"Toshekeni nyie CCM.. " mkuu umeandika kwa hisia sana, ila umeandika ukweli mtupu. Kitila hana uchungu wowote na wanaubungo zaidi ya kuhangaikia namna ya kutunisha account yake ya benki kwa ajili yake na wale wanaomtegemea kupitia ubunge na uwaziri.
Kweli kabisa kuna mambo yanapofanyiwa binadamu ni lazima yafanywe kwa heshima na utu mana wacha Mungu tunaamini binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Mkapa alipunguza wafanyakazi alipoingia madarakani na kuwalipa.Walisema amefanya redundance.
Kuna wengi walipate hela nzuri tu na wakawa wajasiriamali wazuri ,wengine wakajenga magesti wengine wakanunua gari za abiria na wengine mpaka Leo waliacha familia zao zikiwa na maisha mazuri kwa baada ya kulipwa mafao yao ya kupunguzwa kazini.
Hebu fikiri binadamu sio manyama anavunjiwa nyumba anayoishi na familia yake na watoto wake wakubwa na wadogo,kuna paka ,mbwa ,kuku, bata, njiwa ,mfanyakazi wa ndani n.k. halafu anaachwa nje tu bila kulipwa chochote wala kupewa kiwanja kingine kwenye ardhi aliyoiumba Mwenyezi Mungu, sio mungu wa CCM bali Mungu wa wote muumba wa mbingu na ardhi. Mtu anaachwa kama mbu aliyepuliziwa dawa ili asieneze malaria.
Yaani hata wanayama kule Serengeti hawatendewi hivyo wanapovamia makazi ya watu na Mara nyingine wanaua watu lakini bado wanapelekwa kwa utaratibu mzuri kwenye hifadhi yao au nyingine. Oooh, my God ,wapo wapi watu wanamjua Mungu na thamani ya mwanadamu wakamfukuze Mkumbo kwenye sanduku la kura kama vile wanavyomfukuza pepo mchafu aliyemwingia mwanadam ndani ya nyumba ya ibada?
Mkumbo hajawahi kuona maumivu ya wanadamu waliokua wanalala nje na familia zao kwa sababu ya kujenga mapiramidi yanayoitwa barabara kama enzi za Farao.!
Heshima ya mwanadamu ni kubwa kuliko kitu chochote.
Mkumbo hastahili hata kuweka picha yake kwenye karatasi ya kura kuwaomba wanadamu wanaoishi Ubungo wala Kibamba wampigie kura kupitia CCM, Chama cha watu katili kuliko Wakoloni wa Kireno.