Ubunge wa CCM ni "FURSA ya Kutoka" kuwa Waziri, Kupata Ajira ya miaka 5 au mengine mengine

Ubunge wa CCM ni "FURSA ya Kutoka" kuwa Waziri, Kupata Ajira ya miaka 5 au mengine mengine

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Posts
1,484
Reaction score
2,892
Rais Magufuli anamaliza ungwe yake ya kwanza ya miaka 5 na sasa anakwenda ungwe ya pili 2020-25. Bila shaka atashinda kwa maana wapinzani wake wana hoja dhaifu na maandalizi yao ni muda mfupi kiasi ambacho wanakosa muda na agenda ya kupindua meza ya kifikra ili kuchukua Urais. Ila hoja yangu leo, nadhani ijikite kwa wagombea ubunge, hasa kwa dirisha la CCM.

Nadhani wagombea ubunge wanaounga mkono mema Rais anayofanya wanamkwamisha hata kabla hawajaanza safari ya kuomba ridhaa ya wana CCM kabla ya kupata uteuzi wa mwisho.
Kuna vichwa ambavyo vitapenya na huenda katika hao tukapata Spika na Naibu Spika, Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu Waziri. Japo tunakumbuka Mzee Msekwa aakiwa spika, alitengeneza dirisha la sio LAZIMA spika kuwa mbunge nae akafaidika na mfumo huo mwaka 2000.

Kuna watu wasomi kwa kukusanya wingi wa shahada vs wale wanaojua kusoma na kuandika wamo kwenye kundi kubwa la kupwaya kwa maana bila shaka hawajui muktadha wa sasa.

Enzi za Rais Nyerere, Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete term ya kwanza; nadhani sifa ya mbunge kupeleka hoja serikalini au bungeni ilikuwa na mashiko.

Isipokuwa toka 2010 ambapo vyombo vya habari vimekuwa sio chanzo tena cha habari, bali Watanzania kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakionesha kwa uwazi kwa picha au video madhaifu ya barabara, huduma elimu kama shule haina madawati au changamo yoyote na kutaka uwajibikaji wa Serikali (executive branch) ihusike kutatua matatizo ya wananchi.

Nashauri kwa wabunge kwa kuwa bado mna nafasi ya kujitengenezea kampeni, iko haja sifa zenu za wingi wa shahada zisiwafanye kujiona mna akili sana; bali iko haja ya kutuambia mnataka kuitoa jamii ya Watanzania hapa ili ifike wapi kwenye miaka 5 ijayo.

Ntagusia maeneo mawili kwa ufupi na mifano iliyo hai;

AJIRA
Nadhani shida ya ajira ni ukweli ulio wazi
Huenda huu nao umekuwa mkakati wa wagombea, ili mtu akipenya anajua kuna pensheni ya mil 200 na zaidi in 5years. Hapo ni uwe ume deliver au huja deliver.
Zamani mtu wa diploma alikuwa na nafasi ya kuwa DAS, DED ila kwa kuwa wasomi wamekuwa wengi kwa sasa DAS/DED sifa moja wapo ni shahada ya uzamili. .

Ni kwa namna gani hawa wanaogombania ubunge wakikosa uteuzi wa ubunge kuna baadhi wanawinda uteuzi kwa DAS, DC, DED, RC au RAS. Hapa ajira zimekuwa chanzo cha kufukuzia bumu la mshahara wa kibunge au basi ikishindikana kutembea na VX V8 kwa nafasi hizo hapo juu.

Ila nadhani tulitakiwa kupata wabunge ambao wangekuja na hoja za kimkakati kukaa na serikali kwa hoja ili kutengeneza strategic financial leverage kwa ajili ya investment financing kwenye kilimo cha kibiashara na agro-processing au manufacturing kwa kutumia agro inputs.

Kwa mujibu wa tovuti ya TIC

Tanzania has a sugar demand gap of about 220,000 tons met through imports

In 2015 Tanzania imported 60% of its edible oil

Trade in meat has increased significantly, with more and more countries seeking to close their supply gap through imports. Major meat exporters, especially in South America, face logistical challenges to supply new growth areas in Africa, Middle East and Asia


Hii nchi kwa ukubwa wa ardhi iliyopo na vyanzo vya maji, ni namna gani tunaziba pengo la sukari kwa kuzalisha ndani kukidhi soko la walaji wa kawaida na soko la viwanda?

Uhitaji wa mafuta, namna gani tunachagiza kulima kibiashara zao la alizeti kwa mfano ili ndani ya miezi 3 uvunaji unafanyika na kuuza kwenye viwanda vya ndani kukamua mafuta kukidhi soko ambalo lina uhitaji wa 60%?

Pamba, kwanini tutengeneze vitambaa kwa kuweka viwanda ndani ili kutengeneza ajira za Watanzania ila tuna hakika pamba itazalisha vitambaa kwa

School uniforms kwa primary, sekondari na vyuo vya kati
Staff uniforms kwa wanajeshi (JWTZ, Magereza, Polisi, Uhamiaji)
Kanga na vitenge,
uniform za hospitali

On serious notice, CAPEX ya kiwanda cha kati cha kutoka pamba mpaka kuwa na kitambaa cha nguo haizidi bil 20; yet tuna zaidi ya bil 120 zilibaki kwenye bank ya uwekezaji; na hakuna strategic move ya namna gani zitumike.

Mpaka lini tuendelee kulima pamba na kuuza India na China then wakati huo huo makontena ya mashuka lebo ya MSD yanakuwa imported kwa ajili ya hospitali zetu???

Hii sio sawa karne ya 21; wakati karne ya 20 Rais Julius Nyerere walau alitengeneza vitambaa na mashuka na mablaketi kwa kutumia old technology.

Natagemea hii iwe ni agenda kama kweli watu wana nia ya kweli kumuunga mkono Rais JPM.

Nilitegemea hata bunge la juzi lililo ahirishwa, wabunge wawe wakali kwanini TIB kabakiza zaidi ya bil 120 pasipo kuwa na mkakati wa uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati kwa lengo la kutengeneza faida, kutoa ajira, kuongeza tax base, kurejesha mkopo na kupunguza imports.

Hii ni sehemu ya hotuba ya waziri wa fedha…
Benki ya Kilimo Tanzania ilitoa mikopo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 35.86 sawa na ufanisi wa asilimia 176.3 ya lengo la kukopesha shilingi bilioni 20.34 na benki ya TIB shilingi bilioni 18.58 sawa na asilimia 12.86 ya lengo la kukopesha shilingi bilioni 144.5….

Otheriwise, naona, nasikia bla bla nyingi; ni heri hata wangezungumza issues/solutions ili utekelezaji uwe zero then tuilaumu serikali; vinginevyo tunaweza kuwa na bunge ambalo siujui tutalipa jina gani mara baada ya muda wake kuhitimshwa 2025.

Maandiko yameandika …kwa kukosa maono watu hupotea/without vision people perish.

To be honest, kuna wagombea wengi wanaojua kusoma na kuandika na wenye madigrii mengi hawana vision ya kuwafanyia nini wananchi majimboni au Tanzania kwa upana wake. Na ndipo hapo kuna nakisi kubwa kati ya miradi ya mikubwa ya serikali namna gani wagombea hawajui namna ya kui-connect shughuli za uchumi mdogo unazaa biashara ndogondongo na na uchumi wa kati unaozaa biashara za kiwango cha kati.

Kila la kheri wagombea; Watanzania tupo tayari kuwapigia kura; na kuna wakati huwa tunampigia kura hata mtu mwenye kupiga michapo tu, wala hana substance; ila kwa kuwa kajaliwa kuupepete mdomo kwa maneno mengi basi tunadhani huyu ndiye.

Shalom


Tanzania, Tanznaia nakupenda kwa moyo wote.
 
Mkuu mleta mada, kutokana na nguvu na affordability ya social media, mtu yeyote mwenye hoja yoyote ya maana anaweza kuitoa kupitia kwenye social media na ikafika inakostahili. Haihitaji kuwa mbunge kwanza ili ndio utoe hoja za maana.

Kama tayari mtu ana utaratibu wa kutoa hoja za maana, hata akiwa mbunge tunatarajia ataendelea kutoa hoja za maana, lakini kama mtu hajawahi kuonekana anatoa hoja za maana (katika zama hizi za social media) hata awe mbunge hamna kitu hapo zaidi ya kujaza nafasi wazi.

Mwisho wa siku watanzania ndio hawa hawa na tunajijua tulivyo.
 
Kukosa Ajira
Kuaminishwa ziko pesa bwelele kwa wakuunga juhudi
Kukosa muelekeo
Wajinga na wapumbavu ndio kipaumbele kwa watawala
Tumeachwa peke yetu hatuna Mtetezi kama Taifa
Upinzani bado hawajajitambua
Ubinafsi Uchoyo Roho Mbaya vimetutawala sana
Makanisa Misikiti na wasio na imani ni wakati wa kuomba sana
Yajayo ni Mungu atuokoe...
 
Back
Top Bottom