Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Ben,

Wewe ndiye uliyeanza kwa kuandika ulikuwa unaheshimu michango yangu. Hiyo ni weakness kubwa sana, inatumiwa na watu wanaotaka kuonewa huruma.

Wengine tunapojadili hoja we don't carer mwandishi aliandika nini jana. Unaweza kutumia maandishi ya nyuma kama tu kuna contradictions lakini sio kwa kusema eti ulikuwa unaheshimu mawazo yangu, who cares?

Andika hoja zako na songa mbele, unaheshimu mawazo ya mtu au hauheshimu hilo ni chaguo lako.

Double standards? sawa, zionyeshe hizo double standards ziko wapi na hilo ndilo la kujadili.
Kwako hiyo ni weaakness lakini cha kushangaza sana ya double standard huioni! Unapost gazeti unaloona lina habari yenye kuichafua CHADEMA zaidi unaacha hilo lingine kisha unakuja kujitetea kwamba ilitaka kupost baadae.Na hii ndiyo double standard unaposema Dr.Slaa kawaingiza wake za marehemu kwenye siasa ukijua wao ndio waliojileta kwenye siasa tena mwingine kaja kwa nia mbaya,KUICHAFUA NA KIHUJUMU CHADEMA na bado unaniuliza ni kuonyeshe hizo double standard.ya nini kupoteza muda mwingi hivi ikijitetea kama hutaki kuheshimiwa? Yaani una-type kujisafisha halafu unasema hutaki kuheshimiwa?

Pili,Hapo nilikobold, naomba usinipangie cha kujadili.Nani kakwambia nina muda wa kulijadili hilo?
 
Huu ni utetezi wenye kupoteza muda tu,you are so biased!

Halafu unakua mtu usiyeelewa,nani kawaingiza hao wanawake kwenye siasa? si wao wenyewe? au hapa nako unataka kusema ni kwa sababu tangia jana ulikua ukiliongelea hilo suala ndiyo maana hutaki kubadili mawazo?

Kuwa na msimamo hakumaanishi uendelee kushikilia lile baya la kuupotosha umma,kufikia hapo nadhani basi maana halisi ya Msimamo inasumbbua watu wengi sana.

Ila tafadhali naomba uaache kufikiria kwamba inawezekana kuna watu wanakuabudu humu ndani,please and please.Ondoa hayo mawazo.

Pia kuwa kwako katika forums muda murefu hajalishi sana bwana,mbona kingunge amekua kwenye siasa enzi na enzi lakini ameendelea kuwa kichefu chefu kwa wananchi na aibu kwa kizazi hiki?

Unaruka ruka huku na huku. Mimi nimekuambia siamini kuna watu wananiabudu na wala sitaki watu waniabudu. Pia sitaki watu waheshimu mawazo yangu maana hiyo ni weakness kubwa mno kuheshimu mawazo ya mtu. Utafikiri wale wa zidumu fikra za Mwenyekiti. Hakuna mtu mwenye yeyote hapa duaniani ambaye mawazo yake yote ni sahihi

Watu tunachofanya ni kukubaliana/kupingana na kilichoandikwa/hoja na sio kuheshimu mawazo ya mtu. Kama kuna watu unaheshimu mawazo yao, bado wewe ni very weak kwenye hoja, kifupi ni kwamba unawaabudu hao watu.

Binfsi sitaki kuabudiwa na mtu yeyeote kwahiyo hilo wazo la kwamba ulikuwa unaheshimu mawazo yangu lifute. Halinisaidii mimi kwenye nyanja hii ya kupambana kwa hoja.

Pia hii ya kukimbilia kila kitu kabla hata hujajua kusema ni cha mafisadi ni weakness nyingine. Usitoe judgement mpaka una data zote. Hapo inaelekea hata hukujua hiyo habari nimeitoa wapi na kwanini nimepost, wewe tayari umejenga conclusion yako. Hizo tunaita hoja za uyoga, unajenga conclusion kwa foundation mbovu. Ndio maana unaishia kuheshimu mawazo ya watu wengine kwi kwi kwi!!
 
