Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Yes, the problem is not English but is “what to explain to them once they will need him to comment how the campaign is going?
kwa mtindo ambao CCM wakishirikiana na Polisi wanavyofanya madudu kwa kweli hakuwa na la kusema
 

Eeeh lazima nikimbilie kiingereza manake ndicho cha kimataifa zaidi kuliko kiswahili.Labda nikuuulize;Wanapokutana watu wa mataifa mbalimbali ni ipi lugha itakayoweza kuwaunganisha katika mazungumzo yao kati ya kiswahili na kiingereza?
Halafu si mnasema kiingereza nacho ni lugha rasmi Tanzania,sasa kwanini utetee watu wasiojua kiingereza tena ni viongozi wakubwa?
Nimesimama kwenye umuhimu wa kujua lugha za kimataifa kwa watanzania hasa viongozi wake na si kwa Makamba tu.Makamba kama anakijua ni vizuri,ila kwawale wasiokijua waende english course mara moja!!
 
Itakuwa ni aibu tena ni kushangaza kama lugha ina play a role. Ujuzi, uongozi, na usomi hauendani moja kwa moja na mtu kufahamu kiingereza au lugha nyingine ya kigeni. Katika medani za kimataifa kama mtu hajui Kiingereza ndio maana kuna watu wanaitwa wakalimani.

Rais Muammar Ghaddafi alipozungumza na Bi. Rice hivi karibuni alikuwa anamtumia mkalimani. Sasa mtu mwingine anaweza kufikiri kuwa Kanali hajui kiingereza. Ahmeddinajad naye akizungumza na vyombo vya kigeni huwa anazungumza kwa lugha ya kikwao lakini haina maana hajui Kiingereza and so is Bashir wa Syria.

Kama Makamba hata kama anajua Kiingereza anayo haki ya kumtumia mkalimani kumtafsiria. Hata kama ningekuwa mimi Balozi anapokuja kunitembelea n.k ningezungumza Kiswahili tu as a matter of fact sina sababu ya kuzungumza kiingereza kwenye hadhara isipokuwa pale inapolazimu kabisa. Vinginevyo ni kiswahili tu mwendo mdundo.

Tunazo shule za Kiswahili Tanzania, mabalozi wanapokuwa wachukue kozi ya miezi michache au ya immersion ya Kiswahili na watashika mawili matatu.

Kama kuna sababu nyingine iwe, lakini hii ya kiswahili haiwezi na haipaswi kuwa sababu ya msingi hasa kutokana na nature ya uchaguzi wenyewe. Ungekuwa ni uchaguzi wa kitaifa labda lakini huu wa local hakuna sababu ya kutambiana kiingereza.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba CCm ina hali mbaya sana Tarime.wananchi wa tarime wanapaswa kuigwa na Watanzania wote wenye kupenda maendeleo ya nchi yao.Unajua ukilijua halikupi shida, ni nani anaweza kusimama Tanzania na kusema jimboni kwake watoto wa sekondari wanasoma bure kama sio Tarime? Kwani Mgodi uko tarime peke yake? Tunataka watu wenye vision na mission kama wana tarime na siyo siasa za maji taka,Tshirt na kofia.Kipi bora ELIMU au kofia na Tshirt ambazo zinapauka ndani ya wiki moja.Mpaka sasa wanafunzi wa Tarime waliosomeshwa na mgodi ni wengi sana tena mpaka level ya degree, niambie kahama au Geita kama kuna kitu kama hicho, kisa good boys, good men,good people.sifa hazisaidii wala kutujengeni sisi wabongo.Endeleeni kuitwa good boys, sisi huku tunakamua maelimu kutokana na mapato ya wawekezaji then in ten years to come tuone wajanja ni wapi?
 
Kwanza,Makamba kama kawaida yake na chama chake hajui hana uwezo wa kujibu kwa hoja

Pili,kama ilivyo kwa viongozi wengi vilaza wa CCM kiingereza ni ishu,hata hivyo ni bora kuthamini lugha yako ambayo ni kielelezo cha ukombozi wako kuliko lugha ya kigeni.

Hata hivyo Makamba na vilaza wenzie hawatakiwi kutumia hili kama kigezo mojawapo cha kutojua lugha,ni vilaza in nature
 
Yes, the problem is not English but is “what to explain to them once they will need him to comment how the campaign is going?
jamani siyo luhga yetu hii na wala mtu asijione fahali kuzungumza kwa ufasaha kama mzungu.ni lugha tu kama zingine.angalia jinsi ambavyo narais kama wa cubba,venezuela na dhdafi wanavyotumia lugha zao........kuna watu wana thamini english mpaka wanaona tahira la kiingereza linaloonea enlish vema ni lina akili kuliko darasa la saba wa tanzania alifauru lakini bado hajui english
 
Ni kweli kabisa mkuu,ila haya ni mapinduzi yasiyo na kikomo
 

Kwa hiyo unasema.......? Acha hizo unataka kumtetea makamba na ukilaza wake huyo siku zote atabakia kuwa kilaza tu.Silly secretary!
 
Tarime yatikisika

Mwandishi Wetu Oktoba 8, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiishutumu Polisi na vyama vya NCCR-Mageuzi na DP kufanya kazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Tarime, hali katika jimbo hilo imezidi kuzizima na joto la uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili.

Hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amewasili Tarime na ataanza kujibu mapigo akitumia helikopta maalumu ya kukodi ili kukamilisha kampeni kabla ya Jumapili.

Kwa muda mrefu sasa, Chadema imekuwa ikidai kwamba NCCR-Mageuzi wakiongozwa na Mwenyekiti wake, James Mbatia na DP chini ya Christopher Mtikila, wamekuwa wakitumiwa na CCM katika kuvihujumu vyama vya upinzani wakati wa uchaguzi, lakini sasa shutuma hizo zimezidi kukua na kuanikwa hadharani huku Polisi nayo ikiongezwa mkumboni.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumanne, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema ya kuwa kuna ushahidi wa wazi kwamba NCCR-Mageuzi na DP wamekuwa wakifanya kazi ya CCM na sasa wanasaidiwa na Polisi waliopelekwa kulinda usalama jimboni humo.

Akisaidiwa na kiongozi mwingine mwandamizi wa chama hicho, Chiku Abwao, Lissu alisema imethibitika kwamba NCCR-Mageuzi na DP wanatumika na CCM kuvuruga nguvu ya upinzani na vyama vinavyolengwa ni Chadema na CUF. Chiku Abwao amewahi kuwa kiongozi na Mbunge kupitia NCCR-Mageuzi na ametoa siri ya baadhi ya maamuzi ya kuua upinzani aliyopingana nayo kabla ya kukihama chama hicho.

Viongozi hao wa Chadema wamekumbushia jinsi NCCR-Mageuzi ilivyohujumu upinzani katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika kisiwani Pemba, ambako waliweka wagombea kinyume cha maamuzi ya vyama vingine vya upinzani wakati mara kadhaa Mtikila amekuwa akitoa kauli zenye kuvishutumu vyama vya CUF na Chadema.

Lissu alisema wakati mwaka huu, NCCR-Mageuzi na DP vimeweka kambi Tarime kuihujumu Chadema na kuisaidia CCM, mwaka 2005 vyama hivyo, alisema, vilifanya kampeni kuvuruga nguvu ya upinzani na Mtikila wa DP alimwekea pingamizi Mgombea Mwenza wa Chadema, kabla ya pingamizi lake kutupwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na baadaye Mahakama.

Kwa upande wa Polisi, Chadema wanadai kwamba badala ya kulinda amani na kuvitendea haki vyama vyote, jeshi hilo limekuwa likionekana kupokea amri na maelekezo kutoka kwa viongozi na mashabiki wa CCM bila kuzingatia sheria na taratibu za kazi zao.

"Chadema kinalaani vikali matukio ya hivi karibuni ya Polisi kutumia mabavu, vitisho na vitendo vya ukandamizaji ili kuwatisha wananchi wa Jimbo la Tarime kwa lengo la kuisaidia CCM kushinda Tarime. Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo wiki tatu zilizopita, mamia ya wananchi, hasa vijana, wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Tarime wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka mbalimbali ya kubambikiza," alisema Lissu.

Lissu amesema licha ya sheria kuruhusu Mahakama kutoa dhamana kwa wale wanaotuhumiwa kwa makosa hayo, karibu wananachi wote waliokamatwa wakati huu wa kampeni za uchaguzi wamenyimwa dhamana kwa kisingizio kwamba wanahatarisha usalama wakati huu wa kampeni za uchaguzi mdogo.

"Wakati wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakiwa wanakamatwa na kunyimwa haki yao ya kupata dhamana, wanachama wa CCM pamoja na makada wao wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote za kisheria licha ya kufanya vitendo vya uvunjaji sheria wazi wazi," alisema.

Alitoa mfano wagombea wa CCM pamoja na wanaowaunga mkono kutoa kauli za kuchochea vurugu na kauli za kijinai lakini wamekuwa wakiachwa bila kukamatwa wala kuchukuliwa hatua zozote.

"Wagombea wa CCM na wagombea pandikizi wa CCM kutoka vyama vya DP na NCCR-Mageuzi au wapambe wao wa karibu, wametoa tuhuma za uongo na uzushi hadharani kwamba Chadema ndicho kinachohusika na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, hakuna hata mmoja wao aliyekamatwa au hata kutakiwa kutoa maelezo Polisi pamoja na kwamba tuhuma hizo za uzushi na uongo ni kosa la jinai chini ya sheria za nchi yetu," alisema Lissu.

