Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
CCM will do anything to make sure they grasp the power they need manipulating everything at their disposal for their own good!
Shame on them!
 
Kwa hali inavyoendelea inaonekana hata Mugabe alikuwa mstaarabu kidogo kwake huko wala sio CCM tena! Hii ya kupata ushindi at any cost ni sera ya kimabavu hata wakolono hawakuwa hivyo, itafika wakati wananchi watasema heri wakati wa ukoloni!

Wananchi wameshakata tamaa zamani sana na serikali iliyopo madarakani. Na ni muda mrefu tu wananchi walishasema heri mkoloni kuliko wasanii.
 
Mgombea Ubunge, Mnyika, mgombea udiwani na Dk Kapwani (kiongozi wa Chadema mkoani Iringa ambaye alishirikiana na Prof Sarungi kuhudumia majeruhi wa ajali) waliachiwa na polisi lakini mgombea ubunge kagoma hadi wote waliokamatwa watolewe na sasa karudi ndani ili wale vijana nao waandike maelezo watolewe.

Inaelezwa ni mkakati maalumu wa kuhujumu safari ya Mbowe, Zitto na Lissu ambao wanaelekea Tarime kesho.
 
Dawa yao ni hapo CCM itakapopigwa chini ndio kitakapoeleweka hapo!
 
Mh usitake kunambia tanzania na sisi tunaelekea kwenye ule uonevu wa wazi wazi wa R.Mugabe na Mwaikibaki, kama kwei basi ni balaa

Si tu tunaelekea huko bali tumeshawasili na kuna ushahidi wa kutosha. Na hakuna wa kulaumiwa ila ni viongozi wa CCM.
 
Dawa yao ni hapo CCM itakapopigwa chini ndio kitakapoeleweka hapo!

ushindi wa asilimia kati ya 60 -65 kwenda upinzani endapo uchaguzi utafanyika Jumapili kama ilivyopangwa. Endapo utaahirishwa kutokana na vurugu zinazotarajia kutokea, basi CCM itaweza kushinda kwa alimia chache sana uchaguzi utakapofanyika.
 
Habari kutoka Tarime zinasema kuwa mgombea huyo pamoja na yule wa Udiwani walikuwa wanatoka eneo la Buhemba ambapo walikuwa wamemaliza tu kuhutubia mkutano wa hadhara. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka Tarime, msafara wa magari na mamia ya watu waliokuwa wanawasindikiza wagombea kurudi mjini ulijikuta ukisimamishwa kwenye eneo la Gereza la Buhemba.

Aliyeongoza kusimamisha msafara huo ni Kamanda wa FFU mkoa wa Mara Bw. Lyanga ambaye ndiye inadaiwa aliamuru vikosi vyake kuvunja msafara huo na kuwakamata viongozi wa Chadema.

Baada ya kufikishwa Polisi viongozi hao wa Chadema walikataa kuandika maelezo yao pasipo kuwa na Wakili wao. Baada ya vuta nikuvute Wakili wa wananchi hao ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Halima Mdee aliruhusiwa kuingia kituo cha Polisi. Jeshi la Polisi lilikuwa tayari kumuachilia mgombea Bw. Mwera lakini na yeye amekataa kuondoka bila ya kuondoka na wenzake ambao walishikwa pamoja.

Katika vurumai lililotokea kuna watu ambao wamejeruhiwa katika harakati za kuwakimbia Polisi na dereva wa Mgombea Ubunge ameumia vibaya na wakati huo anafanyiwa mipango ya kupelekwa hospitali.

Kumekuwepo na tetesi kwa karibu wiki sasa za mipango ya kuchafua uchaguzi huu ili hatimaye uahirishwe. Kutokana na uwezekano huo viongozi wengine wa Chadema walioko Tarime wamekuwa wakitumia kila ushawishi kuwazuia wananchi kutokwenda kuvamia kituo cha Polisi na kuwatoa viongozi. "Hicho ndicho wanachotoka CCM" alisema mmoja wa viongozi hao ambaye alikataa kutaja jina lake kwani siyo msemaji rasmi wa Chadema.

KLHN itaendelea kukuletea habari mpya.
 
Jamani huu uonevu hadi lini!jamani Serikali ya CCM mkubali kushindwa msitumie nguvu ya dola kutafuta ushindi wa lazima!Tarime hamuiwezi!
 
Jeshi la polisi liko chini ya serikali inayoongozwa na chama gani?