Kwako hiyo ni weaakness lakini cha kushangaza sana ya double standard huioni! Unapost gazeti unaloona lina habari yenye kuichafua CHADEMA zaidi unaacha hilo lingine kisha unakuja kujitetea kwamba ilitaka kupost baadae.Na hii ndiyo double standard unaposema Dr.Slaa kawaingiza wake za marehemu kwenye siasa ukijua wao ndio waliojileta kwenye siasa tena mwingine kaja kwa nia mbaya,KUICHAFUA NA KIHUJUMU CHADEMA na bado unaniuliza ni kuonyeshe hizo double standard.ya nini kupoteza muda mwingi hivi ikijitetea kama hutaki kuheshimiwa? Yaani una-type kujisafisha halafu unasema hutaki kuheshimiwa?

Pili,Hapo nilikobold, naomba usinipangie cha kujadili.Nani kakwambia nina muda wa kulijadili hilo?

Hivi unaelewa maana ya double standards? Pitia hata Wikipendia ujifunze. Ulichoandika hapo juu hata kama kila kitu kingelikuwa kweli bado sio double standard. Inaweza kuwa ni bias lakini sio double standard. hayo maneno mawili ni tofauti.
 
Kazi kukimbilia wikipedia tu,ndiyo maana hoja zimedumaa na unakosea mpaka unafikia hatua ya kufikiria kunaweza kuwa na watu wa kukuabudu hapa.Umekosea sana.Nenda Dar hotwire mkuu.
 
Unaruka ruka huku na huku. Mimi nimekuambia siamini kuna watu wananiabudu na wala sitaki watu waniabudu. Pia sitaki watu waheshimu mawazo yangu maana hiyo ni weakness kubwa mno kuheshimu mawazo ya mtu. Utafikiri wale wa zidumu fikra za Mwenyekiti. Hakuna mtu mwenye yeyote hapa duaniani ambaye mawazo yake yote ni sahihi

Watu tunachofanya ni kukubaliana/kupingana na kilichoandikwa/hoja na sio kuheshimu mawazo ya mtu. Kama kuna watu unaheshimu mawazo yao, bado wewe ni very weak kwenye hoja, kifupi ni kwamba unawaabudu hao watu.

Binfsi sitaki kuabudiwa na mtu yeyeote kwahiyo hilo wazo la kwamba ulikuwa unaheshimu mawazo yangu lifute. Halinisaidii mimi kwenye nyanja hii ya kupambana kwa hoja.

Pia hii ya kukimbilia kila kitu kabla hata hujajua kusema ni cha mafisadi ni weakness nyingine. Usitoe judgement mpaka una data zote. Hapo inaelekea hata hukujua hiyo habari nimeitoa wapi na kwanini nimepost, wewe tayari umejenga conclusion yako. Hizo tunaita hoja za uyoga, unajenga conclusion kwa foundation mbovu. Ndio maana unaishia kuheshimu mawazo ya watu wengine kwi kwi kwi!!

acha kujizungumzia wewe tu,maanke nimegundua wewe ni mtu wakutaka attention kutoka kwa watu.Mkuu tuache tuendelee na mjadala maanke wewe ni mtaka attention for nothing! kama hutaki heshima si ungeignore niliyopost,check unavyo-sweat kujisafisha.kwi kwi kwi,mkulima kala mbegu,anatka kutuua njaa.Hebu tupishe tuendelee na mjadala mkuu.

Please tuondolee kiwingu sasa!
 
halahala vodple na macho ndugu zanguni. Mkumbuke kuwa katikati ya siasa hizi za wajane wa wangwe, kuna ugomvi wa asili baina ya wanawake hao tangu wangwe akiwa hai. Uhasama wao sasa unazidishwa na matukio na msiba huu. Na bado yatakuja mengi, subirini tu kwenye masuala ya mirathi, mtaona watakavyolumbana
 
Kazi kukimbilia wikipedia tu,ndiyo maana hoja zimedumaa na unakosea mpaka unafikia hatua ya kufikiria kunaweza kuwa na watu wa kukuabudu hapa.Umekosea sana.Nenda Dar hotwire mkuu.

Sasa hoja zilizodumaa ndio ulikuwa unaziheshimu? kwi kwi kwi!! kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Sawa mkuu nakubali kutokukubaliana na wewe na nimemaliza kwenye huu mjadala, wacha nihangaike na mengine maana mijadala mingine haijengi tija tena, siku njema.
 
Wakuu, Mtanzania na Ben, muko zaidi ya hapo mlipo, tusaidieni badala ya kutupotosha. Tunawategemea sana humu JF hivyo musipoteze muda na uwezo wenu kwa mambo yanayochelewesha mijadala muhimu. Nchi iko njia panda.
 
Dk Slaa ambaye alisisitiza kwamba hamfahamu Mariam kama mke wa marehemu Wangwe, alisema anasikitishwa na kauli yake ambayo anaamini kuwa imelenga kukichafua chama.

Hii arobaini aliyoifanya Mariam na Profesa Wangwe Dar es Salaam hatukuijua wala wao hawakutaka Chadema iijue," alisema.
Akifafanua alisema ingawa Mariam alitoa taarifa ya arobaini aliyoifanya Dar es Salaam, waalikwa katika taarifa hiyo ni wabunge kwa majina yao na sio Chadema kama taasisi.

Alisema pamoja na kasoro hiyo wabunge wa Chadema Suzan Lyimo na Grace Kihwelu walihudhuria kwa kofia zao lakini waliwakilisha chama kwa salamu ambazo zilisomwa na Lyimo katika hafla hiyo.

"Mimi Dk Slaa nilialikwa kwa ubunge wangu na sio ukatibu mkuu wa Chadema na Mbowe alialikwa kwa jina lake na sio uenyekiti wa Chadema vivyo hivyo wabunge wengine. Sasa Chadema inapolaumiwa tunashindwa kuelewa," alisema na kuendelea.

The most lame excuse one can ever give. Kama kweli Dr. Slaa aliamua kudharau hiyo 40 kwa vile hamjui huyo Mariam, vipi adharau hata uwepo wa Prof. Wangwe?

"Mimi namshauri Mariam akutane na wazee wamshauri kwanza badala ya kukurupuka na kutoa maneno ya kukipaka matope chama. Yeye anataka athaminiwe, atathaminiwaje kama yeye Mariam hataki kukithamini chama," alihoji.

Hivi hili ni onyo, vitisho au ndio utaratibu kuwa msaada kwa wajane utategemea na jinsi watakavyojipendekeza kwa viongozi wa CHADEMA?

Dr. Slaa, nakushauri kama umekosea jambo usiliongelee maana unapofungua kinywa unazidisha kuboronga.
 
Sasa hoja zilizodumaa ndio ulikuwa unaziheshimu? kwi kwi kwi!! kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Sawa mkuu nakubali kutokukubaliana na wewe na nimemaliza kwenye huu mjadala, wacha nihangaike na mengine maana mijadala mingine haijengi tija tena, siku njema.

Kama unachelewa namna hii kuelewa basi huko mbele taifa lina kazi.Unajua nilishikwa na mshangao wa mwaka kwamba muda woote huu bado huelewi?

Kaazi kweli kweli,ila mkuu kesho ulete gazeti lingine lakini uache kuwa biased.Pleaseee! Haya sasa tujenge taifa tuendelee na mjadala.Kwi kwi kwi!
 
Wakuu, Mtanzania na Ben, muko zaidi ya hapo mlipo, tusaidieni badala ya kutupotosha. Tunawategemea sana humu JF hivyo musipoteze muda na uwezo wenu kwa mambo yanayochelewesha mijadala muhimu. Nchi iko njia panda.

Mkuu,

Tafadhali onyesha nilikopotosha umma.otherwise wewe ndiye unaepotosha umma kwa kutaka kuwafanya waamini mimi ni mpotoshaji huku ukijua si kweli.Please buddy,come on and help me on this!

Anyway,niendelee na mjadala!

Btw: Hivi mkuu Kubwajinga,ulitegemea Dr.Slaa ake kimya eti kwa sababu mtu ni mjane yuko kwenye majonzi na anakichafua Chama? Huyo mwanamke angekua na majonzi ya kweli asingepata nguvu za kukubali kutumika kisiasa kukichafua chama.Ukitaka kuonewa huruma kwanza jihurumie,that's all!

Kweli wengi hamna nia njema na CHADEMA,yaani mkuu unataka Slaa akae kimya huku chama kikiburuzwa kwenye sewage? Wakuu mtasubiri sana,na CHADEMA walishaapa kupambana na wale wote wanaotumia kifo cha Wangwe kukipaka matope.
 
