Rafiki yangu wewe hukai ubungo kwanza uko ubungo gani mimi naishi ubungo toka mwaka 90 najua mengi kuhusu hapa ubungo unachojaribu kufanya wewe ni kupata mawazo ya wengine pengine uandae makala , nenda gide kwa mfano uliza kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita mpaka sasa kuna maendeleo gani haswa kwenye sekta ya maji mtandao wa maji ,

Tumechoshwa na hadidu rejea Kiti cha Ubunge Jimbo la Ubungo kinanadiwa na CCM kana kwamba Ubungo haina wenyewe,Alikuja Lamwai(NCCR kwa malumbano m,azito maendeleo hayakuonekana),Kafuata Keenja(vipindi viwili bila lolote) sasa tunaandaliwa kumpokea Mwangunga(Ambaye wizara ya mali asili imemshinda tunaletewa atusaidie nini??!!Sasa sisi wananchi wa Ubungo tunashindwa kuelewa kupewa ubunge wa Ubungo ni zawadi tuu au ni ushindani?
Na huyo Nape ameishia wapi maana nilisikia na yeye alikuwa analitaka hilo jimbo. Ukweli ni kwamba CCM haijawahi kushinda kihalali jimbo la Ubungo. Mara zote wanafanya wizi tu. Mara ya mwisho Chadema walishinda lakini tume ikaamua vinginevyo. Na kwa mtindo wa sasa kwamba wawakilishi wa vyama kwenye vituo hawalipwi tena na tume ya uchanguzi (nafikiri ndivyo ilivyo kwa sasa), CCM wanakuja na rushwa yao na kuwaonga mawakala wa vyama na kusaini matokeo ya uongo kwenye vituo kuonyesha kwamba CCM imeshinda. Kuna haja ya kuangalia ni jinsi gani tunaweza kulinda kura zetu badala ya kutegemea watu wachache wanaowekwa na vyama kama mawakala.
Na wana Ubungo inabidi tufike mahali tuchoke kulazimishwa na CCM kuwa na wabunge wasioijua ubungo. Wagombea wote walioletwa na CCM kugombea ubungo hakuna hata mmoja anakaa Ubungo. Hatutaki mtu akae Masaki au Osterbay halafu eti aje kugombea kuwa mbunge wa jimbo la ubungo. Huyu atayajuaje matatizo yaliyopo Ubungo? Kwa kuambiwa tu? No tunataka mtu anayekaa kati ya wakazi wa Ubungo ndiye aje tumpe Ubunge.
Mnyika, Usiache kugombea tena lakini tengeneza utaratibu mzuri wa kulinda zetu.
Tiba
Ndugu yangu mimi ni mzaliwa wa Ubungo nimekulia Ubungo na kusoma Ubungo sasa nazeekea Ubungo hayo unayoyasema ni sehemu ndogo sana ya maendeleo kwani hata huo mradi wa maji Gide siyo juhudi za hao watu unaowaita Wabunge wakuja,Ni mpango wa miaka kadhaa wa serikali baada ya kuona wananchi wanatoboa bomba linalopita Ubungo kwani wao walikuwa hawapati hayo maji,
Kuletewa ??? !!!!!! Wacha nikushangae kidogo. Mnaletewa na nani ?? Kwani mmlazimishwa ?????? Nawe ukitaka si kagombee.....unalalamika wakati kisu unacho mkononi !!! Usijidhalilishe wakwetu.
Kibiongo wewe uko wapi??Mbona kura tulimpigia Mnyika akachaguliwa Keenja?Mbona hilo liko wazi kabisa?Uchaguzi wa 2005 kituo kimoja wapiga kura waliojiandikisha pale Royal EDP ni 3561 Waliopiga kura jumla walikuwa 4,005 tofauti hiyo ilitoka wapi?Tunajua kinachoendelea ndani ya Uchaguzi wa nchi maskini,Hili la Ubungo tunalielewa sisi wakaazi wa huku,Hakuna Mbunge aliyechaguliwa wa chama tawala ambaye maskani yake ni Ubungo.a shida za ubungo siyo maji tuu Mbunge kukutana na watu wake,kujua matatizo ya watu wake nk
Ndugu kinachotakiwa ni mipango inayotekelezeka kwa kuanzia na wananchi wenyewe wa maeneo husika kama wananchi hawataki kufanya kazi , kupeleka watoto wao shule , kupigania haki zao mpaka mbunge aje tena anayekaa hapo hapo unataka nini zaidi ? anza michakato hiyo mitaani humu jf kuna wachache sana wanaoishi ubungo pia ni watu wachache sana waliounganishwa kwenye mtandao wa kompyuta ubungo jitihada hizi angalia upya
Kibiongo wewe uko wapi??Mbona kura tulimpigia Mnyika akachaguliwa Keenja?Mbona hilo liko wazi kabisa?Uchaguzi wa 2005 kituo kimoja wapiga kura waliojiandikisha pale Royal EDP ni 3561 Waliopiga kura jumla walikuwa 4,005 tofauti hiyo ilitoka wapi?Tunajua kinachoendelea ndani ya Uchaguzi wa nchi maskini,Hili la Ubungo tunalielewa sisi wakaazi wa huku,Hakuna Mbunge aliyechaguliwa wa chama tawala ambaye maskani yake ni Ubungo.a shida za ubungo siyo maji tuu Mbunge kukutana na watu wake,kujua matatizo ya watu wake nk
Mkuu unauhakika wanafanya wizi wa kura, weka vithibitisho hapa jamvini na si kuongea kinadharia tu.