-CHADEMA?
UDP?
CUF?

kuwa chini ya serikali inayoongozwa na CCM haina maana ni tawi la CCM. Polisi siyo jumuiya ya Chama. Keshokutwa upinzani wakichukua madaraka, polisi wataendelea kuwepo na kufanya kazi zao kwa kuongozwa na sheria zao siyo itikadi au manifesto ya chama fulani.

Wabebeshe mzigo polisi wao wenyewe usiwasingizie CCM. Kama Polisi ni wabovu ni wabovu kutokana na upolisi wao; kama wako influenced na CCM tatizo siyo CCM bali Polisi.
 
Wewe wasema!
 
•Mbatia: Upinzani ushindane kwa hoja

Na Richard Mwaikenda, Tarime

MWENYEKITI wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia amesema upinzani wa kisiasa Tanzania usiwe wa kupigana bali uwe wa kushindana kwa hoja.

Bw. Mbatia alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kampeni za chama hicho jana, kwenye stendi kuu ya mabasi mjini Tarime, mkoani Mara.

Alitoa kauli hiyo akilinganisha matukio ya watu kupigwa mawe, mbwa kuvalishwa sare ya CCM, ambayo yamekuwa yakitokea na kudaiwa kufanywa ana vijana kwenye kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea.

Bw. Mbatia, alikemea kitendo cha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa. Kuwatumia vijana wa vijiweni kuwarubuni kwa 'vijisenti' wafanye vurugu, badala ya kuwapa elimu ya uraia ili wajue haki zao.

Alisema, baada ya kuona vijana wapo vijiweni kutokana na kukosa kazi, wanasiasa hao wameamua kuwatumia kufanya maovu badala ya kuwaelimisha namna ya kujikwamua katika maisha yao.

Alisema, matukio ya fujo yanayotokea Tarime si aibu tu bali ni laana kwa Tanzania ulimwenguni kote kwa kuwa kila yanapotokea husambaa duniani kote.

Bw. Mbatia alisema, upinzani Tanzania haupaswi kuwa uadui wa kutukanana, kubebeana mapanga na kubebeana mawe bali kushindana kwa hoja.

Alisema, kwa vitendo vya fujo, vinavyotokea Tarime, vinaonesha jinsi ambavyo viongozi wa siasa hawajaelekeza somo la uraia la kila mwananchi kujua haki yake.

Bw. Mbatia alitumia fursa hiyo kuwanadi wagombea wa chama hicho,
Bw. Enock Haroun anayewanaia Ubunge na Bw.Gidion Wangwe anayewania Udiwani Kata ya Tarime mjini.
 
Habari kutoka tarime zinasema mji mzima ulikuwa mshikemshike huku mabomu ya machozi yakinyesha kama mvua. Polisi wametumia pia risasi za moto. Vijana wawili wemejeruhiwa, mmoja amevunjika mkono na mmoja amevunjika mgu. Bado haijajulikana kama wameumia kutokana na kupigwa risasi au ni kutokana na kimbiakimbia kuepuka vurugu.
 
Hali ya kisiasa na kampeni za ubunge na udiwani katika jimbo la Tarime inaendelea kubadilika kila muda unavyopita.

Taarifa za kukamatwa kwa Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA,Mkurugenzi wa Vijana John Mnyika na wanachama na wapenzi wa CHADEMA zimeleta sura mpya katika siasa zinazoendelea Tarime.
Taarifa zimeripotiwa kuwa waliokamatwa walitoa maneno ya uchochezi katika kampeni za jana za kumnadi mgombea udiwani kata ya Tarime mjini.

Kuna kila sababu ya kuiita hatua hii kuwa ya makusudi kabisa na ambayo inalenga kudidimiza siasa na ushindi wa upande mmoja kwa maslahi ya upande mwingine.Haiwezi kukubalika kuwa eti katika kampeni zinazoendelea jana ndiyo kwa mara ya kwanza kauli za uchochezi zimetolewa katika kampeni za Tarime.

Tangu kuanza kwa kampeni tumeshuhudia na kutaarifiwa namna CCM wanavyotumia jukwa la kisiasa kuvipaka vyama vya upinzani matope na hata Makamu mwenyekiti wake, Pius Msekwa kufikia hatua ya kusema kuwa CCM haioni tatizo jukwa lake kutumiwa na wanafamilia ya Marehemu Chacha Wangwe kuzungumzia kifo cha ndugu yao.Kama hiyo haitoshi, Mchungaji Mtikila alitumia jukwa la kisiasa kuwaita viongozi wa CCM wauaji na alikwenda mbali zaidi kwa kusambaza waraka unaochochea kwa kiasi kikubwa uhasama kwa wanajamii wa Tarime na kuendeleza chuki dhidi ya CHADEMA.

