Ubungo flyover interchange in Dar es Salaam

Ubungo flyover interchange in Dar es Salaam

Maneno Meier

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
2,467
Reaction score
1,697
309304885_403618611943345_5539636474814089045_n.jpg

Kwa uelewa wangu maana ya Fly-over Interchange ni makutano ya barabara nyingi za juu na zenye mizunguko mingi inayo ifanya magari kubadilisha barabara na kuendelea na safari bila kusababisha foleni na yenyewe kutokaa katika foleni katika makutano hayo.

Kwa definition hiyo ningependa kutoa rai kwa mara nyingine tena kwa wote wanao husika na ujenzi na usimamizi wa Ubungo Flyover Interchange ya kwamba mwonekano wa hiyo interchange kwenye hiyo clip sidhani kama utaleta result ambayo inategemea kupatikana. Kwa mtazamo wangu na uelewa wangu wa maana ya Interchage, haitakuwa busara kama hiyo interchange ita kuwa na level tatu tu. Level nne zinatakiwa.

Trafic lights kwenye flyover Interchange haitakuwa na maana yeyote katika mkutano hayo. Kwa kadri siku zinavyo kwenda, mji utazidi kupanuka na magari yata zidi kuongezeka kiasi kwamba baada ya mda sio mrefu itabidi kufanya marekebisho tena, kwani foleni zitaongezeka. Na hiyo ni gharama tena kwetu. Zaidi ya hapo ajali ambazo zitasababishwa na hizo trafic lights, zita kuwa kubwa mno na isitoshe umeme usio na uhakika utalazimisha trafic police ku-direct magari. Ushauri wangu kwa wahusika level nne zina takiwa badala ya tatu.

Barabara ya magari yanayo toka mjini kuelekea Mwenge na U-Turn yake kurudi mjini na yale ya kutoka Morogoro kuelekea Nelson Mandela Road na U-Turn yake kurudi Morogoro yawe katika level moja na barabara ya magari yanayo toka Mwenge kuelekea Morogoro na U-Turn yake kurudi Mwenge nayo yanatakiwa yawe kwenye level moja na barabara ya magari yanayotoka Neleson Mandela Road kuelekea mjini na U-Turn yake kurudi Nelson Madela Road. (Angalia picha)
Screenshot_20181209-083538_Gallery%7E2.jpeg

Screenshot_20181209-084146_Gallery.jpeg


Magari ya kutoka Station ya Mabasi ya Mikoani ya Ubungo kwenda mikoani au Nelson Mandela Road yanabidi kupita chini ya Morogoro Road, nyuma ya stand ya mabasi yaenda kasi kwenda Kimara, na kuibukia upande wa pili. Na yale ya kuingia Bus Station yanatakiwa yaingie chini ya Morogoro Road, mbele ya stand ya mabasi ya Mwendo Kasi, na kuibukia upande wa pili wa Station ya Mabasi ya mikoani ya Ubungo.(Angalia picha)
Screenshot_20181209-145510_Earth.jpeg


Barabara ya Morogoro Road kutoka Ubungo Interchange mpaka Mnazimmoja inatakiwa ijengwe upya. Inatakiwa iwe na barabara nane. Barabara au Lanes nne kila upande. Lanes mbili za katikati kwa ajili ya mabasi ya mwendo kasi kila upande. Katika hizo lanes tatu za kila upande, moja ni ya moja kwa moja kutoka Ubungo Interchange mpaka Mnazimmoja au vice versa. Hizo lanes mbili zilizo baki kila upande ni kwa ajili ya magari yanayo pinda kulia au kushoto na magari yanayo ingia kwenye main road.

Morogoro Road kutoka Ubungo Interchange mpaka Mnazimmoja isiwe na trafic Lights. Kwenye intersections ndogo ndogo kama za Magomeni na Fire Brigade, Morogoro Road inapita juu na hizo nyingine zinapita chini. Nazo zina kuwa na interchanges, lakini bila flyovers. (Angalia picha)
SmartSelect_20181211-061057_Google.jpeg

20181211_073518.jpeg


Njia za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu kila upande. Vivuko vyote vya waenda kwa miguu lazima viwe juu. (Angalia picha)
SmartSelect_20181211-061456_Google.jpeg

SmartSelect_20181211-074339_Earth.jpeg

SmartSelect_20181211-075818_Earth.jpeg


Kazi hizi za kutengeneza intersections au interchanges kama za Magomeni na Fire Brigade hazihitaji makampuni kutoka nje. Wahandisi wetu na makadarasi wetu wanaweza kufanya hizi kazi I am sure, wanatakiwa wawe na vifaa muhimu kama Tanroad na makampuni mengine.
Kinacho takiwa hapa ni usimazi mzuri. Wasimamizi wanatakiwa wajue nini kina endelea na sio wale walio somea miembeni.