Alisema hata ilipotokea kupigwa mawe kwa gari la Chadema aina ya Fuso likiwa limeegeshwa usiku kupigwa mawe na wanachama wa CCM, wahusika wa CCM waliokamatwa na walinzi wa Chadema na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Wilaya waliachiliwa huru pamoja na kukiri kuwa walitumwa na kiongozi mmoja wa CCM kufanya uhalifu huo.

"Kiongozi wa CCM aliyetuhumiwa kuwatuma wahalifu hao naye hajakamatwa wala kuitwa kwa mahojiano na Jeshi la Polisi. Aidha wanachama wengine wawili wa CCM ambao walitajwa kuhusika na tukio hilo mpaka leo hawajakamatwa na kufikishwa Polisi huku Polisi wakisema kuwa wanawatafuta ilihali vijana hao wakionekana mitaani Tarime wakiendelea na kampeni za CCM," alisema.

Katika kuelezea matukio ya mabavu, Lissu amesema wagombea ubunge na udiwani wa Chadema Charles Mwera na John Heche Suguta, Mkurugenzi wa Vijana Makao Makuu John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dk. Ben Kapwani pamoja na viongozi wengine wa wilayani Tarime walikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kisingizio cha kufanya mkutano usiokuwa na kibali.

"Ikumbukwe kwamba Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 na Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge na wa Rais za mwaka 2005 hazizungumzii chochote juu ya vyama vya siasa kuomba vibali vya kufanya mikutano yao wakati wa kampeni za uchaguzi," alisema.

Alisema Chadema hakikuwa na wajibu wowote kisheria wa kuomba kibali cha mkutano wake wa kampeni kwa Jeshi la Polisi na hivyo, kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata wagombea na viongozi si halali na kinalenga kuibeba CCM katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwatisha wagombea, viongozi, wanachama na wapiga kura wanaokiunga mkono Chadema.

Viongozi wa Chadema walikamatwa juzi wakiwa wanatoka eneo la Buhemba ambako walikuwa wamemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara.

Msafara wa magari na watu waliokuwa wanawasindikiza wagombea kurudi mjini ulijikuta ukisimamishwa kwenye eneo la Gereza la Buhemba.

Baada ya kufikishwa Polisi viongozi hao wa Chadema walikataa kuandika maelezo yao pasipo kuwa na wakili wao ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee. Wakili huyo baadaye aliruhusiwa kuingia kituo cha Polisi kabla ya wao kuachiwa huku wafuasi wao wakiendelea kushikiliwa kitendo kilichopingwa na viongozi hao.
 

Wenzetu wanaojali lugha zao wanaweza kukushangaa kweli kama unakaa kwao zaidi ya miezi sita na unashindwa kuongea lugha yao na kukimbilia lugha za watu wengine.

Ndio maana hata mabalozi au wafanyabiashara/wafanyakazi wanalazimika kujifunza.

Ni muhimu kujifunza lugha zingine lakini kila lugha ina mahali pake. Sisi tuna lugha ambayo ndio kubwa Afrika, wakati rais wa Msumbiji anaongea Kiswahili kwenye mkutano wa AU, sisi tunataka Makamba aongee kiingereza na mabalozi walioko TZ?
 
Kampeni Tarime mwee! kunatetesi kwamba Mhe. Mbowe yupo na chopa yake na CCM wameingiza chopa mbili! duh. Mambo ya kampeni hayo, nguvu kubwaaaa!!
 
Aliyekuwa mgombea CCM Tarime ahamia Chadema
Makubo Haruni,Tarime
Daily News; Wednesday,October 08, 2008 @20:00

Aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tanga ambaye alishindwa katika kura za maoni za kuwania ubunge wa Tarime katika uchaguzi mdogo unaofanyika Jumapili, Mwita Mwikwabe, amehamia Chadema.

Mwikwabe, ambaye alishiriki katika kumnadi mgombea wa CCM, Ryoba Kangoye, jana alionekana akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea ubunge wa Chadema Charles Mwera na kwa siku nzima alikuwa katika helikopta iliyotumiwa na Mbowe kwa kampeni katika maeneo mbalimbali.

Mwikwabe ambaye kuhama kwake CCM kumezua gumzo hapa, alikuwa amevalia magwanda kama anayovaa Mbowe na hakutaka kuzungumza lolote kuhusu suala hilo. Wiki moja iliyopita Mwikwabe alizua mtafaruku baada ya kutoa mwito kwa wana-Tarime kumchagua Mbunge anayefaa.

Aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kutangaza kukataa kuhamishiwa Ofisi ya Mwenyekiti wa UVCCM, akisema kazi hiyo ya ukarani ni ya chini mno kulinganisha na elimu yake ya Chuo Kikuu.