Huu ni mfano wa matukio ya kuvunja amani na kuchochea vurugu ambayo jeshi la polisi limeyafumbia macho na kuyazibia masikio kwasababu wapo Tarime kulinda maslahi ya chama dola (CCM).Inasikitisha sana namna polisi wanavyo-operate katika kampeni kwa kuhakikisha kuwa CCM inapora haki ya wananchi wa Tarime ambao kwa ridhaa yao wanaweza kufanya maamuzi ya msingi ya kumchagua kiongozi wanaempenda.

Shutuma dhidi ya mgombea wa chadema na viongozi wake kuwa wametoa maneno ya kuhamasisha vurugu ni aina nyingine ya mbinu za ‘rafu’ wanazotumia CCM katika kuibaka demokrasia ya kweli, uhuru na haki ya wanatarime.Kwa mtu mwenye kufuatilia mambo hatashangaa hali hii kutokea kwani mwishoni mwa wiki kamishina wa makosa ya jinai Robert Manumba alikaririwa akisema kuwa jeshi la polisi litatumia nguvu kukabili hali ya ukosefu wa amani.Kauli ya Manumba ni dhahiri kuwa ilikuwa na kasoro kwa kuwa ilitolewa wakati tayari mazingira ya kuwepo kwa vurugu yalishaandiwa na CCM na vibaraka wake kwa kuendesha siasa za chuki na uchochezi.

Kinachofanyika sasa Tarime ni kutekeleza kauli ya Manumba kwa kutumia nguvu kubwa juu ya matokeo ya vurugu ambazo CCM wameshazitekeleza tangu mwanzo wa kampeni.
Kinachotokea Tarime kwasasa ni kuwa kila anayeonekana kuwa kinyume cha CCM ni mleta vurugu.Njia ya kuwapunguza wanaoipinga CCM ni kuwakamata hasa siku za mwisho wa kampeni na kuwafungulia mashtaka kusudi wasishiriki uchaguzi.Wakati hili linatekelezwa na polisi tusishangae wanatarime wengi wakikosa pia kupiga kura kwa majina yao kutoonekana kwenye daftari la kudumu.Kwa CCM yote yawezekana.
 
wanachezea hisia za watu, wanataka watu waandamane, washambulie magari ya Polisi, lile gari la kumwaga maji liwasambaratishe, "hali ichafuke" na watu wawili watatu wauawe na risasi ambazo itahitajika tume kutambua kama ni za Polisi, na by Thursday au Friday (machafuko yakifikia kilele) uchaguzi utangazwe kuahirishwa as I dokezad last week.

Kama wana hekima yoyote wangesubiri uchaguzi upite na mgombea wa CCM akipoteza kukata rufaa kupinga uchaguzi huo. Lakini sasa ni "at whatever cost".

Umesema vema MKJ,

CCM wanatumia kila weapon walio na uwezo wa kuitumia na kwa hali ilivyo wanataka wanatarime wenyewe wajiingize mtegoni kwa kuendeleza vurugu ambazo wao CCM wamezianza tangu mwanzo wa kampeni lakini kisayansi zaidi kwa kutumia majukwa, vibaraka (mtikila).Wameshaona maji ya shingo na wanataka kugeza picha kusudi waonekane hawamo.

Watuua mwili lakini roho haitakufa kamwe
 
Watatuua mwili lakini roho haitakufa kamwe
 
Habari kutoka tarime zinasema mji mzima ulikuwa mshikemshike huku mabomu ya machozi yakinyesha kama mvua. Polisi wametumia pia risasi za moto. Vijana wawili wemejeruhiwa, mmoja amevunjika mkono na mmoja amevunjika mgu. Bado haijajulikana kama wameumia kutokana na kupigwa risasi au ni kutokana na kimbiakimbia kuepuka vurugu.

Du hii sasa inaonekana itashinda kosovo hii!

Kuna haja ya kutumia risasi kweli? Kwa upande mwingine nafikiria polisi kwa upande mwingine wanachochea hizi ghasia na fujo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom