Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
kpleo.jpg
 
Hujajibu swali!

maswali mengine hayahitaji majibu kwani jinsi yalivyo yanakuwa na majibu ndani yake. Na lako ni mojawapo ya maswali ya aina hiyo. Na hili kuonesha jinsi hiyo unajibiwa kwa swali litakalokuongoza kwenye jibu. Ukijibu hilo swali nililokuuliza utapata jibu ya swali uliloniuliza.
 
Hivi kwanini vyama vya upinzani na wananchi wengine wasiwaachie hawa CCM hilo jimbo (Kuzira)?. Maana lolote litakalofanywa na vyama vya upinzani katika kupigania jimbo hilo, bado CCM itacheza rafu, itatumia maguvu na pesa kuchukua jimbo hilo.

Wananchi wote tukatae kuitambua serikali iliyopo madarakani kwa maana kwamba tuunde serikali yetu wenyewe.
 
Kushindana na CCM kwenye vurugu ni strategy mbovu mno. Njia ya kuwaondoa CCM ni kwa hoja maana penye vurugu wao ndio wanapenda na kupeta.

Hivi Lissu wakati Mtikila anapigwa si angetoa tamko pia?

Kwa nchi zetu maskini, amani ni mtaji muhimu sana.
 
Hali hii Tarime ilitegemewa. Sisiemu hakuna wanakogombea bila rafu.
Kuna mkoa mmoja wa kanda ya ziwa nilishuhudia vijana wa ccm wakiwapiga watu barabarani kwa nondo hadi kulazwa hospital wakiwa taabani ule uchaguzi ulopita 2005, kwa kuwa tu walikuwa wanashabikia mgombea wa chama pinzani na wala polisi hawakufanya kitu pamoja na kwamba waliwajua na kuna mwandishi wa habari aliye warekodi katika tukio hili live.
Polisi wa Tanzania ni tool ya sisiemu katika chaguzi je tufanyeje ili nao tuwakomeshe??????? kweli hatuna namna?
Walimu wakipunjwa mafao yao wanagoma, madaktari pia na wafanyakazi wengine nao wakipunjwa mafao wanagoma Je watanzania tunaweza kuwafanyaje polisi kuonyesha anger yetu jamani????
 
Nchi yetu inapelekwa kuzimu na chama cha Mapinduzi, watanzania tusipokuwa makini historia itakuja kutuhukumu, CCM ya leo imeshakuwa Muflis wameishiwa na sera sasa wanategemea jeshi, na tunawahakikishia wananchi wa Tanzania kwamba wasiwe na wasiwasi kwa Uchaguzi wa jimbo la Tarime, tupo tayari kwa lolote, si mkuki si bunduki Chadema haibanduki Tarime tumejiandaa, kikosi chetu cha vijana kipo makini sana.

Tunawataka CCM waache mara moja kulitumia jeshi la Polisi vibaya, na pia tunamtaka Kamanda Tossi atekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kila analolifanya tunalijua wapo askari wema ndani ya kikosi chake ambao wanatupa taarifa za siri hivyo wasijidanganye. hatua kwa hatua tunazifahamu njama zao na sisi tunajiandaa kikamilifu.
 
Lissu si mkurugenzi wa DP, Mtikila alitakiwa awe na wakurugenzi wake wa kutoa matamko kwa bahati mbaya chama cha DP ni cha mtikila kama MWenyekiti na Mke wake ndiye Katibu Mkuu hivyo kumtpia Lissu msalaba huo humtendei haki ndugu yangu.
 
Kushindana na CCM kwenye vurugu ni strategy mbovu mno. Njia ya kuwaondoa CCM ni kwa hoja maana penye vurugu wao ndio wanapenda na kupeta.

Hivi Lissu wakati Mtikila anapigwa si angetoa tamko pia?

Kwa nchi zetu maskini, amani ni mtaji muhimu sana.

Mtanzania,
Lissu atoe tamshi aseme nini? Mbona mimi sikutoa tamshi? kwi!kwi!kwi!
 
Mtanzania,
Lissu atoe tamshi aseme nini? Mbona mimi sikutoa tamshi? kwi!kwi!kwi!

Jasusi,

Kuna jamaa aliwahi kuniambia, wakati mzuri wa kupinga tendo baya ni wakati linamsulubisha mbaya wako. Wangapi tuko tayari kuona ukweli huo? Inabidi tulaani vurugu za aina yoyote ile bila kuangalia zinamdhuru nani.
 
Kulaani, kukumbusha na kuasa ni muhimu.

Muhimu zaidi ni kuchukua hatua za kisheria -ikibidi kushitaki - na za kijamii kuhamasisha/ kuelimisha watu (this being in the public education category).

CHADEMA wamechukua hatua gani za kisheria, sio lazima kushitaki hata kama ni kukusanya ushahidi unaoweza kusimama mahakamani baadaye kama utahitajika?
 
Jasusi,

Kuna jamaa aliwahi kuniambia, wakati mzuri wa kupinga tendo baya ni wakati linamsulubisha mbaya wako. Wangapi tuko tayari kuona ukweli huo? Inabidi tulaani vurugu za aina yoyote ile bila kuangalia zinamdhuru nani.

Well, if we have enough resources kurukia rukia mambo ya wengine. US could do that.
 
Jasusi,

Kuna jamaa aliwahi kuniambia, wakati mzuri wa kupinga tendo baya ni wakati linamsulubisha mbaya wako. Wangapi tuko tayari kuona ukweli huo? Inabidi tulaani vurugu za aina yoyote ile bila kuangalia zinamdhuru nani.

Mtanzania
Wewe una tatizo kubwa sana na tatizo lako wewe unatafuta na ungependa Haki ya kweli ipatikane ,uhuru wa kweli uwepo , demokrasia ya kweli iwepo na fitina na chuki iwe mwiko.

Wakati wezako wanatafuta umaarufu kisiasa na kaposho ka kufinga mfukoni kapatikane hilo ndilo eneo unapopisha na wanajeshi wezako.

Wezako wana tageti maeneo watayopata umaarufu na pamoja na umaarufu huo wapate kuongeza jimbo ambalo litafanya kiposho kiongezeke.

Sasa wewe unasema Mtikila kweli ktk hilo la Mtikila litawapa umaarufu kiasiasa? na je ktk hilo la Mtikila wanaweza ongeza kijimbo cha kufinga posho?
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana aliwasili Tarime na kulakiwa na mamia ya mashabiki, wanachama na wananchi wa wilaya hiyo.
Kuwasili kwa Mbowe wilayani hapa akija kuwaongezea nguvu wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho, kulibadili kabisa mwenendo wa mambo katika maeneo mbalimbali aliyopita akiwa ndani ya gari na hata alipolazimishwa na wafuasi wake kuteremka chini na kutembea nao kwa miguu huku akisimama katika eneo moja baada ya jingine kuwasalimia wapiga kura wa jimbo hilo.
Msafara wa kumlaki Mbowe aliyewasili majira ya saa 8:00 mchana, ulioongozwa na wapanda pikipiki wanaokadiriwa kufikia 200, ulianzia katika Kijiji cha Komaswa, kilichopo umbali wa kilomita zipatazo 23 kutoka Tarime mjini.

Mara baada ya kupokewa katika kijiji hicho, Mbowe aliyekuwa amevalia kombati alilazimika kusimama katika Kijiji cha kwanza cha Mika kilichopo wilayani Rorya baada ya kuombwa afanye hivyo na wafuasi wake kwa dakika zisizozidi tano.

Akizungumza katika salamu zake hizo za kwanza kabisa, Mbowe alisema amekwenda Tarime kwa nia moja ya kusambaratisha kile alichokiita mtandao wa ufisadi ambao umekuwa ukilitafuna taifa kwa kipindi kirefu hata kuwanyima haki wananchi wenye kipato cha chini.

Katika hali isiyotarajiwa, polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kuufuatilia msafara huo wa Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA uliokuwa ukivuta makumi ya watu kila ulipokuwa ukipita wakitumia magari yaliyokuwa na namba za usajili za nchi jirani ya Kenya.

Kwa mara ya kwanza gari lililokuwa na polisi liliwasili katika eneo la Mika alipokuwa akihutubia mwanasiasa huyo likiwa na namba mbili tofauti; KAD 493 E na 493 KAU E.
Mshindo wa ukubwa wa msafara uliofika kumpokea Mbowe ulizidi kuwa mkubwa baada ya kuwasilia katika eneo la Buhemba ambako kina mama walionekana wakiacha shughuli zao na kujumuika na wana-CHADEMA kumlaki kiongozi wao mkuu huku wakionyesha alama ya vidole ya ‘V', inayotumiwa na chama hicho kuonyesha ushindi.

Hali hiyo ya watu wengi kutaka kumlaki, ilisababisha alazimike kusimama katika eneo hilo na kuwahutubia wananchi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza huku wakipunga bendera za chama hicho na matawi ya miti.

Akihutubia hapo, alianza kwa kusema, '‘CCM na Jeshi la Polisi wanapaswa kutambua kuwa, matumizi ya nguvu za kupita kiasi, risasi na mabomu ya machozi haviwezi kufua dafu mbele ya nguvu ya umma.

"Kamanda wenu nimekuja kukiambia Chama Cha Mapinduzi na Jeshi la Polisi kwamba, mabomu, risasi na nguvu zao wanazotumia mbele ya umma wa wananchi wa Tarime haziwezi kusaidia kwa vile nguvu zao haziwezi kupingana na nguvu ya umma," alisema Mbowe na kupokewa na mshindo wa makofi na vigelegele.
Alisema pamoja na kwamba, polisi wamekuwa wakiwapiga kama mbinu ya kuwatisha, CCM haiwezi kamwe kushinda ubunge wa Tarime katika uchaguzi ulio huru na wa haki.
Akizungumza kwa sauti ya juu, Mbowe alisema ni jambo la kusikitisha kwamba, tangu kampeni zilipozinduliwa Septemba 14 mwaka huu, Jeshi la Polisi limekuwa sehemu muhimu ya kampeni za CCM.

"Nawaambia ndugu zangu haki ya mwana-Tarime kamwe haiwezi kupotea, namwambia Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) na mgombea wake, haki ya wananchi wa Tarime wenye mapenzi mema na CHADEMA hawatakubali kuona ikipotea," alisema Mbowe.

Baada ya kumalizia kuhutubia eneo hilo, msafara wake ulianza kuelekea katikati ya mji wa Tarime kupitia barabara za Nyerere na Nyamwaga hadi kwenye viwanja vya Mennonite, ambako pia kulikuwa na mamia ya wananchi, tofauti kabisa na ilivyokuwa ikifikiriwa awali.
Hali ilizidi kubadilika baada ya kukamata barabara ya Nyamwaga, ambako watu walioona msafara huo, waliacha kazi walizokuwa wanafanya na kufuatilia.

Kitendo hicho kilisababisha biashara zilizokuwa kandokando ya barabara hiyo kufungwa kwa muda kutokana na utitiri wa watu waliofurika kuelekea kwenye viwanja vya Mennonite.
Mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo, Mbowe aliwaomba wananchi wote kukaa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili nje kidogo ya mji wa Dodoma, Julai 29, mwaka huu.Alisema lengo lake kubwa la kufika mjini hapa ni kuendeleza mapambano ya kuhakikisha kwamba jiimbo hilo linabaki mikononi mwa CHADEMA kama njia pekee ya kumuenzi marehemu Wangwe.

"Napenda kuwaambia kwamba leo (jana) nimekuja hapa kwa kazi moja tu ndugu zangu... nayo ni kuendeleza mapambano ya kuhakikisha kwamba tunakomboa jimbo letu na kuendelea kuitawala Halmashauri ya Wilaya ya Tarime. Kufanya hivi ndiyo njia pekee ya kumuenzi marehemu Wangwe," alisema Mbowe.
Mbali ya hilo, Mbowe alieleza kusikitishwa na kukerwa na tuhuma zinazoelekezwa dhidi yake yeye na chama chake kwamba, alishiriki kusababisha kifo cha marehemu Wangwe.
"Eti CCM wanasema mimi na chama chetu tumemuua marehemu Wangwe. Napenda kuwahakikishia kwamba hatukuhusika na suala hili na inawezekana kwamba hao wanaosema, ndio waliohusika," alisema Mbowe.

Alisema kutokana na chuki hizo za kupandikizwa, Tarime itaendelea kudumu na haki ya msingi itatolewa na Mungu kama kweli alihusika na kifo hicho, na kwamba huo ni mkakati wa vyombo vya dola kutaka kudhoofisha nguvu za chama chake pamoja na wabunge wake ambao wamekuwa mwiba mkali kwao.

"Nawahakikishia kwamba mimi siogopi kitu chochote. Hawa hawawezi kunizuia jambo lolote lile, mimi nalindwa na Mungu na kama CCM hawalijui hili, naomba walitambue kuanzia sasa," alisema.
Alisema kwamba yuko tayari kufia Tarime ili kuona haki ya kila mtu inapatikana, kwani hii ndiyo kazi aliyofanya marehemu hadi wakati mauti yakimfika.


"Mimi nasema jamani niko tayati kufia Tarime kwa ajili ya kuona haki za wananchi wote wa hapa zinapatikana baada ya mateso makubwa mliyoyapata kutoka CCM kwa miaka yote iliyopita... nawauliza mko tayari kurudia makosa?" alihoji Mbowe.


Mbali ya hilo, Mbowe alitumia fursa hiyo kutangaza kwamba, kuanzia kesho anakusudia kuanza kufanya kampeni katika jimbo hilo akimnadi mgombea wake wa ubunge, Charles Mwera na yule wa udiwani, John Suguta, akitumia helikopta kama ilivyo kawaida yake.



Mytake:
Neno eti lina maana gani?pesa ya Helikopta ni nani analipa??Lafu sula la kutumia sympathy ili watu wamhurumie nadhani ni kukosa mwelekeo ,matumizi ya neno ndugu inaonesha jinsia anvyopunguza gap la ukabila ambalo limetawala watu wake wa karibu.Unaweza kuta helikopta ni mtaji wa Mbowe na anatumia Ruzuku ya chama kujiingizia kioato..Kama chama kinauzika Helikopta ya nini?walitumia helikopta kiteto na wakashindwa..

lets wait and see
 
Mbowe anafanya vyema.

Kutumia helikopta ni vizuri ukizingatia ubovu wa barabara wilayani tarime na vijiji kuwa scattered sana.

Kingine ni kuwa ushindi wa Tarime kwa Chadema itakuwa imeongezea watu wengi imani na Chadema.

Ila on a positive note sidhani kama Chadema watashinda. Mie yeyote atakaeshinda kihalali kwangu ni sawa CCM sio mama wala baba yangu ingawa ni mwanachama.
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana aliwasili Tarime na kulakiwa na mamia ya mashabiki, wanachama na wananchi wa wilaya hiyo.
Kuwasili kwa Mbowe wilayani hapa akija kuwaongezea nguvu wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho, kulibadili kabisa mwenendo wa mambo katika maeneo mbalimbali aliyopita akiwa ndani ya gari na hata alipolazimishwa na wafuasi wake kuteremka chini na kutembea nao kwa miguu huku akisimama katika eneo moja baada ya jingine kuwasalimia wapiga kura wa jimbo hilo.
Msafara wa kumlaki Mbowe aliyewasili majira ya saa 8:00 mchana, ulioongozwa na wapanda pikipiki wanaokadiriwa kufikia 200, ulianzia katika Kijiji cha Komaswa, kilichopo umbali wa kilomita zipatazo 23 kutoka Tarime mjini. .................................................................................................
....................................................................................................
Mytake:
Neno eti lina maana gani?pesa ya Helikopta ni nani analipa??Lafu sula la kutumia sympathy ili watu wamhurumie nadhani ni kukosa mwelekeo ,matumizi ya neno ndugu inaonesha jinsia anvyopunguza gap la ukabila ambalo limetawala watu wake wa karibu.Unaweza kuta helikopta ni mtaji wa Mbowe na anatumia Ruzuku ya chama kujiingizia kioato..Kama chama kinauzika Helikopta ya nini?walitumia helikopta kiteto na wakashindwa..

lets wait and see

Tanzania bwana, bahati mbaya huu ndio upeo wetu wa kufikiri. I find it hard to respond to comments like this - hivi tumelogwa ?
 
Tanzania bwana, bahati mbaya huu ndio upeo wetu wa kufikiri. I find it hard to respond to comments like this - hivi tumelogwa ?

Mkuu,

Usijisumbue na hizo narrow minded.wengine sijui huja hapa kuondoa stress?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom