Ubunge wa kuteuliwa ni rushwa, matumizi mabaya ya pesa za wananchi na fedheha. Bunge tunaelewa ni sehemu yenye heshima kubwa na mojawapo ya mihumili mitatu ya nchi au dola. Ni sehemu ambayo mtu hutumwa na wananchi wa jimbo la uchaguzi akawawakilishe na kutetea maslahi yao. Ubunge wa kuteuliwa ni udhalilishaji wa wale wanaoteuliwa. Mbunge wa kuteuliwa anafanya kazi ya au anamtetea nani kama siyo kuwafurahisha wale waliomteua? Hivi mbunge wa kuteuliwa naye anatembea kifua mbele kwamba ni mbunge wa nani au anawakilisha nani? Hivi mbunge wa kuteuliwa anapokea yale mamilioni ya shilingi kama mshahara na marupurupu kwa mwezi kwa kazi gani? Mimi nadhani huu ni wizi ambao inabidi ukomeshwe.
Uzoefu unaonyesha kwamba wengi wa hawa wabunge wa kuteuliwa hawachangii hoja bungeni au wakifanya hivyo ni mara chache. Sababu ya kuwa hivyo ni wazi- hakuna msukumo wa kuwafanya wachangie au watoe hoja nzuri bungeni. Wchangie wasichangie pato lao liko pale pale, na hawana watu wa kuwauliza kwa nini wanachangia kidogo au hawachangii kabisa hoja bungeni. Inasikitisha kabisa. Ni gharama isiyostahili kubebwa na walipa kodi wa Tanzania. Ni uptezaji wa pesa ambayo ingeelekezwa eneo lingine kama vile mahospitalini, elimu, miundombinu, n.k. ambako ingelipunguza makali au ingeliboresha.
Kuna ushahidi kwamba katika zoezi zima la kupata wabunge wa kuteuliwa huwa kuna mizengwe mingi ikiwemo rushwa, uswahiba na undugu. Inatokea kwamba baadhi ya watu wanaoteuliwa kuwa wabunge wa kuteuliwa hawana sifa zozote na ndiyo maana hata uchangiaji wao bungeni huwa ni wa shida sana. Watu makini na wenye uzalendo mara nyingi huachwa kwenye kuteua huko.
Sioni mantiki ya kwa nini hawa wabunge wa kuteuliwa wawepo. Inawezekana sababu mojawapo ni kuongeza idadi ya wabunge bungeni. Na kama ni hiyo, kwa nini serikali isianzishe chemba ya pili ya bunge (seneti) kama ilivyo katika nchi nyingi duniani? Na hiyo seneti iwe na wajumbe wa kuchaguliwa tu na siyo kuteuliwa. Chemba ya pili ya seneti itasaidia kurekebisha au kuimarisha mwenendo wa bunge. Kwa sasa bunge linafanya lolote bila chombo kingine kuwepo kinachoweza kulinyooshea kidole. Sheria mbovu au kandamizi hupitishwa bila kujadiliwa kwa umakini wa kutosha. Seneti italeta umakini wa sheria zitakazotungwa.
Kutokana na hayo maelezo hapo juu ni vema basi ubunge wa kuteuliwa ufutwe, na ianzishwe chemba ya pili ya bunge yaani Seneti.