Date::9/29/2008
Mke mwingine wa Wangwe aibuka kumpinga mke-mwenza mdogo

Mke wa kati wa Marehemu Chacha Wangwe, Dotto Mohamed, ambaye anapinga maelezo ya mke mdogo Mariam Wangwe kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimetelekeza familia hiyo baada ya kifo cha baba watoto wao.
Na Kizitto Noya

KIFO cha Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe kinazidi kuibua mengi baada ya mke wake wa kati Dotto Mohamed kukana maelezo ya mke mdogo Mariam Wangwe kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitelekeza familia.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dotto alisema kauli ya Mariam ni nzito mno kuitoa sasa kwani anaamini matukio yanayoendelea baada ya kutokea msiba huo, ndiyo yanayoweka pazia la mawasiliano kati ya Chadema na familia ya Marehemu.

"Sijaisoma taarifa yote ila mtoto wangu ameniletea gazeti ambalo bado ninalo. Mimi ninashindwa kufikiria wala kuwaza kuanza kukilaumu Chama kwamba kimetutelekeza kwani ni mapema mno kufanya hivyo na wote bado tuko kwenye majonzi," alisema Dotto na kuongeza:

Nasema nashindwa kukilaumu chama kwa sababu tangu kutokea kwa msiba huo hakuna aliyetulia, familia bado ina majonzi, chama chenyewe bado kinalia na hata jamii inaendelea kumlilia Wangwe nasema familia yangu bado ina imani na chama na hatuwezi kukilaumu sasa," alisema.

Dotto alisema anaamini Chadema inaongozwa na watu wenye busara hivyo hawezi kuinenea mabaya kabla ya kuridhika kwamba viongozi hao wameanza kupingana na busara hiyo.
"Ninihitaji muda kupima hekima ya chama kabla sijakihukumu kwani kinyume chake nitakuwa sijakitendei haki," alisema.

Alisema mpaka sasa bado anaamini kuwa Chadema iko sambamba na familia ya marehemu Wangwe kwani hata kwenye arobaini iliyofanyika kijijini Komakorere chama hicho kilituma wawakilishi.
Mke huyu wa pili wa Chacha Wangwe anaishi jijini Mwanza na jana alikuja jijini Dar es Salaam kuwachukua watoto wake wawili waliokuwa wakiishi na Mariam, mke mdogo wa Wangwe.

Jana Dotto aliiambia Mwananchi kuwa katika safari yake hiyo pia amepanga kukutana na Mariam na kuzungumza naye ili ajue kiini cha shutuma zake kwa Chadema.

"Kuja kwangu Dar es Salaam ni pamoja na kuwachukua wanangu wawili ambao wamekuwa wakiishi na Mariam; katika ujio huo tutakaa tuzungumze anieleze kwa nini ameamua kuzungumza maneno hayo sasa,".

Alisema hata kama Mariam atafanikiwa kumshawishi aamini maneno yake, bado atahitaji muda kukubaliana naye kwani anaamni kuwa bado ni mapema mno kutoa shutuma hizo.

"Sisi bado tuna imani na Chama na hatuwezi kujua chama kinatuwazia nini hivyo narudia: ni mapema mno kutoa shutuma hizo kwani wote bado tuko kwenye majonzi," alisisitiza.Akizungumzia kauli ya Dotto, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema ndiyo aliyotarajia kusikia kutoka kwa familia ya marehemu Wangwe.

"Nafikiri kauli hiyo ndiyo niliyotarajia kutoka kwa familia ya Wangwe ninayemfahamu kwa sababu kama utakumbuka tangu mwanzo wa msiba, sisi (CHADEMA) tulikuwa tukisakamwa sana lakini tulikaa kimya kwa busara ili tusimkamate mchawi asiyetuhusu," alisema.

Dk Slaa ambaye alisisitiza kwamba hamfahamu Mariam kama mke wa marehemu Wangwe, alisema anasikitishwa na kauli yake ambayo anaamini kuwa imelenga kukichafua chama.

Hiki anacholalamikia kwamba Chadema hawakuhudhiria arobaini ya mume wake, nashindwa kuelewa. Kumbuka mimi nina miaka 60 na tangu nianze kufahamu arobaini, najua zinafanyika mahala alikozikwa marehemu.

Wangwe alizikwa Komakerere na arobaini yake ilifanyika huko na Chadema tulituma mwakilishi. Hii arobaini aliyoifanya Mariam na Profesa Wangwe Dar es Salaam hatukuijua wala wao hawakutaka Chadema iijue," alisema.
Akifafanua alisema ingawa Mariam alitoa taarifa ya arobaini aliyoifanya Dar es Salaam, waalikwa katika taarifa hiyo ni wabunge kwa majina yao na sio Chadema kama taasisi.

