Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Nadhani haka kamchezo ka TARIME kanatupa picha halisi ya mbinu zinazo tumiwa na hawa grini pati. Bado naendelea kuamini kuwa kila kitu kina mwisho wake

Kazi kwetu!!!!!!!!!!!!
 
Hengera sana CHADEMA! Jana nilikesha hapa kusubiria matokeo,leo nilikua na pepa lakini kimeeleweka.

Ushindi huu ni ushindi wa wapenda mabadiliko,wenye nia ya dhati na taifa letu tukufu,wachukia dhuluma,ufisadi,manyanyaso,fitina na vitisho.

Ni ushindi dhidi ya CCM na maluki wa upinzani,ni ushindi dhidi ya polisi wasio waadilifu,usalama wa taifa uliopoteza dira,tume isiokua huru ya uchaguzi,mfumo kandamizi usopenda demokrasia ya vyama vingi ishamiri na ni laana dhidi ya watumiao misiba kama kivutio cha wapiga kura,na ni ushindi dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ili kuidhulumu haki na kiu ya mapinduzi.
Mungu awaponye wale waliomia na kudhalilishwa ktk mchakato huu,awaponye wenye majeraha ya Moyo na Mwili katika kusimamia kile walichoamini.Wanatarime kwa mara nyingine tena wamedhihirisha nguvu ya mabadiliko.
Ni mfano wa kuigwa katika taifa,nguvu wanazotumia polisi dhidi ya wanatarime wakati matokeo rasmi yakisubiriwa kutangazwa ni ishara nyingine ya kutokubali kushindwa.Hili jimbo lisiwe chanzo cha chuki,unyama na visasi.Hizo ni Rasha rasha kwa CCM,wasubiri nguvu kuu 2010.
Mungu Ibariki CHADEMA,wape uvumilivu wanatarime,Mungu Ibariki Tanzania

Imeshatangazwa rasmi?
 
Hali ya Tarime ni tete zaidi ya siku za nyuma baada ya vuta nikuvute ya kutotangaza matokeo sasa naambiwa defender inawaka na natafuta namna kufika iliko ili niweze ku confirm ila naambiwa hapa kwamba watu wamerudi majumbani kutwaa silaha zao baada ya Polisi kuanza upuuzi wao.Stay tuned .
Muungwana anaangalia kwenye TV tu akinywa maziwa huku watu wanaanza kuuana......wananchi wamekataa ya nini sisiemu wang'ang'anie wasipopendwa?
 
Hali ya Tarime ni tete zaidi ya siku za nyuma baada ya vuta nikuvute ya kutotangaza matokeo sasa naambiwa defender inawaka na natafuta namna kufika iliko ili niweze ku confirm ila naambiwa hapa kwamba watu wamerudi majumbani kutwaa silaha zao baada ya Polisi kuanza upuuzi wao.Stay tuned .

Haya ndio mambo ambayo wengi tulikuwa tunayahofia, naona sasa yanatokea. Sirikali isiwalazimishe watu kula wasichotaka. Mkuu Lunyungu tunashukuru kwa updates hizi
 
Jamani bado tu mbona media za kibongo ziko slow kupata habari kwa kujipenyeza? This news should be out by now au ndo urasimu wa taarifa
 
Tbc live- mwera (chadema)aaaaaaaaa! 34,500 votes! Amekabidhiwa cheti cha ushindi
hongera chadema!!!!!!!!! Ushindi kwa demokrasia!
 
Matoke tayari yametangazwa na tume
Mwera 34,545 na Kangoye 28 669

Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaa!

Kuna watu watalia hapa,ila kwa sababu ya kuwa nyuma ya PC itaondoa aibu ya mtu mzima kulia
 
Tbc live- mwera (chadema)aaaaaaaaa! 34,500 votes! Amekabidhiwa cheti cha ushindi
hongera chadema!!!!!!!!! Ushindi kwa demokrasia!



Mkuu,hata lunch sijaenda mpaka kieleweke
 
Huku tunapopelekwa siko kabisa, CHADEMA wameshinda lakini kumeripotiwa mapambano makali baina ya WanaCHADEMA na Polisi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom