Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.

Are you kidding me!? watarime wataunganishaje harakati za kudai fair shares kwa madini yaliyoko wilayani kwao na wananchi wa maeneo mengine ambao bado hawajaona hilo suala kama ni jambo la kupewa kipaumbele?? Kama nilivyosema hapo awali:"If you want to go fast, go alone, if you want to go far, go together.” Huwezi ukawajumuisha wananchi wa sehemu nyingine kwenye hii cause hali wananchi hao wenyewe bado hawajawa tayari ku-join hii battle. So, Tarime wako absolutely right kupigania haki zao kivyaovyao. And I suport them 110%. Ila, siku ambayo watu wa sehemu zingine watakapoamuka toka usingizi na kuamua ku-join hii battle iliyoanzishwa na watu wa Tarime, then hapo ndipo watu wa Tarime nao watakapokuwa tayari kushirikiana/unganisha nguvu na wananchi wa sehemu zingine. And I'll love to see that happening coz it'll be a sort of spiritual awakening kwa taifa la Tanzania. Otherwise, sioni umuhimu kwasasa kwa watu wa Tarime kuunganisha nguvu na mtu yeyote yule. Wakifanya hivyo, then wajue kuwa cause yao iko doomed kiaina.
 
Gustanza_The,

..nimerekebisha kule kwenye posting yangu. nilitaka kusema kwamba siungi mkono dhuluma zinazowakabili wana Tarime.

..nilivyoelekeza hapo mwanzo ni ushauri tu.
 
Gustanza_The,
Mkuu kila la kheri lakini mtakuja nikumbuka maneno yangu...
Bahari kuu ni chafu sana kwa mashua hiyo hamtafika mbali!
 
Gustanza_The,

..nimerekebisha kule kwenye posting yangu. nilitaka kusema kwamba siungi mkono dhuluma zinazowakabili wana Tarime.
..nilivyoelekeza hapo mwanzo ni ushauri tu.

That's very nice of you, Jokakuu! Now, kilichobakia ni wewe kupewa uraia wakudumu wa Tarime (he he he!!)
 

Heshima yako mkuu! Kukiri kwako kuwa hata ktk familia zetu mtu anyeomba agawiwe chake hana maana ya kujiengua kabisa toka kwenye familia, inaonyesha kuwa sasa umeanza kuelewa ni niini haswaTarime wanachokidai. Tarime haiombi kuuda serikali yake (I mean, kuwa na katiba yake, jeshi lake, supreme court yao, bendera yao, wimbo wao wa taifa etc...); bali Tarime inachoomba is something simple: ipewe some sort of absolute power ya kuendesha mambo kadha wa kadha ambayo serikali kuu imeshindwa kuyatekeleza for almost 40 sum years now. Mambo kama vile, mfumo wao wa elimu (mitaala inayolenga zaidi ktk creativity & innovation kando na mitaala iliyopo hivisasa inayokaririsha watoto na kuwafanya wasome ili kufualu mitihani baadala ya kuwaandaa ktk path ya creativity & innovation). Wanataka wapewe uhuru wa kutoa/endesha huduma za jamii kama vile maji, umeme, na huduma za posta (wanataka kuanzisha utaratibu wa zip code/barua kupelekwa moja kwa moja nyumbani kwa watu). And last but not least, supreme power ya kuhozi utajiri wa madini waliyobarikiwa kupewa.


Mkuu, are you really serious about this? Ni nani huyo atakayeiweka dhahabu ya Tarime kwenye kitabu cheusi? Ukisema serikali kuu, nitakwambia "wrong answer!" Ukisema nchi wahisani, nitakwambia yes, wanaweza kufanya hivyo, ila, Tarime sio kwamba inataka kufukuza wawekezaji.Tarime inachodai instead, is a fair share from its God-given natural resources, gold. Kama indiginous wa Bolivia walivofanya chini ya utawala wa Rais Evo Morales.

Nitakukumbusha kitu kimoja hapa: Sudan inalaumiwa sana na mataifa ya magharibi kuwa haijali human rights, kwamba inaendesha mauaji ya kimbari ktk jimbo la Darfur; lakini China imewekeza huko. So inabidi uelewe kuwa we're in the era of globalization ambapo mataifa makubwa yana-fight hard ku-secure scarcy resources zilizopo. Kwahiyo, matifa ya Magharibi yakisema dhahabu ya Taime ina kasoro, then watu wa Tarime wana option ya kwenda na wachina.
 

Wala sio suala la mifugo pekee. Kuna ARDHI, BIASHARA ( hasa ya BANGI ), KOO ipi ni SUPERIOR,...Halafu nimeuliza pia hapa:
KATIBA ya NCHI yetu inasemaje kuhusu madai kama haya? Unakumbuka pia kauli ya Mwalimu kuhusu dhambi mbaya ya UBAGUZI au kuigawa NCHI kwa VISINGIZIO vyovyote vile?
 
Gustanza_The,
Mkuu kila la kheri lakini mtakuja nikumbuka maneno yangu...
Bahari kuu ni chafu sana kwa mashua hiyo hamtafika mbali!

Sasa umeona kwanini Tarime wanadai "autunomous status?" Si umesikiliza madudu aliyoyatoa Rais wako Kikwete alipohutubia bunge leo?

Nimefurahishwa na Mwanakijiji leo, finally ameamua kuchukua my original postion ingawa sio necessarily kuunga mkono hili suala la Tarime kuwa autonomous district.

Nimemuandikia kumshukuru, na hapa chini ni quote yangu:

 
Gustanza_The,

Mkuu nitarudia kusema sijapinga mnachojaribu kutafuta isipokuwa kuna mapungufu na bahati mbaya hamkutumia hekima....

katika swala la familia mtu anapodai mirathi yake kwa sababu ni halali yake hutegemea zaidi jinsi watoto wengine watakavyo pendekeza....Ombi la mtu mmoja hata siku moja haliwezi kuzua maamuzi ya familia nzima kugawana mirathi...hapa ndipo wewe hukupatupia macho ktk maelezo yako. Sisi wote tunataka kufaidika na mirathi ya mzazi wetu lakini hatutaki kugawana Umaskini, isipokuwa kuwekesha kile kidogo tulichonacho kiweze kuzalisha zaidi..Pili umeshindwa kuelewa kwamba hiyo dhahabu iliyopo Tarime sio mali ya wakazi wa Tarime wala kabila la Wakurya kwa sababu nyingi sana ambazo hazina hata hesabu....
Kifupi maombi yako ni maombi ya mjukuu ama mke wa mrithishwa anayetaka kujikata hali yeye sio mrithi halisi..huwezi kabisa kuambia kwa nini Tarime inataka kujitenga kiuchumi ati kwa sababu ya dhahabu wakati kuna vitu vingi mnategemea wilaya na mikoa mingineyo!...hamjitoshelezi kwa lolote na kwa bahati mbaya sijawahi kusikia wilaya inayotaka kujitenga kiuchumi.

Tatizo la swala la Tarime ni kama nilivyosema.. Maskini siku akipata matako hulia mbwata - ndicho kinachowachochea! Nina hakika pamoja na madai yenu hamjakaa na kujiuliza zaidi hivi ni nani hasa mwenye urithi huo? kwa sababu hata Tarime kwenyewe kuna hao Wajomba na Mashangazi...
Je, yule mwenye ardhi yenye madini atagawana sawa na wakazi wote wa wilaya hiyo? What if huyo mwenye ardhi akisema hana sababu ya kugawana na watu wengine hali dhahabu hiyo ipo ktk shamba lake!... what next kwa sababu kama mnavyoona hamfaidiki na madini kuna kila sababu mwenye ardhi ataona hafaidiki na madini...yeye pia anaweza kutafuta Autonomy!
Kisha kuna wilaya nyinginezo ambazo ziko mkoa wa Mara, hawa watapewa kitu gani! What if kila wilaya ambayo mtapitisha dhahabu zenu kwenda nje wakiwalipisha kodi ya kutumia barabara zao, maji yao, na pengine hata Umeme toka Musoma uwe na gharama zaidi kwenu..haya jingine what if Lowassa kisha nunua ardhi hapo kwenu mtamfukuza au?..
Hii nikiwa na maana kuna Watu wa makabila mengineyo ambao wanaishi hapo Tarime hawa watakuwa ktk kundi gani maanake tayari umeisha waita wao wajinga hawataki kutetea mali zao.. nasema hivi kwa sababu hata wewe hapo ulipo uko nje ya Tarime umeweza kuitazama wilaya yako ukiwa nje na kuona maonevu ambayo yanahitaji mjitenge kiuchumi hivyo basi hata hao watu wa Makabila mengine ambao ni wajinga pamoja nakwamba wanaishi Tarime wameshindwa kuona maonezi ya rasilimali zao huko kwao walikotoka!...na unazidi knishangaza kumsifia mwanakijiji hali yu sio Mkurya lakini kaweza kuona Udhaifu wa kiongozi wetu...Na wala sio pekee hapa kjiweni wapo watu kibao wa makabila tofauti ambao wameyaona mnayoyadai... tatizo kubwa la maombi yako ni UKABILA!.. hata kama iwe fact, unapotumia kabila mkuu tayari unaathiri madai yako.. NI sawa na Waarabu wanapodai nchi zao kutumia dini hali sii Waarabu wote waislaam na kesi yao inapelekwa kwa watu ambao sii waislaam..
Sijui hawa waarabu wanategemea miujiza gani! maanake siji hao waarabu wasiokuwa waislaam watajisikia vipi hata kama haki hiyo wanaihitaji.

Mkuu ninaweza kujaza kurasa kwa mapungufu ya mpangilio mzima wa kutokana na hayo machache tu..Ushauri niliowapeni ni wa bure na kama nilivyosema hapo nyuma nawatakieni kila la kheri kwani huko muendako mkuu kwa mashua hiyo hamtafika!
 
Mkuu nitarudia kusema sijapinga mnachojaribu kutafuta isipokuwa kuna mapungufu na bahati mbaya hamkutumia hekima...

First of all, I'm so very glad kwamba hupingi madai ya watu wa Tarime kuwa na autonomous district yao.



Mkuu hivi kweli unajua unachokiongea hapa? Please allow me to explain two things here: One, kuna kitu kinaitwa "title claim." now, hiyo title claim basically inahoziwa na native locals ambao pia nao kwa kila maamuzi wanayofanya lazima yapitie kwenye serikali za kijiji za wilaya ya Tarime. And second, kabla ya serikali kuanza kuingilia kwa nguvu na ku-force mikataba mibaya ichukue nafasi yake, prominent locals walikuja na na superb proposals ambazo zingehakikisha kuwa kila mkazi wa Tarime ana benefit kwa namna moja ama nyingine kutokana na utajiri huo wa dhahabu [sina time ya kuelezea every detail hapa, ila point ni kwamba hiyo assertion yako hapo juu ni wrong].


Oh boy, hivi hujui kwamba huko Nyamongo, Tarime kuna uwanja wa ndege? Hivi hujui kuwa Tarime iko mpakani na Kenya? Kama ikifikia hiyo hatua unayodai eti watu wa mikoa mingine kukataa dhahabu ya Tarime isipitishwe kwenye barabara zao, kwanini watarime wasitumie mpaka wa Kenya kusafirisha hiyo dhahabu? Ama kwanini wasiboresha huo uwanja wa ndege walionao ili ndege zitue na kuondokea hukohuko Tarime? Please mkuu, unaniangusha hapa!!

Hii nikiwa na maana kuna Watu wa makabila mengineyo ambao wanaishi hapo Tarime hawa watakuwa ktk kundi gani maanake tayari umeisha waita wao wajinga hawataki kutetea mali zao...

No! I can't let you construed my words like that mkuu! [You're taking my words out of context!!] Sijasema wala kuwaita watu wa makabila mengine kuwa ni wajinga. Nilichosema ni kwamba, watu wa sehemu zingine bado wamelala usingizi, hawaelewi kile ambacho watu wa tarime wanachokipitia [dhuluma wanayopitia]. Ndio maana nikasema kuwa huwezi kuwashirikisha watu wa sehemu zingine kama vile mlandizi, monduli ama chalinze kwenye hii cause ya watu wa Tarime kwasababu hawajui real situation ya huko Tarime, and therefore ita-make harder kwa wao kuwa enthustiatic na hiyo idea ya "autonomous status." So let make that clear: sijawaita watu wa makabila mengine wajinga.


I'm not sure if it's inferiority complex or what, but I think you're just trying to insinuate some sort of feud [either intetionally or on purpose] kati ya wakurya na makabila mengine ambayo mimi sikui-introduce kabisa kwenye original thread niliyo post. Mama yangu kwanza sio mkurya, kwa taarifa yako. Na sina ukabila ndani yangu hata chembe. Hapa nilipo naishi nchi ya watu [millions of mile from Tz] ambayo wengi wa watu ninao hang/fanyakazi nao sifanani nao hata chembe! So kitu cha mwisho kinachoweza kikaingia moyoni mwangu ni ukabila. I hate ukabila. And I have always hated ukabila. As a matter of fact, i don't even like anyone who talks about ukabila, kama unavyojaribu kufanya hapa. Ila tu ni kwa vile ninakuheshimu mkuu, Mkandara.
 
Nadhani uongozi wa chadema utawawia vigumu sana kutia mguu kule sasa sijui watamtuma nani katika imani hizi upotoshaji wa kifo cha Chacha
 
Last week, CUF na CHADEMA waliweza kuungana na kuweza kumpitisha Mwenyekiti wa Halmashauri kutoka upinzani. Hii ni licha ya Mhe. Msekwa kupiga kambi Tarime. Hii inaonesha nguvu ya upinzani ilivyo Tarime.

Uwezekano mkubwa ni kwa CUF na CHADEMA kuweka mgombea mmoja. Vyama vya NCCR na TLP havina mtaji mkubwa huko. CUF washaliona hilo.
 

I don't think this guy is MKABILA, his request for autonomous status for Tarime is solely based on his ideas of empowerment of the local government, In order to excute the development project in mostly effective way. Na hii imetokana na ukiritimba wa hali ya juu from central government, He believe that people of central governement who lives in Dar -es-salaam they out of touch with regular Tanzanian who wake up in the morning and not sure if they will put food on the table.
I'm saying this because I know Gustanza, he does not judge people based on the color of their skin, belief, or cultural inheritance. This guy is not MKABILA he deeply love all people.
 
Ni aibu kwa mtanzania kuwa na mawazo mabovu kama hayo.Kwanza ni uaini wenyewe hawajaacha kupigana mpaka sasa
 
Nguvu ya upinzani siyo ya chadema kwa kuwa mpaka sasa vyama vingine vya upinzani v.binaonyesha wazi kutokipenda chama cha chadema.ndio maana walikishambulia sana alipokufa chacha kwa imani potofu
 
Gustanza_The,

Heshima mbele, mkuu unataka hata kunifundisha kiswahili mkuu?..
Kiswahili safi tunaposema watu wa sehemu fulani wamelala haina maana wamelala usingizi isipokuwa wamelala kiakili..They can see but their minds are shut!.. ndio Ujinga huo kuu.
Haiwezekani kuwa unaposema watu wamelala hauna maana ya Ujinga kwani kulala kiakili ni Ujinga na ndio maana wazungu wanachukua mali zao bila wao kufahamu..Na kwabahati mbaya Barricks wamechukua mali kibao sasa ndio mnaamka.. Yaani ujinga umewatoka..kwa hiyo binafsi siku zote mtu yeyote anayetumia maneno ya WALE -THEM (generalise) mara zote huwa anajitenga na kundi hilo na kama anazungumzia kabila bila shaka anajiona yeye mbora kuliko kabila lile. Hiyo ndio maana yangu....na sina maana najaribu kuvunja heshima isipokuwa haya ni maneno yako mwenyewe yawezekana hukukusudia kusema hivyo.

Kuhusu Tarime mkuu wangu wala usinambie kitu nimekuwa sehemu hizo toka mdogo nikienda Ikizu kwa jamaa zangu. hata mwaka jana nilikuwepo na kama unakumbuka nilitoa hoja moja kuhusiana na Miwa. Kwa nini Ukivuka mpaka tu kuingia kenya utaona mashamba makubwa ya miwa hali upande wa Tanzania hakuna kitu kabisa yaani pori...Na nikatoa pendekezo linalohusiana na sehemu hiyo... Kwa hiyo naposema zipingi hoja yenu nina maana kwamba Watanzania wote tumehsa amka hatujalala tena na vizuri sana issue hii imepata watu wanaoweza kuisimamia ikiwa wabunge wetu wameshindwa. Ni harakati ambazo zimeanzishwa na Mkurya ma wakurya lakini ziwe na mtazamo zaidi ya mipaka ya Tarime kama Kenyatta na Wakikuyu walivyopigania haki za Wakenya..Ilianzia wapi na kwa maslahi ya nani isiwe sababu ya kuzuia harakati hizi. hadi sasa hivi mnaachamwanya mkubwa sana wa CCM kujibu mapigo yetu tena kwa viabaya sana kuliko hata madai ya Zanzibar ambo inajulikana hapo awali ilikuwa nchi yenye mamlaka yake...
Kuhusiana na uwanja wa ndege unataka kunambia hao wachimbaji wadogo ndio watakuwa na ndege zao zikiruka kwenda nje kuuza hizo dhahabu au?..Hivi kweli unaelewa ukubwa wa investment ya dhahabu na vitu vinavyohusiana na uchimbaji..
Nakuomba sana jaribu kutazama hoja zangu kwa makini zaidi badala ya kufikiria kwamba napinga kile mnachosimamisha na maelezo yako unaposema umefurahi kuona kwamba nakubaliana na hoja ya Tarime kujitenga kiuchumi inaonyesha wazi hujanielewa hata kidogo..Mapambano yanatakiwa yawe kikatiba na sheria inapotoka itazame nchi nzima sio kipande cha nchi ambacho hadi sasa hivi hakina makubaliano na wawakilishi wa mkoa mzima wa Mara acha mbali serikali ya Bara na ya Muungano. Kujitenga kwa Tarime kiuchumi ni issue ambayo haiwezekani kabisa...na mtakuja nambia ila kama mtaweza kurekebisha madai haya issue hii inaweza kuzaa uzito mkubwa sana kitaifa.
 
Unajua kuna wakati hujutia kuwa nchi hizi wakati kama huu maanake Chadema wanahitaji msaada mkubwa sana iwe ktk vyombo vya habari ama kuwafikia wananchi na kuwaeleza ukweli...Yaani basi tu sina hila maanake ndio nimesha kaa kw kinyozi wa maisha.

Lakini pomoja na yote haya nitawaomba viongozi wa Chadema na CUF kitu kimoja muhimu sana pamoja na kwamba niko mbali...
Kwanza mwenyekiti wa Chadema, Mbowe arejee Tarime haraka iwezekanavyo na kufanya mkutano wa nguvu na wananchi wa huko..kama kuna Utata unaohusiana na Mbowe mwenyewe basi achaguliwe mtu mwingine na hatma ya Mbowe iwe ndio imefika kwa sababu ameshindwa kuisafisha mbele ya Umma.

Pili, wapo washikaji kibao toka koo hii ya Chacha au Mwita ambao ni maarufu zaidi ya viongozi hawa waliochaguliwa na CCM au NCCR Mageuzi na wanaweza kabisa kushinda ikiwa Chadema wataweza kurudisha heshima ya chama hicho huko Tarime. Wapo vijana Uingereza na Marekani ambao wanaheshimika sana tarime na Chadema inaweza kabisa kuwatumia hawa vijana kurudisha kiti hiki cha Tarime...Ni swala la mawasiliano tu kati ya viongozi na vijana wengi hapa JF hili swala linaweza kabisa kuwa na mwanzo mpya yaani Chadema kuwafikia wana JF inapobidi kupata ushauri wa bure..
Nina hakika kabisa kuwa wananchi wengi wamechoka na mbinu za CCM na kwa yeyote yule atakayepigania CCM tarime ni lazima anapingana na matakwa ya wananchi wengi wa Tarime.. Jina pekee haliwezi kumpitisha Prof. Wangwe kwa sababu mfumo wa kujilimbikiza mali na kudhulumu rasilimali za wana Tarime bado ni ilani endelevu ya CCM ktk uwekeshaji...
Chadema wakishindwa uchaguzi wa tarime this time basi ndio imetoka na hakika nitalaumu Uongozi ulipo madarakani kwa kuzembea...
 
Mkandara,

..kuhusu suala la viwanja vya ndege Tarime..

..masuala ya anga serikali ina mamlaka fulani ktk hilo.
 
Lasthope,
Nikutoe tu wasiwasi kuhusu leakage ya information. Kama tulipata nyaraka nyeti za Serikali kuhusu BOT, kama tunapata Nyaraka nyeti za CCM za kila kikao nyeti, mathalan kikao cha NEC Butiama, cha ajabu nini CCM kupata taarifa za CCM. Inaonyesha tu jinsi ngoma ilivyo draw! Hamhitaji kupata taabu na mambo hayo katika age ya IT kama ilivyo leo! Vinginevyo nini faidi ya utandawazi! Mengine kwa sasa nayahifadhi, unless kuna mtandao unaoweza ku- draw information kutoka kwenye moyo na ubongo wa Binadamu! Kimsingi niwaeleze wapenzi wetu kuwa Chadema inapenda kwenda na Katiba na Kanuni yake, na mchakato wote utakuwa wazi wala msiwe na hofu.Na mchakato wowote wa uchaguzi lazima uanzie au uwe na Baraka ya Tarime, no imposition.
 


Mkuu Salaa
Asante kwa kutuondoa wasi wasi sis wana mapinduzi na watanzania haswa.
Kule juu kuna ushauri toka kwa Mkuu Mkandara .Jambo muhimu sana kwa sasa ni Chadema kuwa wazi juu ya maneno yahusuyo kifo cha Mkuu Wangwe .Kama ambavyo huwa tunataka CCM waje hapa waseme basi naungana na Mkandara kusema Chadema waende Tarime na si maelezo .Yale ambayo yangaliweza kusemwa kule maelezo yaelezwe pale Tarime na hapo kila kitu kitakuwa wazi .

Tunataka kuona Chadema inawakomboa Watanzania na hivyo transparency is vital kabisa .It is about time Chama kiende Tarime na kieleze msimamo na uhakika wa Chadema na tukio zima .

Sina wasi was kabisa na Chadema nina waamini sana lakini pia niwe wazi kwamba kwa mambo kama haya yakiachwa mwishoni Chadema watashindwa kuyasema .Msingoje sana muda uende .Kuna umuhimu sasa wa kurudi Tarime na ku clear the sky .
 
..kuhusu suala la viwanja vya ndege Tarime..

..masuala ya anga serikali ina mamlaka fulani ktk hilo.

What you [JokaKuu] fail to grasp here ni kwamba, endapo kama madai ya Tarime yatakubaliwa, then hiyo airspace itakuwa chini ya Tarime, brother! I kindly suggest kwamba: rudi tena kasome encyclopedia yako upya juu ya nini maana ya neno "autonomous."
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…