Asanteni sana.
SmartSelect_20181211-061456_Google.jpeg
SmartSelect_20181211-061057_Google.jpeg
SmartSelect_20181211-061456_Google.jpeg
 
Endelea hivo hivo waweza pata hata nafasi ya kibarua hapo mradi ukianza.....
 
Endelea hivo hivo waweza pata hata nafasi ya kibarua hapo mradi ukianza.....
Mkuu ushauri wangu huo hauhusiani chochote na kutafuta kibarua wala kazi au kutaka kukuza profile yangu. Cha kujiuliza hapa ni kwamba hiyo project ikiisha ni nani atanufaika nayo?

Wajapani ambao ni wafadhili na wajenzi wa hiyo interchange, kulingana na maelezo niliyo yapata kama ni sahihi, sio miungu wao. Ni binadam kama sisi. Wana akili kama sisi na wamesoma na kukariri symbols na principles zile zile ambazo hata sisi tumezipitia. Tofauti tulio nayo ni kuwa wao wameamua kuzitumia hizo symbols, principles na formulars za mahesabu na physics walizo jifunza na kukariri kwenye kutatua matatizo ambayo kama binadam tunakabiliana nayo.

Sasa kama sisi tumesoma na kukariri hayo madudu kwa ajili ya kupata vyeti vya mapambo kwa ajili ya nyumba zetu ni tatizo letu, sio lao. Na mimi kama mtumiaji wa hiyo interchange na barabara na ndiyo mlipaji wa gharama ya za ujenzi wa project hiyo, nina haki ya kusahihisha conditons ambazo zimewekwa kulingana na matakwa yetu. Kwa sababu nataka kitu kinacho ni fiti mimi au sisi na sio wao.

Mkuu usiwe kila wakati unakuwa so intimidated na wazungu au watu weupe. Jiamini kwa kile ulicho nacho. Usiwe na mawazo na fikra ya kutaka kufanya kitu kwa ajili ya sifa au kwa ajili ya kutaka kupata kitu. Fanya kitu kwa hiari na sio kila mara kusubiri kuambiwa nini cha kufanya. Kama Mimi ningetaka kazi kwenye hiyo project ningekuwa nimesha watafuta wahusikia na kupeleka maombi yangu ya kazi kwao.

Watu kama wewe mkuu nawasikitikia sana. Kama umeenda shule na kupata shahada au asta shahada ya chuo, halafu una kuja kuwa na fikra potofu kama hizo, mimi najiuliza kwa nini sasa uliamua kupoteza mda wako wote huo mwingi shuleni na vyuoni? Si ungetumia muda wako vizuri kufanya vitu vingine ambavyo vingekusaidia zaidi?

Ombi langu kwako. Jitahidi kubadilsha mindset yako na ya jamii inayo kuzunguka ili usiwe ndiyo mtu ambaye mpaka leo anakubali kuwa mzungu ndiye mtu wa kwanza aliye ugundua mlima Kilimanjaro. Kama yeye aligundua huo mlima, wale watu walio kuwa wanaishi kando kando ya huo mlima je? Ina maana wao walikuwa hawana macho ya kutambua kuwa hicho wanacho kiona ni mlima na kileleni kuna barafu? Don't be intimidated and be oppressed by white people.

Usione kwamba kila kitu wanacho kifanya na kukingundua wazungu ni sawa. No, ulimwengu hauko hivyo. Zamani labda ndiyo kwa sababu tulikuwa hatujapanuka kimawazo, lakini sio leo.

Wazungu hawakuanza na majawabu ya maisha ya kisasa, isipokuwa Alexandria ambayo ukiangalia kwenye ramani utaona huo mji uko Afrika, wakaja wakatago nao pia ni Afrika tunisia, wakaja wagiriki, warumi na hivi sasa mataifa mengine ya kizungu na waasia. Sisi waafrika kidogo tuko nyuma lakini tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu. Sio rahisi kwetu, kwani kuna wakoma kama wewe ndiyo wanaturudisha nyuma.
 

Attachments

Back
Top Bottom