Alisema pamoja na kasoro hiyo wabunge wa Chadema Suzan Lyimo na Grace Kihwelu walihudhuria kwa kofia zao lakini waliwakilisha chama kwa salamu ambazo zilisomwa na Lyimo katika hafla hiyo.

"Mimi Dk Slaa nilialikwa kwa ubunge wangu na sio ukatibu mkuu wa Chadema na Mbowe alialikwa kwa jina lake na sio uenyekiti wa Chadema vivyo hivyo wabunge wengine. Sasa Chadema inapolaumiwa tunashindwa kuelewa," alisema na kuendelea

"Mimi namshauri Mariam akutane na wazee wamshauri kwanza badala ya kukurupuka na kutoa maneno ya kukipaka matope chama. Yeye anataka athaminiwe, atathaminiwaje kama yeye Mariam hataki kukithamini chama," alihoji

Kauli ya Dotto na Dk Slaa imekuja siku tatu baada ya mke wa tatu wa Marehemu Wangwe kuzungumzia utata wa kifo cha mumewe na kukitupia lawama Chadema kwamba kimeitelekeza familia baada ya kifo hicho.

Mariam alienda mbali zaidi na kumtaka spika wa Bunge Samwel Sitta kuchunguza kifo hicho akidai kuwa haridhiki na uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi.

Wangwe, mwanasiasa machachari aliyepata umaarufu kwa kuibua hoja tata bungeni, alifariki dunia katika ajali ya gari wakati akisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mazishi ya mfanyabiashara na mbunge wa kwanza wa jimbo la Tarime Bhoke Munamka.

Lakini mazingira ya kifo chake yalizua utata mwingi baada ya kuchukuliwa kama agenda ya uchaguzi mdogo katika kampeni zinazoendelea sasa jimboni humo kumpata mrithi wa kiti chake.

Tayari Jeshi la Polisi limemfungulia mashtaka Deus Mallya aliyekuwa akisafari na marehemu kwa tuhuma za kusababisha mauaji hayo.

Lakini mke huyo mdogo wa Wangwe anaona juhudi hizo za polisi ni ndogo na hivyo, serikali na Spika Sitta hawana budi kuongeza uzito wao.

“Sipendi mambo haya yaishe hivi hivi," alisema mama huyo. "Familia ya Wangwe haijaridhishwa na namna polisi wanavyofuatilia kifo cha Wangwe."

"Wasiwasi wangu ni uchunguzi unaofanywa na polisi kwani hawajawahi hata kufika kuniuliza kuhusu kifo cha Wangwe nikiwa kama mke wake.“Labda maelezo yangu yangewasaidia kwa kiasi fulani.

Akizungumzia hali ilivyokuwa katika kipindi cha kuelekea kifo cha mumewe, Mariam alisema mambo yalikuwa magumu sana nyumbani, hasa baada ya Wangwe kusimamishwa nafasi yake ya makamu mwenyekiti wa Chadema.

Pia Mke wa pili wa marehemu Chacha wangwe,Doto amesema

cha msingi ni viongozi kusaidi kulea watoto tisa aliowaacha marehemu ambao ni Zakayo na Rhobi (18) ambao ni mapacha, Bob (17), Pendo (16), Beatrice, (15) na Wangwe mwenye miaka 14 ambao ni watoto wa mke mkubwa nayeitwa Ghati.

Kwa yeye Doto ana watoto wawili, Mwajuma (11) na Ghati (6) wakati Mariam ana mtoto mmoja anaitwa King (1).

Source plz!

Kuna kumtambua mke kwa sura na kumtambua mtu kwa nyaraka. Jamani kwenye viongozi wa CHADEMA mtuambie, kwenye nyaraka alizoandisha Chacha Wangwe bungeni na makao makuu ya chama chake, aliandika wake watatu au aliwataja tu wale wake wawili wa kwanza na kumuacha Mariam Wangu?

Asha
 
Wakuu sorry,

Source Mwananchi
 
The most lame excuse one can ever give. Kama kweli Dr. Slaa aliamua kudharau hiyo 40 kwa vile hamjui huyo Mariam, vipi adharau hata uwepo wa Prof. Wangwe?

Hivi hili ni onyo, vitisho au ndio utaratibu kuwa msaada kwa wajane utategemea na jinsi watakavyojipendekeza kwa viongozi wa CHADEMA?

