalia mipango kwa mwaka 2015 kama Mungu akipenda mwaka 2012 dunia isiishe maana wanasemasema sana. Kuna viongozi wazuri sana Sikonge ila tu wengi wakiondoka Sikonge basi wanasahau kabisa na kuja kukumbuka kurudi Sikonge kuomba ulaji tu. Hii haitawapeleka mbali kwani unakuta wanapitwa hata na Mwalimu wa shule ya Msingi, kijana Said (Hitler) Nkumba. Huyu Nkumba mwenyewe ni mshamba wa kutupwa jamani. Yaani pamoja na yote, kaja kujenga mzinga wa jumba kule Mole. Utafikiri anajiandaa akizeeka basi arudi kulima tumbaku. Sasa unategemea mtu kama huyu alete mawazo mapya kwa wananchi? Kama yeye mbunge anaenda kujenga Mole, basi walimu wa shule za msingi wakajenge Ntankwa kama siyo Utawambogo.
Umasikini na ujinga wa Sikonge, umeifanya Sikonge kuwa moja ya mihuli ya kuipigia kura CCM. Yaani Sikonge hata uweke NYANI kwa kiti cha CCM, basi ni kuwa watamchagua CCM. Nina uhakika kabisa, utasikia Wanyamwezi wanamsifia kuwa huyo nyani kapendeza sana ndani ya suti ile ya kijani na kwa hiyo atampigia kura. Siku Sikonge itaamka basi ujuwe CCM imekufa. Nina uhakika CCM kura yao ya mwisho kabisa itakuja kutoka Sikonge. Ubaya tu ni kuwa hela za kifisadi hazifiki kabisa Sikonge. OVYO KABISAAA...... Ila huwezi kushangaa hilo kwani unakuta mtu anajiona MATAWI sana na kisa tu ni kuwa anafanya kazi kwa Hemed Nassor au ndugu zake. "ahhh, sasa hivi mie ni Bishaushi na ninafanya kazi kwa Rashid Koronzo..........." Jamaa kakupigia kisuti cha kaki na ndani ana wake wawili........... Ka uswahili ndiyo kamejaa na kujifanya mtu wa dini saaana wakati dini yenyewe haifahamu.
Nilicheka siku moja mzee fulani kakutana na Sheik wa Sikonge. Aliposalimiwa "salaam Aleikum mwana Mbati......" Mzee akajibu kwa adabu sana (ingawa alikuwa mkristo) kuwa ".... waleka Muislaam." Hapa alimaanisha Aleikum Salaam ila hilo neno kwa Kinyamwezi linakuwa "kaacha Muislaam".
Bado nakusanya datas na ntakuja na habari kamili soon juu ya uchaguzi wa Sikonge.
Mapalamu ya kuchoka.
Muhanya..... (Mkuu)
Twende tukapige kazi tulichukue jimbo letu, mimi binafsi nina uhakika wa kuzoa kura vijiji vifuatavyo Sikonge, Ipole, Tutuo, Chabutwa, Mlogoro, Kabanga, Mibono mpya, Usunga I and II, Msuwa, Kininga, Kipanga, Kiloleri, Mkolye, Utimule.
Mzee naona ushavisahau vijini vyetu nini? ha ha ha - wakati tunakatiza kutafuta maembe, matonga ,tulantu na ntararii. :smiling: