Ubunge: Jina Irene Uwoya larejeshwa kwenye ubunge viti maalumu

Ubunge: Jina Irene Uwoya larejeshwa kwenye ubunge viti maalumu

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana JF,

Waswahili wanasema bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, ndio hivyo tena Irene vitu maalum vimwemwangukia, sipati picha itakuwaje huko bungeni. Tunaomsupport tunamwombea kila la heri kuleta utetezi mwema kwa watu wote.

Hongera Irene kwa kubwaga vigogo wengi.
Irene Uwoya apeta viti maalum vijana taifa, sasa kuingia mjengoni

Unaweza ukaanza kujizoesha kumuita kwa jina lake jipya, Mheshimiwa Irene Uwoya kwasababu mrembo huyo amepita kwenye kinyang'anyiro cha viti maalum vijana taifa.

Kupitia mkutano wa halmashauri kuu ya CCM uliofanyika mjini Dodoma kuanzia juzi, Uwoya amepata kura nyingi za kumwezesha kuingia mjengoni mwaka huu. Akiongea na XXL ya Clouds FM, Uwoya amesema awali katika kura hizo alifungana na mtu mwingine na hivyo ukafanyika uamuzi wa kumchagua mmoja.

"Niliweka mtu wa kunihesabia kura lakini tukafungana, tukajikuta watu wawili tumefungana lakini baadaye hatukutangaziwa majibu kwasababu kamati zilikuwa hazijakaa kuamua kwahiyo sasa hivi ndio nimepata
majibu," amesema.

"Tabora nilipita kwa kura nyingi sana na huku taifa pia nimepita kwahiyo namshukuru Mungu."

Naye mume wake, Hamadi Ndikumana ametumia mtandao wa Instagram kumpongeza mke wake kwa kuukwaa ubunge.

"Hongera sana mke wangu kwa ushindi uloupata, tumshukuru Mungu kwa kupokea maombi yetu na kukufikisha ulipo stahili. Kama nnavyo kwambia siku zote binadamu hukupenda pale wanapoona watapata faida wapo wengi ulikua nao karibu wengine uliwasaidia mda mrefu ila wakati uliwahitaji walijitenga nawe," ameandika.

"Kwangu ni faraja kubwa na naona kama Mungu alipanga hivyo kurejesha furaha ya penzi na ndoa yetu, siku chache tu zimepita nikirudi uwanjani baada mda mrefu pia kupata nafasi yakuwa karibu na familia
yangu. Namshukuru Mungu kwa kunirejesha karibu na familia yangu tena kwa kishindo kikubwa.Mungu azidi kukusimamia na akuongoze kataka nafasi hiyo mpya aliyo kupa muheshimiwa mbunge viti maalum kupitia chama chako cha CCM."

Chanzo: bongo5.com
 
duhh hii nchi tunarudia makosa yaleyale yanayotuumiza muda mrefu..hapa kilichofanyika ni sawa na wananchi kumpa kura diamond aanze kuimba kwa kichina just because watu wanajua anajua kuimba
Mtu mwenyeji wa dar anaenda kugombea sehem ambazo ni mgeni hivi tangu lini .... ila ndo tz hii tukiambiwa tuchague viongozi bora wa kuleta maendeleo sie tunachagua viongozi dhaifu ambao lengo lao kuu ni kupata mshahara, hata mkila mchanga wao haiwahusu...

Anyway naona watu wamepanda mapera wanategemea mchele huko mbele, anayeniona Mimi hater naomba ajiulize kichwani mwake maana ya political leader amfanyie reference huyo
 
Nampa hongera,lakini niwe muwazi...mkuu upo sawa kabisa huyu irene amefuata "COUNTING FIGURES" mule ndani bhasi...namimi nachosikitika tu CCM wameshindwa kutambua kuwa bunge lijalo la 11 chini ya serikali ya awamu ya 5 litakuwa gumu sana zaidi ya hili lililopita hivyo inabidi wapitishe wabunge makini na wenye uwezo wa kujenga hoja sana badala yake wametuongezea wabunge dhaifu maana mtu kama irene sidhani kama ataweza kwenda sawa na kina TUNDU,MNYIKA,KAFULILA...kweli CCM wameishiwa viongozi wanawake na jembe lao la kike(Ester Bulaya) limewakimbia limekuja upinzani matokeo yake wanaanza kusimamisha wagombea wa d'zain hiyo!
 
Huyu ndikumana angejua ndo anazidi kumpoteza huyo demu wala asingeandika hivyo
 
Huyu ndikumana angejua ndo anazidi kumpoteza huyo demu wala asingeandika hivyo

Hivi kufuatana na kufunga ndoa Halali hivi huyu si ni mrudi tayari, mme Mrudi , mwanae, mrudi, baba na mama washamuaga mbele ya kanisa kwenda Urundini Burundi-Bujumbura.
 
Hivi kufuatana na kufunga ndoa Halali hivi huyu si ni mrudi tayari, mme Mrudi , mwanae, mrudi, baba na mama washamuaga mbele ya kanisa kwenda Urundini Burundi-Bujumbura.

Duh! Wanaofaham watatuelezea
 
watakuja humu kulalama mbunge hatumuoni wakati wanajua wazi hiyo mtu ni wa dsm labda steps intertiment ihamie uyui
 
Mill 11 kwa mwezi nyumba ya kuishi bure umeme 24hrs bure, maji bure gari vx v8 anaendeshwa na dereva! hongera sana ccm ila bunge lijalo litakuwa na changamoto nying sana!
 
CCM naona tunajiandaa kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni. Si bure.
 
Yaani hili bunge sasa tutajaza wavuta bange na machangudoa
 
Yaani hili bunge sasa tutajaza wavuta bange na machangudoa
hii ni zaidi ya hatari, kumbe hakuna haja ya kusoma sana dili lipo nje nje , ni kujikweza ccm utapata ulaji
 
Back
Top Bottom