Mapema jana asubuhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliwataka wakazi wa Tarime kuondoka kwenye vituo vya kura mara baada ya kutumia haki yao ya demokrasia na kurudi nyumbani wakisubiri kutangazwa kwa matokeo.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Lewis Makame aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi. Alisema kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kukaa ama kukusanyika katika vituo hivyo kwa lengo la kuepuka usumbufu ama fujo.

Kauli ya Jaji Makame imekuja siku moja baada ya Mbowe kuwaambia wakazi wa Tarime wakati akihutubia mkutano wa hadhara juzi kwamba siku hiyo inabidi baada ya kupiga kura waondoke hatua mita 100 ambako wanaweza kukusanyika kusubiri matokeo.

Kwa mujibu wa Jaji Makame kauli hiyo ni ya upotoshaji. Alisema kuwa sheria ya uchaguzi hairuhusu mpiga kura kubaki eneo la kituo.Aliahidi kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki na hautakuwa na mizengwe kwani kila chama kitakuwa na wasimamizi katika kila kituo.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tarime, Trasias Kagenzi, amewataka wakazi wana-Tarime kuacha kutumiwa na wanasiasa aliodai ni “wa kutoka Dar es Salaam” kwa kuwachonganisha kufanya fujo na kufikia hatua ya kumwaga damu huku wao wakipanda ndege na kurudi Dar es Salaam.

Wakati hayo yakielezwa, Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila amesema ni afadhali CCM itwae ubunge wa Tarime, kama sio chama chake, kuliko Chadema.

Amesema hayo kutokana na kusambazwa kwa waraka aliodai uliandaliwa na viongozi wawili wa Chadema kwamba ametubu kutokana na maneno aliyokuwa akisema kuwatuhumu viongozi wa chama hicho kuhusika na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.
 

Looh! utafikiri ka copy na ku paste maneno ya Mtanzania!
 


Hivi kweli helikopta inahitajika kweli kwenye uchaguzi wa jimbo dogo kama la Tarime? Nani analipia gharama zake? Hivi haya si ndiyo marehemu Wangwe aliyokuwa anayapinga??
 
Kujiunga na chama chochote kilichopo kwa mujibu wa sheria ni mojawapo ya haki za kila mwananchi. Hata hivyo Mwita kanikumbusha enzi za akina Steven Wasira, Njelu Kasaka, John John Guninita, Wilbroad Slaa na wengine wasiokuwa maarufu. Natumaini kijana anamulika vema aendako.
 
Looh! utafikiri ka copy na ku paste maneno ya Mtanzania!
Watu wa Tarime wamezoea kuchinjana na wala siyo sababu ya kuchonganishwa na wana siasa mimi nafikiri mpaka wetu ulitakiwa uwe mto Mara huko Tarime wana tabia ya Kenya ambako wamezoea kuchinjana
 
Hivi kweli helikopta inahitajika kweli kwenye uchaguzi wa jimbo dogo kama la Tarime? Nani analipia gharama zake? Hivi haya si ndiyo marehemu Wangwe aliyokuwa anayapinga??

CCM wamepeleka 2 huko Tarime.....hivi ndivyo sisi wananchi tunavyopinga....
 
huu ndio mwanzo wa mwisho wa hatma ya kisiasa ya mwita. Tamaa ya mali na uchu wa madaraka ndio vimemfanya ahamie chadema. hiyo ni njaa tuu ndio imemkimbiza. namfahamu alipokuwa kiongozi wa DARUSO. hakufanya lolote zaidi ya kujikomba komba kwa CCM. kwa CHADEMA, amepotea!.
 

Mkuu naona unafanya kazi ya Sheikh Yahya, utabiri...waachie wenye fani yao...nani kakwambia ni amepotea? nadhani ametumia haki yake ya kikatiba..
 
Watu wa Tarime wamezoea kuchinjana na wala siyo sababu ya kuchonganishwa na wana siasa mimi nafikiri mpaka wetu ulitakiwa uwe mto Mara huko Tarime wana tabia ya Kenya ambako wamezoea kuchinjana

Ipole,

Kwa vile Tarime wanatabia ya kuchinjana hawafai kuwa watanzania sio? kwanza hiyo tabia ya kuchinjana umeistablish vipi hadi kufikia hiyo conclusion? any scientific inquiry? vipi wa Bukoba nao mto kagera uwatenge tuwaweke nchi yingine siyo, au vipi walioko Kilimanjaro ambao wanaonekana kwa jamii kuwa ni watafutaji na wahangaikaji, tuwahamishe nchi nao?

Huwezi kusema Tarime wamezoe kuchinjana wakati sijswahi sikia mtu yeyote kachinjwa huko, kama unazungumzia waliochomana visu week hii, kwani sehemu zingine za tanzania hawachomani visu????
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…