Dr. Slaa, nakushauri kama umekosea jambo usiliongelee maana unapofungua kinywa unazidisha kuboronga.

Kubwa Jinga Jinga umeanza tena!

Kwani nani alikwambia ni utaratibu kwa wajane kujitokeza hata miezi miwili haijapita kuanza kulia lia kuwa chama kimawatelekeza?

Ni utaratibu wa wajane kujitokeza kuanza kusema chama cha siasa kimeua mume halafu hapo hapo kukilalamikia chama hicho hicho kuwa hakilei watoto?

Halafu mbona huyu mke mwenza wetu hazungumzii kuhusu wake wenzake?

Jamani Mariam Wangu wasemee na wengine basi halafu badala ya kulilia mali tu lilia CHADEMA iwasomeshe watoto. Hasa mtoto wako wa mwaka mmoja, maana watoto wa wake wenzako wameshakuwa wakubwa kiasi

Asha
 
Mkuu,

Tafadhali onyesha nilikopotosha umma.otherwise wewe ndiye unaepotosha umma kwa kutaka kuwafanya waamini mimi ni mpotoshaji huku ukijua si kweli.Please buddy,come on and help me on this!

Anyway,niendelee na mjadala!

Btw: Hivi mkuu Kubwajinga,ulitegemea Dr.Slaa ake kimya eti kwa sababu mtu ni mjane yuko kwenye majonzi na anakichafua Chama? Huyo mwanamke angekua na majonzi ya kweli asingepata nguvu za kukubali kutumika kisiasa kukichafua chama.Ukitaka kuonewa huruma kwanza jihurumie,that's all!

Kweli wengi hamna nia njema na CHADEMA,yaani mkuu unataka Slaa akae kimya huku chama kikiburuzwa kwenye sewage? Wakuu mtasubiri sana,na CHADEMA walishaapa kupambana na wale wote wanaotumia kifo cha Wangwe kukipaka matope.

I am sory kama nimekukwaza, ila sijasema umepotosha nimesema unechelewesha mijadala muhimu. Thanks kwa kuendelea na mjadala vyema.
 
Dada hebu shika usukani,wacha nikale nondoz.Mkuu kuna watu hapa nia yao ni moja tu kuona CHADEMA ikichafuliwa mbele umma.By,the way latest news kutoka Tarime zinasemaje? Please mlioko huko tafadhali tuwekeeni picha za mikutano ya kampeni.

Mafisadi watakua wameshikwa pabaya sana,Revolution forever,kwa kutumia Nguvu ya Umma.
 
I am sory kama nimekukwaza, ila sijasema umepotosha nimesema unechelewesha mijadala muhimu. Thanks kwa kuendelea na mjadala vyema.

Mkuu,

Umesema kwenye post yako hapo juu.Hebu isome tena .Hata hivyo asante kwa uungwana.tukate ishuz mkuu.Heshima nawe!
 
Kubwa Jinga Jinga umeanza tena!

Kwani nani alikwambia ni utaratibu kwa wajane kujitokeza hata miezi miwili haijapita kuanza kulia lia kuwa chama kimawatelekeza?

Asha

Asha,
Kwani kuna muda gani uliowekwa kwa familia kujisikia kuwa wametelekezwa ndio walalamike? Mbona majibu ya chama yanafuatana na vitisho?
 
Dada hebu shika usukani,wacha nikale nondoz.Mkuu kuna watu hapa nia yao ni moja tu kuona CHADEMA ikichafuliwa mbele umma.By,the way latest news kutoka Tarime zinasemaje? Please mlioko huko tafadhali tuwekeeni picha za mikutano ya kampeni.

Mafisadi watakua wameshikwa pabaya sana,Revolution forever,kwa kutumia Nguvu ya Umma.

Latest!

Komba leo kafukuza wananchi kwenye mkutano wake. Alikuwa anaimba nyimbo za TOT wanawake wakaanza kupigiwa mayowe kama ya msiba. Akaacha kuimba akauliza wangapi watapigia kura CCM, halaiki ikanyoosha vidole viwili juu ile V-ishara ya vema na ushindi ya CHADEMA. Komba akachukia akasema sasa kama nyie ni CHADEMA mnakuja kufanya nini kwenye mkutano? Hebu ondokeni haraka sana tuacheni wenyewe

Asha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom