Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
msekwa always a loser! short on vision and long on poor judgement!

Kaiyurankuba,
Siku zote twamjua hivo, ila kwa mshangao wake wa matumizi makubwa ya chama anacho kiongoza yeye ama yanamdhihirisha jinsi alivo, ama yanatuhabarisha kwamba chama kinaenda ndivyo sivyo, yaani hakuna mawasiliano kati ya viongozi wakuu hata kwa matumizi makubwa ya mabilioni is just one man show!
 

wanawanyima wananchi haki ka kwa na muwakilishi wa kuwawakilisha mawazo na mattz yao bungeni kwa miaka mi3, hivi hawa kwa nini wasichukiwe na wananchi, wanafikiria mwisho wa pua zao tuu, CCM wajinga kweli yani
 
Khaaa

Mwe, ndio tusema'ge wamewakumbukia'ga wake sao? au ndo tusemage wamesoka kasi?

after all kauli yao inaonyesha kuwa wanachama wa chadema wanapenda ugomvi kitu ambacho sio kweli kwa asili. wameonyesha ugomvi baada ya kuona kulikuwa na dalili za kuingizwa King na CCM hivi hivi, si unajua hiki chama cha mafisadi siku hizi hakiaminiki?
 

Kweli kabisa Philemon,

Ninaamini kama Kikwete angekuja Tarime labda hali ingekuwa tofauti kidogo. Watu wamechoka, watu Tanzania wamechoka, wamedhoofu, wana njaa na shida nyingi sana. Wengi wa wananchi wa Tarime sio kwamba wanataka pesa toka kwa serikali yao, wanachotaka ni kusikilizwa, kuheshimiwa, kupewa hali mbadala baada ya dhahabu ambayo wamekuwa wanachimba kwa miaka yote hii kuchukuliwa na wazungu kimizengwe.

Kikwete angekuja akawaeleza wananchi anachofanya au anachotaka kufanya kwa kizazi chao na vizazi vijavyo. CCM inabidi irudi kule ilikokuwa zamani sana kabla ya Nyerere kung'atuka- chama kinachojaribu (au kuonekana) kuwajali wakulima na wafanyakazi wa Tanzania. Haya mengine ya kuleta matajiri wa Mwanza, Musoma na watendaji wa ccm kwenye mashangingi zaidi ya arobaini ni mchezo uliopitwa na wakati kwenye siasa za Tarime.
 
kwa maisha mabovu kihivyo ulitegemea wafurahi kubakia TARIME KAZI NA DAWA BWANA!
 
Ikifikia polisi wa Tanzania wanatumia magari kama ambayo yalikuwa yanatumiwa na polisi wa makaburu kule Afrika kusini wakati wa Apartheid basi ujue nchi inaelekea kubaya sana.
Yaliyofanywa (na yaliyotaka kufanywa) na polisi Tarime ni aibu kwa serikali na inabidi sasa wakuu wa polisi na majeshi wakae chini na kujiuliza kama wao ni watanzania kama sisi au wao ni wafanyakazi wa wakoloni.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…