Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
- Thread starter
- #21
Mods hongereni kwa kuweka heading sawa.Nashukuru sana kwa umakini wenu.Keep up the same spirit!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa habari zilizonifikia ni kwamba last week viongozi wakuu wa CHADEMA walimfata kijana mmoja aliyekuwa machachari kwenye siasa za vyuo vikuu nchini ambae hafungamani na upande wowote kisiasa za vyama wakijaribu kumshawishi akagombee Tarime maana wanaona anauzika na the fact kwamba ni mtu wa huko wakadhani anaweza kuwatoa kimasomaso, baada ya kuongea naye sijui walichokubaliana kimsingi japo walisema pia ikiwa yeye hataki awaonyeshe mtu anayedhani anaweza kuuzika wa huko, ila cha ajabu ni kwamba baada ya muda Mzee Kingunge akampigia simu huyio kijana akimwambia "nasikia umefatwa kushawishiwa kijana mbona hatuambiani?" Sasa kitu cha kushangaza ni kwamba nani alimwambia Kingunge hiyo ishu au humohumo ndani ya chadema ndo wamo informers wa ccm? je namna hii kweli chadema watatoboa kama kila wanachofanya ccm wanakijua within minutes? Je ni kweli hawana mtu tarime wa kugombea au wanatishwa na propaganda za ccm? Si wanifate mimi nikagombee, kwi, kwi,kwi.........
Huu nao ni udaku. Hebu tuambie ni kiongozi gani wa CHADEMA huyo! Kule CHADEMA ni chama tawala, kina watu mashuhuri kama yule Mwenyekiti wa Halmashauri Bwana Mwera halafu kuna yule bwana Sasi ambaye gazeti la Mwananchi lilimuandika kwa kirefu kuwa CCM ilimuandamana zaidi hata ya Chacha. Na yuko kule Tarime, kwa nini asigombee? mi naamini wako wengi tu. Labda bado wako kwenye maombolezo ndio maana hawasemi chochote kuhusu mgombea sasa hivi. Kwani tume imeshatangaza uchaguzi tayari jamani? Marehemu hata siku arobaini hajakaa!
Asha
Chadema yapata pigo John Nditi, Morogoro
Daily News; Monday,August 11, 2008 @08:36
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Morogoro kimepata pigo baada ya viongozi wake wawili wakuu kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi hao ni Katibu wa Wilaya ya Ulanga wa chama hicho, Said Kaole na Katibu Msaidizi wake Hassan Mohamed.
Viongozi hao walikuwa ni miongoni mwa wanachama 40 kutoka vyama vya upinzani walioamua kuvihama vyama vyao na kujiunga na CCM mwishoni mwa wiki.
Wanachama hao wapya walikabidhiwa kadi za CCM na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba wakati wa ziara yake ya siku saba mkoani Morogoro.
Mbali na idadi hiyo ya wanachama wa upinzani kurejea CCM, watu 396 walijiunga na chama hicho na kupewa kadi za uanachama pamoja na kufunguliwa kwa mashina 17 ya CCM na Katibu Mkuu huyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanachama waliorejea kutoka kambi ya upinzani walidai kuwa wameamua kujiunga na CCM kufuatia utekelezaji mzuri wa Ilani yake juu ya kuwapatia wananchi maendeleo ya kweli, ikiwamo ujenzi wa shule za sekondari, zahanati na maji safi tofauti na ilivyo kwa vyama hivyo wa upinzani.
Makamba aliwataka viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya shina, tawi, wilaya na mikoa kuanza kwenda kwa wanachama kuimarisha uhai kwa ajili ya kukipatia ushindi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka ujao na uchaguzi mkuu wa 2010.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, CCM imeamua kuanza mikakati yake ya ushindi kwa uchaguzi huo ili kuweka mazingira ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.
"Viongozi wa CCM wa ngazi zote sasa hakuna kulala …ni wakati wa kwenda kwa wananchi na wanaCCM kushughulikia matatizo yao na kuyazungumzia yale tuliyotekeleza," alisema Makamba.
HabariLeo
Jinsi Siasa za Tanzania Zilivyo...Itakuwa Maajabu Lile Jimbo Likichukuliwa Tena Na Chadema.
Uchaguzi utafanyika kati ya mwezi march na april 2010. Hekaheka za uchaguzi huambatana na matumizi makubwa ya fedha (chakula, malazi, spika, magari, diesel na posho za wapiga debe/wapambe), marehemu alifadhiliwa na G9 baada ya NEC kumpitisha kwa nguvu Kisyeri Chambiri ambaye hakutakiwa. Kumbuka Kisyeri Chambiri alishindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM.
Kwa sasa G9 hawana sababu tena ya kufadhili chadema kwani shida yao ilikuwa kumwondoa chambiri kwa vyovyote vile.
Chadema haina hulka ya kufadhidi kampeni za wagombea ubunge wake labda ianze sasa! Uchaguzi huu utakuwa na vurugu nyingi na matumizi makubwa ya nguvu na fedha hivyo baada ya matokeo wananchi wakawaida watakuwa wamechoshwa na siasa.
Then, octoba 2010 kutakuwa na uchaguzi tena wa madiwani wabunge na rais, kampeni zitaanza upya tena, nguvu yote ya chadema itahamia kwenye urais na akina slaa/zitto watakuwa majimboni kwao wakihangaika, hapo ndio itakuwa mwisho wa chadema tarime, hawatapata hata udiwani.
Kwa habari zilizonifikia ni kwamba last week viongozi wakuu wa CHADEMA walimfata kijana mmoja aliyekuwa machachari kwenye siasa za vyuo vikuu nchini ambae hafungamani na upande wowote kisiasa za vyama wakijaribu kumshawishi akagombee Tarime maana wanaona anauzika na the fact kwamba ni mtu wa huko wakadhani anaweza kuwatoa kimasomaso, baada ya kuongea naye sijui walichokubaliana kimsingi japo walisema pia ikiwa yeye hataki awaonyeshe mtu anayedhani anaweza kuuzika wa huko, ila cha ajabu ni kwamba baada ya muda Mzee Kingunge akampigia simu huyio kijana akimwambia "nasikia umefatwa kushawishiwa kijana mbona hatuambiani?" Sasa kitu cha kushangaza ni kwamba nani alimwambia Kingunge hiyo ishu au humohumo ndani ya chadema ndo wamo informers wa ccm? je namna hii kweli chadema watatoboa kama kila wanachofanya ccm wanakijua within minutes? Je ni kweli hawana mtu tarime wa kugombea au wanatishwa na propaganda za ccm? Si wanifate mimi nikagombee, kwi, kwi,kwi.........
Jinsi Siasa za Tanzania Zilivyo...Itakuwa Maajabu Lile Jimbo Likichukuliwa Tena Na Chadema.
DUh hii kali,,, yaani mtu anafuatwa kuombwa, anakujulisha, baadaye anapigiwa simu na Kingunge anakujulisha na wewe unaweka mambo hadharani JF...
Kwa tafsiri yangu, kama hii habari ni ya kweli, basi wewe ndiye kijana mwenyewe, kama si kijana mwenyewe, huyo kijana hafai hata kuongoza mtaa maana hana 'kifua' na katika siasa kunahitajika 'kifua'.
Does that mean jimbo halitakuwa na mwakilishi hadi 2010? Thats very long, why?